Busara symbol - click for home page
BUSARA NEWSLETTER
June 2006

In this edition:

Sauti za Busara 2007

Taarifa kwa wasanii (Mwisho wa kupokea maombi 31/8/2006)

Mchango wa wadhamini

Tusaidie kusambaza taarifa

Angalia filamu!

Wasanii Wetu

Bi Kidude – zaidi ya miaka 90 na bado najisiki kama motto wa miaka 16

Jagwa Music – Mchiriku waenda kimataifa

Yajayo

Tamasha la Nchi za Jahazi – ZIFF

Tamasha la Avante Mozambique!

Nafasi

Nafasi ya kazi na mafunzo kwa msimamizi wa shughuli za sanaa

Voluntary Placements for Experienced Professionals

Photo exhibition available for showing

Tamasha la B-Connected

Busara Office: CD faves

Utabiri wa hali ya hewa – Zanzibar – February 2007

Wasiliana Nasi

 

Sauti za Busara 2007

topback to the top

 

Tamasha la nne la Sauti za Busara litafanyika kama kawaida mwezi wa Februari, kuanzia tarehe 9 hadi 14 2007; na kama kawaida kiingilio ni bure kabla ya saa mbili usiku kila siku.

A sneak preview of 2007 festival poster

Tamasha hili hufanyika kila mwaka katika kipindi ya katikati ya mwezi wa Februari,na ni tukioi ambalo huvutia watu wa jinsia , rika, Imani na mataifa mbalimbali katika kujionea na kusherehekea utajiri wa aina mbalimbali za muziki wa waswahili na watu wa Afrika ya Mashariki.

Tamasha hili huonyesha aina mbalimbali za muziki na maonyesho ya jukwaani hususan kutokea Afrika ya Mashariki, pamoja na baadhi ya vikundi kutoka nje ya Afrika Mashariki hualikwa pia. Mwaka huu tamasha litafanyika katika uwanja wa Ngome Kongwe eneo la Mji Mkongwe, vile vile maonyesho mengine yanatarajiwa kufanyika katika vitongoji mbalimbali pembezoni mwa Mji Mkongwe, na mojawapo ya fukwe maridadi Zanzibar.

 

Taarifa kwa wasanii ( Mwisho wa kupokea maombi 31/8/2006)

Zaidi ya vikundi na wasanii mia moja wameshiriki katika moja ya matamasha yaliyopita ya Sauti za Busara na baadhi yao ni Juma Nature & Wanaume family, Saida Karoli, Mchinga Generation, Ferooz na Das Nundaz, Eric Wainaina ( Kenya), Ghorwane ( Mozambique), The Shrine Synchrosystem ( Uingereza), Taffetas ( Uswisi), Atongo Zimba ( Ghana), African Revolution Band, Maulid ya Hom, El Tanbura ( Misri), Seiyun Popular Arts ( Yemen), Culture Music Club, Chibite, Wagosi wa Kaya na wengineo wengi.

Baadhi ya wasanii wa Afrika ya Mashariki kama Afrikali Band, Oya Theatre, Zemkala, Jagwa music, X Plastaz, Sina Chuki Kidumbak na wengineo wameanza kupata mialiko ya kushiriki matamasha nje ya nchi baada ya kuonekana katika tamasha la Sauti za Busara.

The animated Lucy gyrating to The Shrine Synchrosystem at 2006 festivalJe unataka kushiriki?

Kwa wasanii wanaotaka kushiriki katika tamasha lijalo la 2007, unatakiwa kutuma maombi yako kabla ya mwisho wa mwezi wa Agosti. Tuma maombi yako kwa njia ya barua pepe (email) au barua ya kawaida kwa ofisi ya Busara Promotions (Anuani hapo chini). Maombi yaambatane na nakala za kazi yako ya hivi Karibuni (CD, Kanda za kaseti na/au video). Picha pamoja na maelezo ya kina ya msanii au kikundi, na pia kama una kumbukumbu za maelezo kutoka katika vyombo vya habari juu yako tafadhali ambatanisha pia.

