Kanuni za nyimbo za amani

Nyimbo za Amani (Songs for Peace) Kanuni za shindano


Mdhamini wa shindano

Nyimbo za Amani zimedhaminiwa na Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam, na Busara Promotions.

 

Song for Peace

Maelezo ya malengo ya shindano

(Angalia “Vigezo” chini ni nani anastahili kuwa mshindani)

Sauti za Busara huwaleta watu pamoja kusheherekea muziki wa Afrika na kuwasilisha taswila chanya ya Afrika kwa dunia. Tamasha hutoa fursa kwa wasanii wa nyumbani kufikia soko la kimataifa, kongamano la watu kujielezea, kusoma kupitia kwa watu na kuthamini tamaduni mbalimbali.

Tamasha la 12 litafanyika katika Mji Mkongwe, Stone Town, Zanzibar kuanzia tarehe 12 – 15 Februari 2015 likijumuisha vikundi vipatavyo 35, vyote vikifanya maonyesho ya moja kwa moja (Live), asilimia 50 ya vikundi vyote kutoka Tanzania na vingine kutoka bara la Afrika na kwingineko.

Watanzania wa rika zote na historia mbalimbali wanathamini, kufurahi na kujivunia kuwa na nchi ya Amani. Amani hainunuliki, Amani lazima ilindwe hatuwezi kuchukulia kimzaha. Mwakani tutakuwa na uchaguzi mkuu hapa Tanzania, Sauti za Busara itaonyesha suala la AMANI & UMOJA kuwa ndio mada kuu za tamasha.

Vikundi vyote vya Tanzania vitakavyoshiriki tamasha vitaombwa kutunga nyimbo moja maalum ya Amani na au Umoja na kuicheza nyimbo hiyo kipindi cha tamasha.

Jopo la wataalam wa mambo ya muziki watateuliwa kufanya uamuzi wa kuchagua nyimbo bora zenye ubunifu zihusuzo ‘Amani na Umoja’ zitakazochezwa kwenye tamasha. Jopo hilo litajumuisha watu watano kutoka katika sekta za utamaduni kama wanamuziki, waandaaji wa muziki, waandishi wa habari, waalimu wa chuo cha muziki Zanzibar (DCMA) na au wawakilishi kutoka Serikalini.

Ili ustahili kuwa mshiriki wa shindano la nyimbo za Amani lazima nyimbo yako iwe ya Kiswahili.

Wasanii kutoka nje ya Tanzania wataombwa nao kutunga/kuimba nyimbo za Amani katika Tamasha lakini hawatajumuishwa kwenye shindano, ni wasanii wenye asili ya Tanzania tu ndio wanaoruhusiwa ushiriki wa shindano.

Vigezo vya shindano lazima vitolewe/vipelekwe mapema kwa jopo la majaji na wasanii wataoshiriki. Vigezo vya uteuzi vitajumuisha maudhui ya nyimbo, mpangilio wa muziki, ubora wa kisanii, ubunifu na uhalisia, Ustadi wa onyesho na au mwitikio wa watazamaji.

Jopo la majaji litachagua washindi wa watatu wa nyimbo bora za Amani katika tamasha la Sauti za Busara 2015. Washindi watatangazwa siku ya jumapili tarehe 15 Februari.

Tuzo za pesa za Kitanzania zitatolewa. Hii ikiwa kugharamia malipo ya kurekodi kwenye Studio, kama nakala ya kusikiliza (audio) na au Kuona (Video) kwa washindi: Milioni 4 mshindi wa kwanza, Milioni 3 mshindi wa Pili na Milioni 2 mshindi wa tatu.

Washindi watakabidhiwa asilimia 50% ya zawadi kwenye tamasha na asilimia 50% baada ya kuwasilisha nakala yao (CD)

Jinsi ya kuingia

Ushiriki wa shindano hili itachukuliwa moja kwa moja ukikubali masharti ya shindano.

Wimbo utakaowasilishwa lazima uwe umetungwa na muhusika/mshiriki.

Msanii atakubaliwa kuwa mshiriki na kuwa na haki ya kushindana ikiwa atawasilisha mkataba aliosaini kabla ya tarehe 30 Novemba 2014.

Taasisi haitakuwa na haki ya kushiriki kwenye shindano, ikiwa moja kwa moja, au kupitia mwakilishi binafsi. Ili kuhalalishwa ushiriki, mshindani lazima akamilishe na kutoa maelezo sahihi.

