Shindano la nyimbo za amani

Song for Peace Amini ndio Mpango mzima Sauti za Busara Busara Promotions

Shindano la Nyimbo za Amani

Sauti za Busara huleta watu pamoja katika kusherekea: ‘Rangi Tofauti, Watu Wamoja’.

Tunathamini na kutambua Tanzania kua moja ya nchi zenye amani duniani. Mwaka 2015 ukiwa ni mwaka wa uchaguzi nchini Tanzania, tunaamini kwamba ili maendeleo ya taifa yaendelee bila kizuizi, tunahitaji kuimarisha umoja, kuheshimu tofauti, na kutunza na kulinda amani hii yenye thamani.

Katika tamasha la 12, vikundi 19 vitakavyoshiriki vitawakilisha Tanzania, na vikundi vingine 18 vikiwakilisha sehemu mbalimbali barani Afrika na dunianikote. Wakati tunawaleta pamoja wasamii mbalimbali na hadhira kusherekea muziki wa Afrika, Sauti za Busara imeeandaa shidano, na kutoa zawadi ya fedha taslim kama ada ya kurekodi studio itakayotolewa kwa Nyimbo za Amani.

Shindano la Nyimbo za Amani litafanyika katika tamasha la Sauti za Busara litafanyika Mji Mkongwe, Zanzibar kati ya saa 10:00 jioni Alhamisi tarehe 12 na 2:00 usiku siku ya Jumapili tarehe 15 Februari. Shindano liko wazi kwa watanzania au watu wenye asili ya Tanzania.

Together as One: Amani Ndio Mpango Mzima!

  • Vikundi vyote vya Kitanzania vinavyoshiriki katika tamasha vinaalikwa vinakaribishwa kutunga nyimbo MOJA maalum yenye dhima ya amani na umoja, na kuimba nyimbo hii kwenye seti zao katika tamasha.

  • Nyimbo zote zitakazojumuishwa katika shindano lazima ziwe zimetungwa kwa uhalisia na washindani.

  • Ili ziwe na uhalali wa kuingizwa katika shindano hili, Nyimbo zote za Amani lazima ziimbwe live.

  • Ili ziwe na uhalali wa kuingizwa katika shindano hili, Nyimbo zote za Amani lazima ziwe na mashairi ya Kiswahili

  • Jopo la wataalam wa muziki kutoka Tanzania litaamua nyimbo zipi za Amani zenye ubunifu zaidi kushika nafasi ya kwanza, pili na tatu kama zitakavyoimbwa katika tamasha la Sauti za Busara 2015.

  • Washindi watatangazwa katika tamasha usiku wa Jumapili tarehe 15 Februari.

  • Fedha taslim zitatolewa. Hizi zitajumuisha gharama za kutengeneza rekodi za kitaalam studio za nyimbo zilizoshinda: 4/- TSh (Tuzo ya kwanza), 3m/- TSh (Tuzo ya pili) and 2m/- TSh (Tuzo ya tatu).

  • Vigezo vya uamuzi vitajumuisha ujumbe wa mashairi na uwasilishaji, mpangilio wa muziki, usanifu wa kisanii, uhalisi na ubunifu, ujuzi wa kutumbuiza na/au mwitikio wa hadhira.

  • Wakati huo huo wasanii wa kigeni pia wanashauriwa kujumuisha nyimbo za amani na umoja katika maonesho yao ya tamasha, wasanii wenye asili ya Tanzania tu ndio wenye uhalali wa kushiriki katika shindano hili.

Ushiriki katika shindano hili utachukuliwa moja kwa moja kama kukubaliana na Sheria za Shindano.

Unaweza pia kudownload Sheria za Shindano.

Shindano la Nyimbo za Amani linadhaminiwa na Busara Promotions, kwa msaada wa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.

Kwa taarifa mpya tazama www.busaramusic.org and www.facebook.com/sautizabusara