Vibali kwa waandishi wa habari

Maombi ya vibali vya kutoa habari YAMEFUNGWA

  • Sign up for our press list (ENGLISH)

  • Waandishi wa habari, jisajili hapa (KISWAHILI)

  • Press_Conference_ZNZ_by_Peter_Bennett_IMG_2519_hr_editp
  • Grace_Barbé_Press_by_Peter_Bennett_IMG_2575_hr_editp

Vibali kwa waandishi wa habari
Tumeanza kuruhusu maombi kwa ajili ya vibali kwa waandishi wa habari katika Sauti za Busara 2018.
Mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 19 December 2017.

Maombi ya vibali vya kutoa habari
Usahili kupitia mtandaoni kwa wanachama ni lazima. Tafadhali fata maelekezo vizuri wakati una kamilisha usahili wako mtandaoni.

Jaza nafasi zote zilizo achwa wazi.Chombo husika cha habari kinapaswa kutoa sifa zake mapema kwakua haitokua rahisi kufanya maombi wakati wa tamasha.
Punde utapomaliza kujaza fomu ya kuomba kibali , utapokea barua pepe kutoka katika uongozi kukujulisha wamepokea maombi yako. Nafasi ni chache hivyo sio vyombo vya habari vyote vitapata vibali. Busara promotions ndio wana haki ya kutoa au kutotoa kibali.
Fomu ya usahili mtandaoni

Kuhusu vibali kwa vyombo vya habari
Chombo cha habari kitachopewa kibali kwa ajili ya kutoa habari za tamasha kitapatiwa cheti cha kumruhusu aingie kwenye tamasha, uwezo wa kuingia kwenye mikutano yote ya habari ya tamasha, sehemuiliyoandaliwa ngome kongwe  kwa ajili ya kutoa habari na iliyowezeshwa na wifi, mahojiano na wasanii pamoja na watu wote wanaohusika na sanaa ya muziki katika kipindi chote cha vikao na wataalamu.
Shughuli zinazohusisha stendi  ya mic, mwanga wa nyongeza au shughuli inayohusisha mtu zaidi ya mmoja inaruhusiwa katika kipengele cha kibali kurekodi filamu kwenye tamasha tu.
Kibali cha kupiga picha (mbele ya steji ) kitatolewa kwa wale wenye kibali cha kurekodi filamu au kupiga picha kwenye tamasha. Wapiga picha wote hawatoruhusiwa kuwepo katika steji au nyuma ya steji katika mda wowote, labda ikiwa amepata ruhusa kutoka katika uongozi.

Bei za Sauti za Busara 2018

Wakimataifa

Mkazi wa Africa mashariki

Raia wa Tanzania

Kibali cha chombo cha habari kwenye tamasha

USD 120

USD 60 

20,000/- TSh

Kibali cha mpiga picha kwenye tamasha

USD 250

USD 60

50,000/- TSh

Kibali cha kurekodi filamu kwenye tamasha

USD 2,500

USD 500

500,000/- TSh

Tafadhali tambua kua ada hizi ni muhimu kusaidia kufikia malengo ya tamasha na pia kuweza kuleta wasanii wakiafrika kwenye Tamasha. Mchango wako unathaminika. Kuna idadi chache za vibali zitavyo tolewa bure na vitatolewa kwa Busara za uongozi wa tamasha. Vibali hivyo vitatolewa kwa vyombo vitavyo saidia na kukuza tamasha liweze kuendelea  au ambavyo vilishawahi kufanya kazi hiyo kwa matamasha yaliyopita. Utoaji wa viungo kuthibitisha ushiriki wako katika matamasha yaliyopita itaweza kufanya ombi lako kuangaliwa zaidi kipindi cha uchakataji wa kutoa vibali.


Ustahiki wa kupata kibali kwa chombo cha habari
Vibali vitatolewa kwa wataalamu wanao tambuliwa na chombo husika cha habari kitachohusika kwenye Tamasha. Utatakia kutoa anuani ya barua pepe kutoka kwa muhariri wa tangazo lako kukutambua ya kua wewe ndie utakayehusika na Sauti za Busara 2018. Utakapo wasili ngome kongwe , na kupewa kibali chako pamoja na kitambulisho chako utatakiwa kuleta nakala ya barua kutoka kwenye chombo cha habari husika.
Tafadhari tambua pia wakati unapo rekodi filamu nje ya ngome kongwe yakupasa uwe na kibali kutoka Wizara ya habari (Zanzibar).


Uthibitisho wa vibali kwa vyombo vya habari
Maombi yatapokua yamekwisha chakatwa, Taarifa ya uthibitisho itatumwa moja kwa moja kupitia barua pepe ifikapo Januari. Tafadhali njoo na chapa ya barua pepe hiyo ufikapo katika tamasha.
Wawakilishi wasiozaidi ya watatu kutoka kwenye stesheni ya redio,televisheni au mtandao wowote wataruhusiwa kwa kibali kimoja, ambapo itajumuisha maripota wawili na mshika kamera mmoja au mpiga picha..


Taarifa ya nyongeza
Kutokana na ufinyu wa bajeti, hatutoweza kulipa gharama za safari, malazi na gharama zingine zozote kwa chombo chochote au mwanachama yoyote aliyepewa kibali. Vibali kutoka Sauti za Busara ni cha mwanachama aliyepewa na hairuhusiwi kuhamisha umiliki.
Kwa matumizi ya kibali isivyotakiwa, Sauti za Busara watakua na haki ya kubatlisha kibali hicho muda wowote.
Tafadhali kumbuka kutuma nakala za ushiriki wako katika matamasha ili tuweze kuweka kwenye kumbukumbu zetu. 
Shukrani,Tunatambua na kuuthamini ushiriki wako katika kuipeleka Sauti za Busra mbele na kuizidi kuitambulisha kimataifa.

Tarehe ya mwisho
Mwisho wa kutoa vibali kwa vypmbo vya habari kwa ajili ya Sauti za Busara 2018 ni 19 December 2017.


Kwa maswali, tafadhali wasiliana na  press@busara.or.tz

  • Kyekyeku_Press_by_Peter_Bennett