Busara symbol - click for home page

Facebook

Find the official
Sauti za Busara
group on Facebook

 

Principal Sponsor

Zantel logo

 

Main Sponsors

Norwegian Embassy
HIVOS - people unlimited
UN Joint Programme
Goethe Institut
British Council
CULTURESFRANCE
US Embassy, DSM
 

logo sponsors

Memories of Zanzibar logo
ZanAir logo
Gallery Tours
FLY540.COM
 

Festival Party Sponsor

Zanzibar Hotel Group at Sau Inn, Jambiani

 

media sponsors

fROOTS
ZG Design

with thanks to

NMB Ltd, United Petroleum, Alliance Française de Nairobi, Embassy of Germany, Ultimate Security, SMOLE 2 Project, Tabasam Tours, Dhow Countries Music Academy, Stone Town Traders, Southern Sun DSM, Embassy of Denmark, Stone Town Café, Mercury’s Restaurant, Archipelago Café & Restaurant, Monsoon Restaurant, Clove Hotel, Zanlink, ChuChu FM 90.9, ZG Films, Linear Velocity, Footcandles, www.zanzibar.net

Thanks also to: Ministry for Information, Culture & Sports, and to all the people of Zanzibar:
"Shukurani kwa kukubali kuwa tamasha hili ni letu sote na mchango wenu ndio ambao umelifanikisha."

Zantel Advert

SzB logo Sauti za Busara

Music Festival, Zanzibar

11 - 16 February 2010

English version >>>

Mtanange wa saba wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka ilikuwa ni kuanzia tarehe 11 hadi 16 Februari 2010.

Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.

Wito kwa wasanii 2011 >>> Matamasha bora afrika - gonga hapa >>> 2010 PICHA - na maelezo zaidi >>>

Wasanii walioshiriki

Thandiswa (South Africa)  Ba Cissoko (Guinea)  Malick Pathé Sow (Senegal)  Fresh Jumbe & African Express (Tanzania / Japan)  Simba & Brown Band (Mozambique)  Banana Zorro & the B Band (Tanzania)  Chidi Benz (Tanzania)  Mim Suleiman (Zanzibar / UK)  Nyota Ndogo (Kenya)  Del & Diho (Mayotte)  Makadem (Kenya)  Mari Boine (Norway)  Dawda Jobarteh (The Gambia)  Jhikoman (Tanzania)  Mzungu Kichaa (Tanzania / Denmark)  Massar Egbari (Egypt)  Sinachuki Kidumbak (Zanzibar)  Debo Band (Ethiopia / USA)  Joel Sebunjo  (Uganda)  Bamba Nazar & The Pilgrimage (Suriname / Netherlands)  Maia & the Big Sky (Kenya)  Tausi Women's Taarab (Zanzibar)  Swahili Encounters (Zanzibar / Various)  Shirikisho Sanaa Group (Zanzibar)  Kilua Ngoma (Tanzania)  Swifatui Abraar Group (Tanzania)  DJ Eddy (Zanzibar)  DJ Yusuf (UK / Zanzibar)  Sowers Group (Tanzania)  Maureen Lupo Lilanda (Zambia)  Best of WaPi (Tanzania)  Sosolya Dance Academy (Uganda)  Mapacha Africa (Kenya)  KVZ Tupendane (Pemba)  na wengineo.

Kitabu cha Tamasha

pata PDF (4MB)

Ratiba ya Tamasha

timetable

pata kurasa za katikati
za PDF (270k)

Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea.

"This year’s musical feast is richer and tastier than ever. As always our main focus is to showcase the wealth and variety of East African music - up coming and established groups; acoustic and electric; innovative and classic; from city and shamba."

Yusuf Mahmoud, Festival Director

"Mwanandege" umbrella dancers

Matembezi ya Ufunguzi

Kama ilivyo ada kutakuwa na matembezi ya ufunguzi wa tamasha siku ya tarehe 11 Februari, matembezi hayo yataambatana na burudani za Beni, Mwanandege, Ngongoti, wachezaji na wanasarakasi. Mkusanyiko huo utawasili maeneo ya Forodhani nyakati za saa kumi na moja alasiri na kuingia ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe.


