Call for artists 2015

 
 
CALL FOR ARTISTS ADVERT
  • Je muziki wako ni wa laivu?

  • Je muziki wako umehusiana na Africa, Uarabuni au nchi za bahari hindi?

  • Je umevutiwa kupiga muziki mwezi ujao wa Februari Zanzibar?

  • Kama unaweza kujibu ndio, ndio, ndio - basi endelea kusoma...

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote.

Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 400 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jupiter & Okwess International, Joel Driscoll and Sekou Kouyate, Cheikh Lo, Khaira Arby, Mokoomba, Samba Mapangala & Orchestra Virunga, Nneka, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate, Jagwa Music, Fredy Massamba, Thandiswa, Culture Musical Club, Orchestre Poly Rythmo na wengineo wengi. Tamasha huchukuwa vikundi vya wasanii wanaoncheza muziki wa laivu tu.

MWISHO wa kupokea maombi - 31 Julai 2014

Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri, malazi,chakula na matumizi madogo madogo. Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri

Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2015. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa

Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2016

Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi yaliyokamilika kutoka kwako kabla ya tarehe ya MWISHO ya kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:

  • form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
  • nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
  • picha moja au mbili(Picha zinaweza kutumwa kwa journey@busara.or.tz)

Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini. Vitu vyote vitakavyotumwa lazima viaandikwe FOR PROMOTIONAL USE ONLY. Bonyeza hapa kwa fomu ya maombi.

Call for Artists 2015

Busara Promotions

by post

in person

Busara Promotions

PO Box 3635

Zanzibar

Tanzania

Airport Road , opposite Golf Club. Maisara, Zanzibar, Tanzania