Busara symbol - click for home page

Facebook

Find the official
Sauti za Busara
group on Facebook

 

Principal Sponsor

Zantel logo

 

Main Sponsors

Ford Foundation

Ford Foundation

SDC
British Council
Embassy Netherlands

Embassy of the Kingdom of the Netherlands

Norwegian Embassy
Goethe Institut
CULTURES FRANCE
 

logo sponsors

ZanAir logo
Memories of Zanzibar logo
Wahapahapa logo
Gallery Tours
UNESCO logo
 

media sponsors

fROOTS
ZG Design
TBC1


 

Festival Party Sponsor

Kendwa Rocks


 

with thanks to

Dhow Countries Music Academy, Alliance Française de Nairobi, Embassy of Germany, Faculty of Arts and Science (EA) - Aga Khan University, Fly540.com, Stone Town Café, Mercury’s Restaurant, Archipelago Café & Restaurant, Clove Hotel, Kidude Café Restaurant, Tabasam Tours, Zanlink, Tower Top at 236 Hurumzi, Hakuna Matata Beach Lodge , Monsoon Restaurant, Serena Inn, Chavda Hotel, Southern Sun DSM, Malindi Guest House, Ultimate Security, ScreenStation (UK), Linear Velocity, Footcandles, 1time airline, National Arts Council of Namibia, www.zanzibar.net,

Thanks also to: Ministry for Information, Culture & Sports, and to all the people of Zanzibar:
"Shukurani kwa kukubali kuwa tamasha hili ni letu sote na mchango wenu ndio ambao umelifanikisha."

Zantel Advert

SzB logo Sauti za Busara 2009

Music Festival, Zanzibar

12 - 17 February 2009

English version >>>

Mtanange wa sita wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 12 hadi 17 Februari 2009; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya machweo.

2009
festival
programme
72 page
booklet

(PDF 4.2mb)

Festival Programme

Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.

Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea.

CLICK HERE - FOR LATEST PICTURES AND BLOG REPORTS

Wasanii watakaoshiriki

(angalia 10 bora hapa)

Samba Mapangala & Orchestra Virunga (Kenya / DRC)Natacha Atlas (Egypt / UK)Msondo Ngoma Band (Tanzania)Oudaden (Morocco)Jagwa Music (Tanzania)Joh Makini (Tanzania)Comrade Fatso  & Chabvondoka (Zimbabwe)TY (UK)Culture Musical Club (Zanzibar)Bi Kidude (Zanzibar)Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar)Wahapahapa Band (Tanzania)The Moreira Project (Mozambique / South Africa)Katapila ‘Sangula’ Ngoma (Tanzania)Elemotho (Namibia)Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte)Mamillion (South Africa)Segere Original (Tanzania)Carola Kinasha & Shada (Tanzania)Mutinda (Kenya)Sansa Troupe (Uganda)Swahili Encounters (Zanzibar / Various)Best of WaPi 2009 (Pan Africa)Iddi Achien'g (Kenya)Rachel Magoola (Uganda)Omega Bugembe Okello (Uganda / USA)Safar (Zanzibar)DJ Yusuf (UK / Zanzibar)Zinduka Ngoma (Zanzibar)Kiumbizi (Pemba)Jang’ombe Nursery School (Zanzibar)Tarbia (Zanzibar)Zimamoto (Zanzibar)DJ Side (Zanzibar)

Nani na lini

"This year’s musical feast is richer and tastier than ever. As always our main focus is to showcase the wealth and variety of East African music - up coming and established groups; acoustic and electric; innovative and classic; from city and shamba. We also welcome visiting performers from across Africa: from Cape Town to Cairo, from Casablanca to Comoros, all bringing their flavours to the mix."

Yusuf Mahmoud, Festival Director

Samba Mapangala

Samba Mapangala & Orchestre Virunga (DRC / Kenya)

"Mwanandege" umbrella dancers

Matembezi ya Ufunguzi

Kama ilivyo ada kutakuwa na matembezi ya ufunguzi wa tamasha siku ya tarehe 12 Februari, matembezi hayo yataambatana na burudani za Beni, Mwanandege, Ngongoti, wachezaji na wanasarakasi. Mkusanyiko huo utawasili maeneo ya Forodhani nyakati za saa kumi na moja alasiri na kuingia ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe.

Burudani kutoka Afrika chini ya anga

Kuanzia siku ya Alhamisi mpaka Jumapili, kutakuwa na burudani ya vikundi kumi kila siku. Wasanii wakubwa wataonyeshana kazi na wale wanaochipukia. Kwa pamoja tuna mseto wa vikundi thelathini kutoka Zanzibar, Tanzania bara na Afrika Mashariki. Vikundi hivi ni mchanganyiko wa vile vya muziki wa asili, vionjo mchanganyiko na ule wa kileo. Vilevile kuna vikundi vingine kumi kutoka Komoro, Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia, DRC, Morocco, Misri, Nigeria na Uingereza.