Burudani kutoka Afrika chini ya anga

Kuanzia siku ya Alhamisi mpaka Jumapili, kutakuwa na burudani ya vikundi kumi kila siku. Wasanii wakubwa wataonyeshana kazi na wale wanaochipukia. Kwa pamoja tuna mseto wa vikundi thelathini kutoka Zanzibar, Tanzania bara na Afrika Mashariki. Vikundi hivi ni mchanganyiko wa vile vya muziki wa asili, vionjo mchanganyiko na ule wa kileo. Vilevile kuna vikundi vingine kumi kutoka la nchi za Afrika.

Mtiririko wa maonyesho ya muziki ni wa “Bandika Bandua” yaani ni onyesho moja baada ya lingine. Maonyesho yote huanza wakati wa jioni, muda ambao joto la jua linapoanza kupungua, mara nyingi kundi la mwisho hupanda stejini nyakati za saa sita ya usiku.

Sekembuke

Jukwaa kuu

Jukwaa kuu la burudani lipo eneo la Mji Mkongwe, ndani ya ukumbi wa kihistoria wa Ngome Kongwe (upande wenye majani) na juu upo wazi. Kipindi cha tamasha ukumbi huu hupambwa kwa rangi mbalimbali, na pia kunakuwa na vibanda ishirini kwa ajili ya huduma za vinywaji, chakula, uuzaji wa nguo, bidhaa za kisanii, pamoja na kanda na CD za wanamuziki mbalimbali.

Pirika pirika ni nyingi kila siku ya tamasha ndani ya ukumbi huu, wenyeji na wageni wa rika, tamaduni na jinsia mbalimbali hujazana kwa wingi. Muda wa jioni kunakuwa na watoto na familia nyingi katika hali ya furaha na bashasha, wadau mbalimbali wa sanaa na utamaduni kutoka kona mbalimbali hubadilishana mawazo. Giza linapoingia wapenda muziki nao hujifaragua na kujirusha kutokana na mirindimo ya muziki na burudani mahiri.

Old Fort, Stone Town

Kila mtu anakubali kwamba kipindi nyoyo ya kila mhudhuriaji hukongwa kutokana na mandhari ya tamasha, na Sauti za Busara huthibitisha kuwa ni “tamasha rafiki zaidi duniani!”

Tiketi na viingilio

Kiingilio ni bure kwa wale watakao ingia kabla ya saa kumi na moja jioni. Baada ya hapo utahitajika kuwa na tiketi au pasi maalum ya kuingilia. Bei zinatofautiana baina ya wageni, wakaazi na. Kwa wanaopendelea kukaa kwenye viti kuna tiketi maalum za VIP.

location says it all

Usafiri Na Malazi

Kwa mahitaji yako yote ya usafiri na malazi hapa Zanzibar pamoja na usafiri wa anga kwa Afrika, tunafurahi kukufahamisha kuwa wasiliana na Tabasam Tours iliyopo Zanzibar. Wao wanatoa huduma za uhakika za usafiri wa kwenda na kurudi uwanja wa ndege, maandalizi ya malazi na pia unaweza kupata pasi ya siku nne ya tamasha kupitia kwao.

Na zaidi ni kwamba kutakuwa na punguzo la asilimia 5 kwa wale watakaowatumia Tabasam Tours kufanya taratibu zao za malazi. Ulizia "Busara Discount".

Usafiri Na Malazi>>>

Sherehe ya kumalizia tamasha

Tarehe 16 jumanne siku ya mwisho wafanyakazi wa tamasha, baadhi ya wasanii na wale wote wanaopenda kwa pamoja tutaelekea katika moja ya fukwe murua Zanzibar. Huko kutakuwa na ma-DJ, wacheza sarakasi, vikundi mbalimbali vya muziki na hivi ndivyo tutakavyohitimisha karamu yetu kwa mwaka 2010.

Sherehe ya kumalizia tamasha>>>.

 

Finalé Party
Busara Xtra

Kumbuka kuwa, siyo sisi pekee. Zanzibar ina maeneo mengine mengi ambako matukio kedekede hufanyika kwa mfano katika mahoteli, migahawa na kumbi mbalimbalii. Hii tumeibatiza jina la “Busara Xtra” na tutafanya kila jitihada kukufahamisha yale yote yatakayojiri.

 

this site is hosted by Zanzibar.NET


Warning: mysql_free_result(): supplied argument is not a valid MySQL result resource in /home/busara/public_html/festivals/2010/index_swah.php on line 277