Kwa wasanii wanaochaguliwa kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara, gharama zao za usafiri, malazi, chakula na malipo ya onyesho zitalipwa na waandaaji (Busara Promotions). Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki watatakiwa kujilipia wenyewe gharama za usafiri.

Mchango wa wadhamini

Tamasha hili lisingeweza kuwa lenye mafanikio kama si kwa mchango mkubwa wa wadhamini na wafadhili mbalimbali.

Busara Promotions imeandaa taarifa maalum kwa wadhamini na wafadhili mbalimbali juu ya namna ya kushirikiana ili kufanikisha tamasha la nne la Sauti za Busara. Taarifa hiyo imeambatanishwa na DVD ya tamasha, azimio, bajeti na orodha ya namna mbalimbali ambazo jina lako linaweza kuwa miongoni mwa wafanikishaji wake. Iwapo una nia ya kushirikiana nasi tafadhali wasiliana nasi.

 

Tusaidie kusambaza taarifa

Kama unayo nafasi ya kulitangaza tamasha la Sauti za Busara tunatanguliza shukrani za dhati kwa msaada wako.

Je unayo orodha ya anuani za barua pepe, tovuti, ubao wa matangazo au nafasi katika jarida?

Maneno machache tu na taarifa juu ya tovuti yetu yatasaidia sana. Nasi pia tutakuwa tayari kukutangaza katika moja ya kurasa za tovuti yetu.

Tunaweza pia kukutumia matangazo ya ukutani (posters) na postikadi za tamasha kama si gharama sana.

 

Angalia filamu!

Si filamu kamili, lakini kuna filamu kibao fupi, picha na maelezo ya tamasha katika tovuti mbalimbali:

Filamu fupi za tamasha la mwaka 2006
(Associated Press)

2006 video clips

Taarifa mbalimbali za tamasha la mwaka 2006

2006 review

Taarifa mbalimbali za tamasha la mwaka 2005

2005 review

Taarifa mbalimbali za tamsha la mwaka 2004

2004 review

Taarifa mbalimbali za tamasha la mwaka 2006

2006 In pictures: Swahili music festival

 

Wasanii wetu

topback to the top

Bi Kidude – zaidi ya miaka 90 na bado najisiki kama motto wa miaka 16

 

Bi_Kidude_&_Taarab_Masters-by_Peter_Bennett-DSC00770Mshindi wa tuzo ya WOMEX 2005, Bi Kidude atakuwa tena ziarani barani Ulaya wiki hii, akiambatana na kundi lake la Unyago. Msanii huyu mkongwe lakini ambaye anendelea kutamba katika ulimwengu wa sanaa, atafanya maonyesho matatu katika tamasha la kimataifa lijulikanalo kama Festival Mundial nchini Uholanzi kati ya terehe 15 na 18. Vile vile Bi Kidude atapata nafasi ya kuzungumzia filamu yake inayotarajiwa kuzinduliwa hapo mwezi wa Februari 2007 ijulikanayo kama “As Old As My Tongue” inayotengenezwa na kampuni ya ScreenStation UK.

Upigaji picha za filamu hii ulianza miaka mitatu iliyopita hapa Zanzibar na katika safari mbalimbali za kimuziki za Bi Kidude. Zaidi ya kuwa ni filamu inayoelezea maisha yake, inaelezea mambo mbalimbali ya kisiasa, kiutamaduni na kijamii kisiwani Zanzibar.

Bi Kidude ni msanii ambaye anafahamika kama shujaa aliyepamabana na vikwazo vingi hadi kufikia hapo alipo. Na amejijengea himaya ya mashabiki wengi ndani na nje ya nchi. Yeye ni kipenzi cha Masultani, Marais na mabaharia wa kale wa majahazi, historia yake ni changamoto kuwa umri si kikwazo cha kutimiza ndoto zetu. Bi Kidude hupendelea kukaa nyumbani kwake akiwa na wajukuu, jamaa na marafiki, yeye ni mwongeaji sana na mpenda wageni, pia hupendelea kuvuta sigara.

