wito kwa filamu za muziki
Mpango wa filamu za muziki wa kiafrika wa siku nne katika tamasha la Sauti za Busara huonesha filamu za muziki ndefu na fupi pamoja na video kama kiongezeo cha show za live za wasanii kwenye jukwaa juu, Mara iliyopita sehemu ya kukaa ya amphitheatre ilibadilishwa kuwa nafasi kwa ajili ya sinema ya muziki wa kiafrika ambapo washabiki na wapenda tamasha hukusanyika pamoja kuangalia filamu saba za kiafrika kuona filamu nyingi zinavyo kusanywa kutoka afrika.
Sauti za Busara inatafuta filamu ndefu pamoja na filamu fupi fupi zenye kusisimua kutoka bara la afrika, ambazo zitakuwa zikionyeshwa kuanzia saa moja wakati wa tamasha mwezi wa pili. Filamu hizi ziwe kivutio na kiburudisho katika bara la Afrika. Hii inaweza kuwa ni ala za muziki na video, burudani zilizonakiliwa, kimsingi tunatafuta:
Mwisho wa kutuma maombi ni: 30 September 2011
Maombi yako yatashughulikiwa ikiwa tutapokea maombi pamoja na kopi mbili za filamu yako kabla ya tarehe 30 September 2011.
Waombaji wote watajulishwa maamuzi ya jopo la uchaguzi ifikapo mwezi November.
Jinsi ya kutuma maombi ni rahisi...
Hatua ya kwanza :
Jaza:fomu hii ya maombi.
Hatua ya pili:
*Njia ya kutufikia mpaka mlangoni
Ofisi ya Busara Promotions, Tumetizamana na Golf Club, Maisara, Njia iendayo uwanja wa ndege, Zanzibar, Tanzania
*kwa njia ya posta
Busara Promotions, PO Box 3635, Stone Town, Zanzibar, Tanzania
Hatua ya tatu:
Tuma picha au filamu zenye ubora kupitia barua pepe ifuatayo busara@busara.or.tz