Tamasha la Sauti za Busara 8 – 11 February 2018
Stalls_at_Sauti_za_Busara_2014_(photo__Peter_Bennett)
Stalls_at_Sauti_za_Busara_2014_(photo__Peter_Bennett)
Kipindi cha tamasha kuna idadi ndogo ya vibanda vya kukodi kwa ajili ya kifanyia biashara ndani na nje ya Ngome Kongwe eneo la Bait El Ajaib, sehemu ambayo unaweza kuonyesha bidhaa zako. Vipaumbele vinatolewa kwa wenyeji na watu kutoka Afrika Mashariki ambao wanataka kuuza bidhaa zenye ubora kama sanaa za mkono, vinyago, nguo, muziki, vyakula na viburudisho. Bei ya vibanda ni tofauti kulingana na bisahara husika, sehemu na mahitaji stahiki.

Mwisho wa kupokea maombi: tarehe 09 December 2017

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa busara@busara.or.tz


AINA YA BIASHARA SEHEMU MALIPO (pamoja na pasi mbili)
Vyakula & Viburudisho
(bila ya Pombe)
Mambo Club
(Main Stage)
Amphitheatre
600 000/- TSh (US$300)

400 000/- TSh (US$200)
Nguo, Vinyago, Sanaa za mkono, etc Mambo Club
(Main Stage)
Amphitheatre
400 000/- TSh (US$200)

300 000/- TSh (US$150)
Mashirika/Makampuni Mbalimbali 600 000/- TSh (US$300)
Taasisi zisizokuwa za kiserikali Mbalimbali 200 000/- TSh (US$100)
Tafadhali jaza fomu hii kama unataka kufanya au kuonyesha biashara yako kwenye tamasha la Sauti za Busara 2018.
Wafanyabiashara watakaokubaliwa watajulishwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Januari 2018.

Vigezo na masharti

MALIPO

 1. Malipo yote lazima yafanyike kabla ya tarehe 31 Januari 2018.
  Busara Promotions inapokea malipo ya hundi, pesa taslim au malipo ya benki moja kwa moja.
 2. Ikiwa malipo hayajapatikana kwa muda ulioelezwa basi eneo la biashara atapatiwe mtu mwingine.
 3. PESA HAITARUDISHWA baada ya malipo kufanyika.

BIASHARA

 1. Ruhusa ya kufanya biashara kwenye SzB 2018 ni kuanzia Jumatano tarehe 7 Feb 2018 saa 3:00 asubuhi mpaka Jumatatu tarehe 13 Feb 2018 saa 8:00 mchana TU.
  Mfanyabiashara anatakiwa awepo eneo la biashara siku ya Jumatano ya tarehe 7 Feb kuanzia saa 4:00 asubuhi kuwa tayari kuanza kufanya biashara kabla ya saa 10:00 jioni siku ya Alhamis tarehe 9 Feb.
 2. Hairuhusiwi kwa mfanyabiashara kumkodisha mfanyabiashara mwingine.
  Mfanyabiashara aliyefanya maombi na malipo ndio anayeruhusiwa kuwepo eneo la biashara.
 3. Mfanyabiashara haruhusiwi kufanya biashara ya pombe na sigara.
  Kama mfanyabiashara ataleta bidhaa hizo basi biashara yake itakamatwa na kutolewa.
 4. Waandaaji wa tamasha wana haki ya kumpatia eneo mfanyabiashara pindi atakapofika
 5. Hairuhusiwi kutumia alama yoyote ya Sauti za Busara kwenye kitu chochote kama fulana, kofia au vinyago vitakapoonekana vitakamatwa.
 6. Bidhaa bandia haziruhusiwi.
 7. Mfanyabiashara lazima aonyeshe jina la biashara yake mbele ya banda lake kulingana na maombi aliyofanya (tangazo karatasi A4)

PASI

 1. Kila banda litapatiwa pasi mbili za wafanyabishara. Pasi za ziada lazima zilipiwe mwanzo.
 2. Mfanyabiashara lazima ahakikishe wasaidizi wake wana pasi halali za kufanyia kazi.
  Kwa yeyote atakayegundulika hana pasi halali atatolewa.
 3. Mfanyabiashara lazima atoe majina ya wasaidizi wake, na kuambatanisha na picha moja ya paspoti saizi, kabla ya tarehe 31 Januari 2018.
 4. Mfanyabiashara lazima atoe ushirikiano kwa walinzi wa tamasha itakapohitajika.

ZIADA

 1. Waandaaji watatoa umeme na taa kwa mfanyabiashara, mfanyabiashara mwenye vifaa kama Jokofu, blenda, kikaangio cha umeme, atahitajika kuchangia gharama za umeme. Makubaliano yafanyike mwanzo.
 2. JENERETA HALIRUHUSIWI eneo la biashara.
 3. Viti viwili na meza ndogo itatolewa kwa kila banda. Viti au meza za ziada itabidi kukodiwa kutoka kwa waandaaji kwa gharama za ziada, kama ikihitajika. Makubaliano yafanyike mwanzo.
 4. Mfanyabiashara haruhusiwi kuwasha moto ndani ya ukumbi, muuza mishkaki makubaliano yafanyike mwanzo.
 5. Mfanyabiashara haruhusiwi kuwasha muziki.
 6. Mfanyabiashara haruhusiwi kuuza pombe au bidhaa yoyote yenye kilevi bila ya ruhusa kutoka kwa waandaaji.
 7. Silaha ya aina yoyote hairuhusiwi ndani ukumbi.

Wafanyabiashara wote wanahitajika kusaini makubaliano haya kulingana na vigezo na masharti ya eneo la biashara. Mfanyabiashara atakayekiuka masharti haya basi atazuiwa kufanya shughuli zake papo hapo.