Shindano litaanza rasmi siku ya Alhamis, tarehe 12 Februari 2015, saa 10:00 jioni, muda wa Tanzania. Maonyesho lazima yafanyike kwenye tamasha la Sauti za Busara kati ya Alhamis, tarehe12 Februari, saa 10:00 jioni na Jumapili, tarehe 15Februari, saa 1:00 jioni. Jopo la majaji litaanza kazi Alhamis, tarehe 12 Februari 2015, saa 10:00 jioni na kumalizia tarehe 15 Februari 2015 saa 1:00 jioni.

Mahitaji ya maudhui

a. Onyesho la nyimbo ya Amani lazima ipigwe Moja kwa moja (Live) na kwa lugha ya kiswahili, yenye maudhui ya kuchochea muendelezo wa Amani/Umoja. Nyimbo haitakiwi kuwa na ujumbe unaochochea fujo, kuto heshimu, kuudhi, kutukana,kutisha mtu/pande nyingine. Kwa lungha nyingine nyimbo iwe na maudhui yanayofaa kwa dunia nzima.

b. Nyimbo lazima iwe imetungwa na mshindani na isiwe na viashiria kwamba inamilikiwa na mtu/tassisi nyingine chini ya sheria za haki miliki.

c. Jopo la majaji lina haki pekee ya kufelisha kikundi chochote ambacho nyimbo/onyesho lao haliendani na na sheria za shindano.

d. Kikundi lazima kithibitishe kwamba kimesajiliwa chini ya BASAZA na au BASATA. Kikundi lazima vilevile kithibitishe kwamba kipo tayari kutoa nyaraka mbalimbali za uthibitisho pindi zitakapohitajika.

Mahitaji ya Kiufundi

a. Kikundi lazima kitume mahitaji yao ya kiufundi kabla ya uthibitisho wa ushiriki wao.

b. Tamasha litatoa mahitaji ya kiufundi yaliyopo ndani ya uwezo wao.

c. Maonyesho ya nyimbo za Amani yatarekodiwa moja kwa moj, kwa nakala za kusililiza (Audio) na au kuona (Video)

Uhakiki

a. Vikundi vitakavyoshiriki lazima viwe vya Tanzania, au watu wenye asili ya Tanzania. Ruhusa za wazazi au walezi zinahitajika kwa watoto walio na umri chini ya miaka 18.

b. Watu/taasisi zifuatazo hazitaruhusiwa kushikiri kwenye shindano hili, watu/taasisi yenye uhusiano na Serikali ya Marekani kama waajiriwa, Maafisa wa mashirika ya Marekani, Wanafunzi, Wakurugenzi au wakala yoyote kujihusisha katika uongozi, matangazo, ubunifu, uamuzi na au suala lolote linalohusu shindano, na au mke, mume, mchumba, mtoto, ndugu na ambao wanaishi nyumba moja na watu hao.

Uteuzi wa washindi

a. Jopo la majaji lenye utaalamu na muziki wa Tanzania watafanya uteuzi wa nyimbo bora za kuhamasisha “Amani na Umoja” zenye ubunifu. Jopo litashirikisha viongozi kutoka sekta za kiutamaduni wakiwemo wasanii, waalimu kutoka Chuo cha Muziki Zanzibar (DCMA) na au wawakilishi kutoka Serikalini.

b. Jopo litakuwa na kazi ya kuchagua nyimbo bora 3 za “Amani na Umoja” katika tamasha la Sauti za Busara 2015

c. Tuzo zitatolewa siku ya jumapili ya tarehe 15 Februari 2015

Zawadi

a. Zawadi ya pesa itatolewa, ikiwa itagharamia malipo Zawadi ya pesa itatolewa, ikiwa itagharamia malipo ya kufanykufanya rekodi zenye ubora milioni 4 mshindi wa kwanza, milioni 3 mshindi wa pili, milioni 2 mshindi wa tatu.

b. Washindi wote watapatiwa asilimia 50% ya zawadi na nusu yake italipia gharama za kurekodi a u kwa msanii pindi atakapoleta nakala yake aliyorekodi, katika kipindi kisichozidi, tarehe 30/04/2015.

c.Kodi zote juu ya au zinazohusiana na tuzo yoyote, na matokeo ya uwasilishwaji huo, ni jukumu la kipekee la mshindi.

d. Nyimbo zitakazoshinda zitawekwa kwenye kurasa ya Facebook ya Sauti za Busara na au Ubalozi wa Marekani.