Mtiririko wa maonyesho ya muziki ni wa “Bandika Bandua” yaani ni onyesho moja baada ya lingine. Maonyesho yote huanza wakati wa jioni, muda ambao joto la jua linapoanza kupungua, mara nyingi kundi la mwisho hupanda stejini nyakati za saa sita ya usiku.

Sekembuke

Jukwaa kuu

Jukwaa kuu la burudani lipo eneo la Mji Mkongwe, ndani ya ukumbi wa kihistoria wa Ngome Kongwe (upande wenye majani) na juu upo wazi. Kipindi cha tamasha ukumbi huu hupambwa kwa rangi mbalimbali, na pia kunakuwa na vibanda ishirini kwa ajili ya huduma za vinywaji, chakula, uuzaji wa nguo, bidhaa za kisanii, pamoja na kanda na CD za wanamuziki mbalimbali.

Pirika pirika ni nyingi kila siku ya tamasha ndani ya ukumbi huu, wenyeji na wageni wa rika, tamaduni na jinsia mbalimbali hujazana kwa wingi. Muda wa jioni kunakuwa na watoto na familia nyingi katika hali ya furaha na bashasha, wadau mbalimbali wa sanaa na utamaduni kutoka kona mbalimbali hubadilishana mawazo. Giza linapoingia wapenda muziki nao hujifaragua na kujirusha kutokana na mirindimo ya muziki na burudani mahiri.

Old Fort, Stone Town

Kila mtu anakubali kwamba kipindi nyoyo ya kila mhudhuriaji hukongwa kutokana na mandhari ya tamasha, na Sauti za Busara huthibitisha kuwa ni “tamasha rafiki zaidi duniani!”

Tiketi na viingilio

Kiingilio ni bure kila siku kuanzia saa kumi jioni hadi machweo. Baada ya hapo utahitajika kuwa na tiketi au pasi maalum ya kuingilia. Bei zinatofautiana baina ya wageni, wakaazi na. Kwa wanaopendelea kukaa kwenye viti kuna tiketi maalum za VIP.

Take One Home  - Souvenir t-shirts

Souvenir T-shirts

We are very grateful to East Africa's low cost airline FLY540.COM for stepping in at the last minute to sponsor the souvenir t-shirts.

Fly540.com

location says it all

Usafiri Na Malazi

Kwa mahitaji yako yote ya usafiri na malazi hapa Zanzibar pamoja na usafiri wa anga kwa Afrika, tunafurahi kukufahamisha kuwa wasiliana na Tabasam Tours iliyopo Zanzibar. Wao wanatoa huduma za uhakika za usafiri wa kwenda na kurudi uwanja wa ndege, maandalizi ya malazi na pia unaweza kupata pasi ya siku nne ya tamasha kupitia kwao.

Na zaidi ni kwamba kutakuwa na punguzo la asilimia 5 kwa wale watakaowatumia Tabasam Tours kufanya taratibu zao za malazi. Ulizia "Busara Discount".

Usafiri Na Malazi>>>

Sherehe ya kumalizia tamasha

Siku ya mwisho wafanyakazi wa tamasha, baadhi ya wasanii na wale wote wanaopenda kwa pamoja tutaelekea katika moja ya fukwe murua Zanzibar. Huko kutakuwa na ma-DJ, wacheza sarakasi, vikundi mbalimbali vya muziki na hivi ndivyo tutakavyohitimisha karamu yetu kwa mwaka 2009.

Shughuli hii imepangwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 17 Februari, Kendwa Rocks.

Sherehe ya kumalizia tamasha>>>.

Finale Party
Busara Xtra

Kumbuka kuwa, siyo sisi pekee. Zanzibar ina maeneo mengine mengi ambako matukio kedekede hufanyika kwa mfano katika mahoteli, migahawa na kumbi mbalimbalii. Hii tumeibatiza jina la “Busara Xtra” na tutafanya kila jitihada kukufahamisha yale yote yatakayojiri.


Pictures:

See photos from Sauti za Busara 2009 >>>

Bi_Kidude_Zanzibar_by_Eirik_Folkedal_DSC_8530_HR Mohamed_Ilyas_by_Eirik_Folkedal_DSC_8407_HR Rachel_Magoola_Uganda_by_Masoud_Khamis_1012707 Rukia_Ramadhan_in_Safar_Zanzibar_by_Masoud_Khamis_1011583
TY_UK_by_Eirik_Folkedal_DSC_7870_HR _Carnival_Parade_arrives_by_Pernille_Baerendtsen_IMG_7066 _Carnival_Parade_arrives_by_Pernille_Baerendtsen_sauti_za_busara_03 __audience_by_Eirik_Folkedal_DSC_8376_HR

 

also, some great pix at:

Jeremy Llewellyn-Jones Gallery

Jonathan Littlejohn Gallery


Video:
  • YouTube logo See 10 minutes of video highlights

Text:

this site is hosted by Zanzibar.NET