 

Jagwa Music – Mchiriku waenda kimataifa

Jagwa_Music-by_Muhidin_Michuzi-IMG_0343Umewahi kusikia kuhusu Bongo Flava na Congotronics. Kaa tayari sasa kwani “Bongotronics” inakuja, ni muziki wenye umaarufu katika maeneo ya watu wa kipato cha chini jijini Dar es Salaam.

Jagwa Music ni kikundi kinachopiga muziki wa mchiriku ambao ulizaliwa kutoka katika muziki wa kimwambao ujulikanao kama chakacha. Ala zinazotumika katika muziki huu ni pamoja na Keyboard ndogo ya mkono, ngoma, filimbi, mkwasa, kibao cha kukalia na wakati mwingine gitaa pia hutumika.

Mwaka 2005 Jagwa Music ilipata nafasi ya kwenda nchini Uingereza kushiriki katika tamasha la WOMEX, na waliweza kuwa kivutio kikubwa hasa kutokana na uchezaji wake. Na tayari waandaji wa matamasha kutoka nchi mbalimbali wameanza kutoa mialiko kwa kikundi hiki.

Jagwa wamerekodi albamu zaidi ya kumi katika kanda za kaseti, lakini kwa mara ya kwanza mwaka huu wameweza kurekodi CD yao ya kwanza ambayo inafanyiwa marekebisho nchini Ujerumani na itazinduliwa mapema mwaka 2007.

Vilevile kwa mara ya kwanza wamerekodi kanda ya video ya kwanza inayojulikana kama Maisha Popote, na inatarajiwa kurushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni hivi Karibuni.

 

Yajayo

topback to the top

Tamasha la Nchi za Jahazi – ZIFF

ZIFF Festival of the Dhow CountriesKuanzia tarehe 14 hadi 23 mwezi wa Julai Zanzibar itakuwa tena mwenyeji wa tamasha la tisa la Nchi za Jahazi ambalo ni tamasha maarufu kabisa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Ni tukio linalosubiriwa kwa hamu kubwa kabisa, kutakuwa na maonyesho ya filamu mbalimbali, muziki, kazi za sanaa, semina, warsha na mambo mengine mengi.

 

Tamasha la Avante Mozambique!

Avante Mozambique! FestivalTumepata mwaliko wa kupeleka vikundi viwili kutoka Tanzania kwenda kushirki kataka tamasha la Avante Mozambique. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mnamo mwezi wa Septemba na tunatarajia kuwapeleka Jagwa Music kutoka dar es Salaam na Bi Kidude.

 

 

Nafasi

topback to the top

Nafasi ya kazi na mafunzo kwa msimamizi wa shughuli za sanaa

crew-by_Masoud_KhamisBusara Promotions inatafuta mtu atakayeweza kufanya kazi na kupata mafunzo ya kuwa msimamizi wa shughuli za sanaa kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa Agosti 2006 hadi Machi 2007.

Mwombaji ni lazima awe raia wa Afrika Mashariki na mwenye moyo wa kupenda na kutaka kutunza muziki wa kiafrika. Ni muhimu kwa mwombaji kuwa na ujuzi wa msingi wa Kompyuta, ufahamu wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Kwa yule atakayepata nafasi hii atakuwa akipata mafunzo kazini amabayo ni pamoja na masuala ya uandaaji wa matamasha, semina, warsha, namna ya kufanya matangazo, kusimamia wasanii na ufahamu wa sura ya muziki wa Afrika Mashariki.

Atakayechaguliwa katika nafasi hii atafanya kazi katika ofisi za Busara Promotions zilizopo eneo la Mji Mkongwe Zanzibar, na awe tayari kusafiri pale atakapohitajika. Busara Promotions itagharamia posho ya kujikimu na vile vile mwombaji atapata cheti maalum mara tu baada ya kumaliza mafunzo na tunamini ya kuwa nafasi hii itamwezesha mwombaji kuwa dereva bora katika maendeleo ya muziki Afrika Mashariki.

