Busara symbol - click for home page

Mtiririko wa Picha za 2011
best of 2010
Facebook

Find the official
Sauti za Busara on Facebook

Principal Sponsor

Zantel logo

Main Sponsors

Norwegian Embassy
hivos
GoeTheInstitut
from the american people
ACP Music Festivals network

Logo Sponsors

Memories
cultures france
gallery tour
ZGPH
Grand Malt

Media Sponsors

Memories
See Full List

SzB logo Sauti za Busara 2011

Music Festival, Zanzibar

9 - 13 February 2011

English version >>>

Tarahe ya Tamasha la mwakani: 8 – 12 February 2012 >>> SzB 2011 video highlights >>> Lione vipi tamasha lilivyoenda na habari nyingizo >>> Picha za tamasha la 2011.
 
 

Kidokezo cha video Sauti za Busara 2011

waone wasanii wanoangaliwa sana

Bi Kidude (Zanzibar)
Bi Kidude (Zanzibar)
 
 
 

Wasanii wa 2011

Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin)  Blick Bassy (Cameroon)  Otentikk Street Brothers (Mauritius)  Culture Musical Club (Zanzibar)  African Stars Band (aka Twanga Pepeta) (Tanzania)  Kwani Experience (South Africa)  Jagwa Music (Tanzania)  Mlimani Park Orchestra (Tanzania)  Bi Kidude (Zanzibar)  Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar)  Bismillahi Gargar (Kenya)  Djeli Moussa Diawara (Guinea)  Christine Salem (Reunion)  Yaaba Funk (UK)  Muthoni The Drummer Queen (Kenya)  Jahazi Modern Taarab (Tanzania)  Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden)  Sinachuki Kidumbak (Zanzibar)  Les Frères Sissoko (Senegal)  Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East)  Groove Lélé (Reunion)  Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar)  Swahili Encounters (Zanzibar / Various)  Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various)  Nomakanjani Arts (Zambia)  Percussion Discussion Afrika (Uganda)  Staff Band Namasabo (Tanzania)  NEWS Quartet (Mauritania / Various)  Maureen Lupo Lilanda (Zambia)  Lelelele Africa (Kenya)  Atemi & the Ma3 Band (Kenya)  Black Roots (Zanzibar)  Sauda (Tanzania)  Wanyambukwa Artist Group (Tanzania)  Nyota Kali Band (Tanzania)  Cross Border (Zanzibar / Tanzania)  na wengine wengi.

Nakala ya kitabu

Pata nakala ya kitabu PDF (5mb)

Ratiba ya tamasha

festival timetable

Pata ratiba ya tamasha PDF (70kb)

main stage before the show

Tamasha la muziki la Sauti za Busara, hufanyika  katikati ya mji wa kihistoria Ngome kongwe Zanzibar, huonyesha muziki mbali mbali wa Africa kwa wasanii zaidi ya mia nne wanaoshiriki kwa siku tano.Kila mwaka wakati wa tamasha makuta makongwe ya mambo club hurindima kila watu wakizidi kuongezeka na muziki kupaa angani. Tamasha linakuwa lina vionjo, na matukio ya kuburudisha ya hapa na pale mjini na visiwani mote kama vile maandamano ya ufunguzi.

Muziki wa Afrika – chini ya mawingu ya Afrika.

Kutoka jumatano hadi Jumapili vikundi visivyopungua arobaini hufanya maonyesho laivu kwenye jukwaa kila siku. Majina makubwa hushuka jukwaani  pamoja na wasanii chipukizi. Kuna kiasi cha vikundi thelasini hapa Zanzibar, Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla, na vikundi kumi kutoka nje ya Afrika mashariki vikiwakilisha nchi za Ethiopia, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Afrika kusini, La Renioun, Madagaska, Maurishiz, Ghana, Mali na Senegal.

Muziki wa aina zote hufanya kwa laivu, shoo huanza saa 11 jioni na kuendelea bila kusita ikimalizia kundi la mwisho usiku kati. Kwa wale wenyeji kiingilio ni bure mpaka saa 12 jioni, baada ya hapo kiingilio ni kiasi ya  yuro moja (2000 TSh), watu zaidi elfu tano huhudhuria tamasha kila siku. Fungua bei za tiketi hapa. Asilimia themanini ni watu kutoka katika maeneo ya Afrika mashariki na wengine kutoka Afrika, Asia, Ulaya na kwengineko.

Sauti za Busara ni tamasha linalo fanyika kila mwaka hapa Afrika ya mashariki na limekuwa lijulikana kama “Tamasha rafiki zaidi duniani”.

audience SzB2010

Tamasha la nane la Sauti za Busara litafanyika tarehe 9 mpaka 13 mwezi wa Februari 2011. Likija pamoja na

  • 400 Wanamuziki : Hivyo ni vikundi arobaini, ishirini vikitoka hapa hapa Tanzania, na ishirini kutoka sehemu nyingine za Afrika. Vikundi vya mijini, mashamba, vikundi vinavyotumia vyombo vya umeme, vilivyoanzishwa na vikundi chipukizi.
  • Maandamano ya Ufunguzi :  Maandamano ya tapitayo barabara kuu katika siku ya ufunguzi, ikiwemo ngoma ya beni, ngoma za kienyeji, kikundi cha wanawake cha mwanandege, sarakasi, na viburudisho vingi vya kushangaza. Angalia Maandamano ya Ufunguzi.
  • Swahili Encounters : Siku nne ambazo wasanii hushirikiana, wenyeji walioalikwa, wanamuziki wanaotembelea tamasha hupata muda wa kuzitafsiri nyimbo za kiswahili na kuziwasilisha jukwaani. Angalia Swahili Encounters.
  • Semina za Mafunzo : Kuwajenga wasanii, viongozi, waandishi wa habari, watengeneza filamu, na mafundi wa vipaza sauti na taa kuwa na ujuzi endelevu kutoka hapa Afrika ya mashariki.
  • Waanzilishi wa Sanaa : Makongamano ya kila siku yanayowakutanisha wataalamu wa sanaa wa hapa nyambani na wakigeni.
  • Filamu za Muziki wa Kiafrika : Filamu za muziki za kumbukumbu, filamu ndogo ndogo za muziki, video, na filamu za burudani za laivu.
  • Biashara wakati wa Tamasha : Vinywaji na vywakula vya kienyeji, cd za muziki, mapambo ya dhahabu, nguo, na mengi mengineyo hupatikana ndani ya ukumbi wa tamasha. Fungua fomu ya maombi ya vibanda vya biashara ndani ya ukumbi wa tamasha.
  • Busara Xtra : Wakati wa tamasha Kisiwa cha Zanzibar hurindima na matukio tofauti. Ngoma za kienyeji, ngoma za kudensi, shoo za kiana, mashindano ya ngalawa, viburudisho vya baada ya pati, na burudani za taarabu asilia hupangwa na wenyeji. Angalia Busara Xtra.

audience SzB2010


"Tamasha la Sauti za Busara huwavutia vijana wa kizanzibar na kuwaleta pamoja na utamaduni wao, kutoa nafasi kwa wasanii na wataalamu wa muziki kukutana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja. Kuuweka utamaduni hai, kutoa ajira kwa wenyeji, na kuikuza Zanzibar  kama mfano katika sekta ya utalii-inayoheshimu utamaduni wa kizanzibar."

Yusuf Mahmoud, Festival Director


Photo galleries  / Profiles of all artists who participated during 2004 – 2011 / Video blogs and press coverage Sauti za Busara 2011 / Zanzibar accommodation / Visitor Information / More Top African music festivals in Africa

this site is hosted by Zanzibar.NET