Kanuni za tamasha la Sauti za Busara

a. Wasanii wote ambao wapo tayari kushiriki kwenye mashindano ya nyimbo za Amani wanatakiwa wathibitishe ushiriki wao kwa barua pepe, itumwe Busara Promotions kabla ya tarehe 30 Nevemba 2014.

b. Busara Promotions imekubali kutoa huduma zote kwa wasanii kulingana na vipengele vilivyoainishwa kwenye mkataba wake na msanii amekubali kutoa huduma husika. Mpango wa tamasha utatoa maelezo ya kina yatakayotolewa kwa wasanii pindi yatakapokuwa tayari.

c. Msanii atatengewa muda wa majaribio ya sauti na onyesho yatakayoainishwa kwenye mkataba hapo baadae, maelezo yote muhimu kwenye (kiambatanisho 1). Msanii atakuwa na ruhusa ya kuwa eneo la jukwaa na vifaa vya muziki kwa kipindi cha majaribio ya sauti na onyesho tu. Uchelewaji wa kufika utasababisha kusitishwa kwa majaribio ya sauti na malipo ya onyesho.

d. Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa. Hivyo tunasisitiza wasanii wote kufanya maonyesho yao moja kwa moja (Live). Ikiwa msanii anataka kupiga kwa kutumia CD (playback) inabidi ruhusa ipatikane mapema na anaweza kuruhusiwa kwa kutumia vifaa tu. Ikiwa msanii ataonekana kukaidi agizo hilo, papohapo atashushwa kwenye jukwaa na kupoteza haki zake zote ikiwemo malipo ya onyesho.

e. Busara Promotions itahakikisha inatoa ulinzi wa kutosha kuhakikisha hakuna mtu asiyehusika anakuwepo kwenye sehemu ya jukwaa au nyuma ya jukwaa katika eneo la tamasha. Wasanii na wafanyakazi wa wasanii wanahitajika kufuata maelekezo yatakayotolewa na walinzi wa tamasha. Msanii anahusika na usalama wa vifaa vyovyote ambavyo vimeachwa bila ya uangalizi ndani ya eneo la tamasha isipokuwa jukwaani na nyuma ya jukwaa.

f. Busara Promotions itatumia mfumo wa vibali ili kudhibiti uwepo wa watu wasiohusika kwenye eneo la jukwaa na nyuma ya jukwaa . Wasanii watahakikisha mada ya mkataba na Busara Promotions, wasanii wote kwenye kikundi, mameneja, mafundi wanasajiliwa katika mfumo wa vibali kabla ya tarehe 31 Januari 2015. Wasanii wanatakiwa wawe na pasi zao muda wataokuwepo eneo la ukumbi wa maonyesho.

g. Wasanii wamekubali kupigwa picha, kurekodiwa kwa sauti (audio) na picha (video) wakati wa onyesho lao. Busara Promotions inawajibika kutoa vibali kwa waandishi wa habari ambao wataruhusiwa kurekodi maonyesho ya wasanii na hata matukio mengine. Tamasha litachagua na kutoa vibali kwa wawakilishi ambao wanauhakika na matumizi ya vitu watavyovirekori kutumika ipasavyo kwa faida ya tamasha na wasanii/msanii husika. Pindi wataalam wakifanya kazi kwa niaba ya Busara Promotions, tamasha litatumia nakala kusambaza taarifa kulingana na asili ya nyaraka husika, kama taarifa kuhusu tamasha na wasanii wajao. Wasanii wameikubalia Busara Promotions kurekodi nyimbo mbili tu kwa ajili ya matangazo na si baishara, ikiwemo nyimbo ya Amani.

Wajibu na haki

a. Mdhamini wa shindano hana ulazima kuidhinisha nyimbo au ujumbe uliotolewa kwenye nyimbo, mdhamini hatajihusisha na hali yoyote ya kimigongano itakayohusisha ushirikishwaji wa baadhi ya washiriki kwenye maonyesho.