Kwa yeyote atakayependa kuomba nafasi hii basi tafadhali tuma barua pepe au kwa njia ya posta ikiambatanishwa na vielelezo vya kuthibitisha uwezo wa mwombaji, ili viweze kufika ofisi za Busara promotions kabla ya tarhe 27 Juni 2006.

Voluntary Placements for Experienced Professionals

Occasionally Busara Promotions is able to offer short term placements for skilled and experienced music professionals, for example: music producers and sound engineers. Such placements are usually on a voluntary basis and involve on-the-job training of Tanzanians.

Contact us for more details in case you fit the bill.

 

Photo exhibition available for showing

Poster for photo exhibition

This stunning photographic exhibition received an enthusiastic response at WOMEX (UK, 2005) and in Zanzibar during the 2006 festival from locals and visitors alike. There are over 40 pictures taken mostly of performers in preceding Zanzibar festivals and of Bi Kidude on the road.

This exhibition is now available to institutions, organisations and even for corporate promotions within East Africa. If you think you might like to host this exhibition please get in touch for further details.

 

Tamasha la B-Connected

topback to the top

Dar es Salaam – 21 Mai 2006

Busara Promotions imefarijika kwa kushirikishwa katika tamasha la B-Connected mbalo liliambatana na matamsha mengine katika nchi za Afrika Kusini, Ethiopia, Hungury na Uholanzi.

“Hili ni tamasha zuri sana kuliko mengine niliwahi kuhudhuria” Joshua kijana wa kimasai aliyekuwa akivuja jasho kutokana na kucheza muziki alimwambia mwandishi wa Daily News

Wengi wa wasanii washiriki walipata nafasi ya baada ya kushinda katika mashindano yaliyoandaliwa kwa ajili ya kusaka vipaji vya wasanii wachanga. Mwanzoni mwa mwezi wa Mei Busara ilishiriki kama mmoja wa majaji wa shindano la kusaka vipaji Zanzibar na pia iligharamia usafiri wa kwenda na kurudi Dar es Salam – Zanzibar kwa washindi ambao walikuwa ni BZ Brook wa upande wa muziki wa kizazi kipya na Shirkisho Sanaa Group kwa ngoma za asili.

 

Busara Office: CD faves

topback to the top

 

Looking for some music suggestions? Here’s what’s getting played in the Busara Office at the moment:

Toumani Diabate & Symmetric Orchestra

Boulevard de l’Independence

(Mali)

World Circuit

Gigi

Gold & Wax

(Ethiopia)

Palmbeat

Wanaume Family TMK

Ndio Zetu

(Tanzania)

Bongo Records

Ursula Rucker

Ma’at Mama

(USA)

K7

Various Artists

Midnight in Mali

(Mali)

Sterns

Tiken Jah Fakoly

Coup De Gueule

(Ivory Coast)

Wrasse

Various Artists

Rough Guide to Tanzania

(Tanzania)

World Music Network

Gotan Project

Lunatico

(France)

XL

Natacha Atlas

Mish Maoul

(UK)

Mantra

Samba Mapangala

Song & Dance

(DRC)

Virunga

The Streets

The Hardest Way to Make an Easy Living

(UK)

679

Atongo Zimba

Savannah Breeze

(Ghana)

Hippo Records

 

Utabiri wa hali ya hewa – Zanzibar – February 2007

topback to the top

 

Zemkala-by_Muhidin_Michuzi

Busara Sunshine

Bringing people together

Busara Sunshine Taffetas-by_Masoud_Khamis
Busara Sunshine

Atongo_Zimba-by_Masoud_Khamis

Busara Sunshine

Sinachuki_Kidumbak

Busara Sunshine

 

Wasiliana Nasi

topback to the top

 

Busara Promotions, PO Box 3635, Zanzibar, Tanzania

busara@zanlink.com

+255 24 223 2423 or +255 777 428 478
Fax: +44 870 132 1190

Find us in Stone Town, between Africa House and Serena Hotel, opposite Amore Mio.

 

We are continually in the process of revising and updating our mailing-list. If you have received this more than once, or would prefer to receive it at another address, please let us know. Alternatively, you can click here to unsubscribe.