b. Shindano halitaruhusu ukiukwaji ya haki miliki au ukiukwaji wowote wa mmiliki halali, jopo la majaji lina uwezo wa kufelisha nyimbo yoyote inayoonekana kukiuka haki miliki ya upande mwingine

c. Washiriki lazima wame wamiliki halali wa nyimbo zitakazowasilishwa. Nyimbo hubaki kuwa mali ya mshiriki, na mdhamini wa shindano na Serikali ya Marekani haitadai hati miliki kwa mshiriki yoyote aliyekuwepo kwenye mashindano. Washiriki wamekubali kumpa madhamini wa shindano nyimbo zilizowasilishwa kwa ajili mchakato wa shindano. Washindi wanatakiwa wampatie mdhamini wa shindano kumkubalia kutumia nyimbo zao ulimwengu mzima, kuzitengeneza upya, kuzisambaza/kuonyesha kwenye vyombo vya habari mbalimbali kulingana na muingiliano na utendaji wa shindano.

d. Mshiriki lazima akubali kwamba ana jukumu la kuwasilisha mahitaji kwa ajili ya onyesho lake la shindano

e. Mdhamini wa shindano ana haki ya kuthibitisha uhalali wa mshiriki na njia za ushiriki na kumfelisha mshiriki yeyote ambaye anaonekana hajafuata sheria rasmi za shindano. Mdhamini wa shindano ana haki ya kuomba nyaraka kwa hiari ili kuthibitisha na kuhakiki na kulingana na sheria rasmi za shindano.

f. Ikiwa zawadi au baadhi ya sehemu ya zawadi haijapatikana, Mdhamini wa shindano ana mamlaka ya kubadilisha zawadi yenye kulingana au kubwa zaidi ya zawadi iliyotangazwa.

g. Mdhamini wa shindano ana mamlaka ya kumfelisha mshiriki yeyote ambaye anaonekana (i) amekiuka sheria rasmi za shindano au (ii) ameonyesha utovu wa nidhamu au votendo vyenye kila dalili za kumtisha, kumtukana au kumsumbua mtu mwingine yoyote.

h. Mdhamini wa shindano ana haki ya kuboresha, kuahirisha au kusitisha kabisa shindano kwa uamuzi wake na kwa sababu yoyote.

i. Washiriki wa shindano wamekubali kulinda na kutodhuru upande wa mdhamini wa shindano, ndugu, kampuni tanzu, maofisa, wakurugenzi, waajiriwa, wafanyakazi na mawakala, dhidi ya madai, uharibifu, wajibu, hasara, gharama au madeni na matumizi (ikijumuisha lakini isiyo na kikomo kwa malipo ya mwanasheria/wakili) yatakayotokana na (i) ukiukwaji wa kanuni za shindano (ii) ukiukwaji wa haki zozote za shirika mwenza zikiwemo za hati miliki, mali akili, faragha, utangazaji au haki nyingine za kimiliki zenye mahusianon na shindano; au (iii) madai yoyote kwamba ombi/maombi yameleta madhara yoyote, yakiwemo ya kifedha kwa shirika mwenza lolote. Sheria hizi zitaendelea kuwepo kwa muda usiojulikana baada ya kumalizika kwa shindano hili.

j.Shughuli za utoaji wa zawadi zitaendana kwa mujibu wa sheria za Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama kutatokea migongano ya kisheria kati ya Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi nchi inayofanyika mashindano sheria zake zitatumika.

k. Waandaaji wa shindano watachukua hatua stahiki katika kulinda taarifa muhimu za washiriki. Taarifa za mawasiliano zilizotolewa zinaweza kutumika baadae kwa ajili ya shughuli zingine. Mawasiliano hayo yanaweza kutumiwana mdhamini wa tamasha na au mtu/taasisi nyingine ikikubalika kisheria.

l. Mdhamini wa shindano hana jukumu wala dhima kwa hasara atakayoipata mshiriki au kushindwa kutumia vifaa vya ufundi au upatikanaji wa taarifa za ushiriki wa shindano. Wadhamini wa shindamo hawana dhamana juu ya matatizo ya vifaa kwa hali yoyote itakayojitokeza wakati shindano, au ukosefu wa barua pepe kwa ajili ya mawasiliano yahusuyo shindano.

m. Mdhamini wa shindano hana dhamana ya hasara yoyote itakayotokana na uharibifu au upotevu wa vifaa vitakavyotumika katika shindano. Washiriki wote hawana haki ya kutoa madai ya aina yoyote kwa mdhamini wa shindano ikiwa kutatokea hali hiyo katika kipindi cha shindano.

n. Mdhamini wa shindano hana jukumu la kusimamia hatua yoyote kama kutatokea usitishwaji au uchelewaji wa baadhi ya maonyesho kutokana na hali ya hewa, moto, mgomo, matukio ya kigaidi na au sababu yoyote ile.