Tamasha la muziki la Sauti za Busara 2007
|
Tamasha la nne la Sauti
za Busara litafanyika hapa Zanzibar, mwezi wa pili tarehe 9 hadi 14 mwaka
2007. kiingilio kikiwa ni bure kwa watu wote watakaoingia ukumbini
kabla ya saa 12:30 jioni.
Pia waweza kuangalia….. (www.busaramusic.com)...
Africa Directions (zm),
Amani Drummers of Burundi (bi), Annet Nandujja
& The Planets (ug), Ba Cissoko
(gn), Bi Kidude (znz), Black Roots (znz),
Chibite (tz), Culture Musical Club (znz),
Dhow Crossing (znz/no), Ellika & Solo (se/sn),
Imena (rw), Jhikoman (tz),
Kinobe & Soul Beat Africa (ug), Makadem
‘Ohanglaman’ (ke), Manyani Nani
(tz), Matona & G-Clef (znz), Menwar
(mu), Nazareth Choir (tz), Netsayi
(zw/uk), Olith Ratego (ke),
OSB Crew (mu), Qasida Swiffat Nabawiyyatul
(znz), Shailja Patel (ke/ca), Shirikisho
Sanaa (tz), Tamarind Band (tz), The
Collaboration ft Chiwoniso & Busi Ncube
(zw), Yunasi (ke), Zemkala
(tz)
|
|
|||||||||
Tiketi
na Gharama zake
Kiingilio cha kila siku sasa kitaanza
kutumika kuanzia saa 12:30 jioni. Kwa wasio wakazi gharama ziko kwa
dola za kimarekani kwa sasa, hii itawasaidia watu kutoka nje ya nchi
wanaohitaji kufahamu gharama za tiketi kuwa na ufahamu thabiti wa gharama
na viwango vyake kwa kulinganisha na fedha za kigeni.
|
Vikundi 40 kutoka Zanzibar, Tanzania bara, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Mauritius, Zimbabwe, Africa Magharibi na Ulaya.
Kutakuwapo na bendi ya beni, watembea kwa miguu pamoja na sarakasi.
Eeh bwana! Hatutakuwa peke yetu.
Wakiwamo watu wengi hapa mjini, kutakuwapo na maonyesho mbalimbali yatakayoandaliwa
na mahoteli, mikahawa na wafanyabiashara wengine, haya yote tunayaita "Busara
Xtra" tukiwa na maana ya maonyesho nje ya eneo la tamasha, nia ikiwa ni
kuwapa fursa wageni watakaohudhuria tamasha letu kupata nafasi ya kuona matukio
mengine yatakayojiri wakati wa tamasha la Sauti za Busara. Tutajitahidi kadiri
ya uwezo wetu kuwafahamisha nini kinachoendelea kwenye "Busara
Xtra".
Tunazo filamu chache ambazo tunadhani ungependa kuziona, mahsusi ikionyeshwa kwa mara ya kwanza filamu inoyaitwa "As Old As My Tongue" ambayo inaelezea ngano na maisha ya Bi Kidude.
Wiki moja kabla ya tamasha,
wasanii walioalikwa watakutana pamoja katika kile kinachoonekana kama
uchanganuzi wa misingi na tofauti walizonazo kimuziki. Michango yao inapokutana
na kuingiliana kwa vyovyote kuna kitu kipya kitazaliwa. Kaa tayari kushuhudia
matokeo ya semina hiyo wakati wa maonyesho.
Semina hii ni ya wazi kwa wasanii kutoka Afrika Mashariki pamoja na wataalamu
kutoka katika nyanja ya muziki tu. Iwapo upo katika mojawapo ya nafasi hizo
basi wasiliana
nasi kwa maelezo zaidi.
Kwa kuzingatia nia na matokeo ya maonyesho ya picha ya mwaka 2006 "Pale muziki uliponifikisha" na kwa kutambua
kwamba kuna picha nyingi nzuri zinazopigwa mahali fulani, tumewaalika wapiga
picha kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki katika maonyesho ya picha
za wasanii wa Zanzaibar nje ya nchi na wasanii wa nje ndani ya Zanzibar.
Katika siku ya mwisho ya tamasha, watu wote tutaondoka katikati ya mji na
kuelekea pwani ya kaskazini mwa Zanzibar (Kendwa Rocks) ambako kutafanyika kubwa sherehe za ufungaji wa tamasha (Festival Finale Party). Huko kutakuwa na maonyesho mbalimbali yatakayofanyika
katika ufukwe wenye mchanga mweupe wa bahari. Kumbuka kuwa siku hiyo itakuwa
ni sikukuu ya wapendanao hivyo usisahau kuja na umpendae tushereheke na kucheza
mpaka majogoo.
| Kwa masuala yote yanayohusu usafiri na mahali pa kukaa ndani ya Zanzibar (pia usafiri wa anga ndani ya bara la Afrika), tunachukua nafasi hii kukushauri kutumia Zanzibar’s Tabasam Tours. Wao watakusaidia kuandaa masuala ya usafiri, malazi na kukuandalia Pasi ya siku 4 . Pia watatoa punguzo la
asilimia 5 kwa wote watakaohitaji huduma zao wakati wa tamasha hata
kama ni kwa siku moja ya tamasha. Jaribu kuuliza kuhusu "Punguzo
la Busara". |
Tamasha la muziki la Sauti za Busara
huwakutanisha watu wa rika mbalimbali pamoja katika kusherekea utajiri na
utofauti wa muziki wa waswahili. Sifa zake zinazidi kukua kwa haraka sana.
Jukwaa kuu la tamasha litajengwa katikati ya migomba, nyuma ya ukuta wa kale
na kihistoria ujulikanao kama "Ngome kongwe" ndani ya Mji Mkongwe,
mji ambao umeorodheshwa na UNESCO kuwa eneo la urithi wa kimataifa. Wakazi
wa Afrika Mashariki wanatazamia kwa shauku na fahari kubwa kila mwezi wa pili
wa mwaka, ambapo Zanzibar huandaa" tamasha kubwa la usuhuba duniani"
Waandaji wa tamasha wanayo
furaha kutambua ukarimu wa misaada kutoka kwa wafadhili na wadhamini kwa ujumla,
kwani bila mchango wao tamasha hili aghalabu lisingaliweza kufanyika. Hatua
hii ya maandalizi wakati wote imekuwa ni jinamizi kwetu. Tumepokea baadhi
ya ahadi na bado tunahitaji msaada. Zaidi ya yote, tamasha la Sauti za Busara
linatiwa nguvu na wafuatao:
Ford Foundation,
Swiss Agency for Development & Cooperation, Celtel Tanzania, Holiday Inn,
British Council, Ubalozi wa Ufaransa, Art Moves Africa, CulturesFrance,
fROOTS Magazine, Ubalozi wa Ujerumani,
Archipelago Café & Restaurant, Mercury's Restaurant, Tabasam Tours, Kendwa Rocks, Ultimate Security,
Zanzibar Gallery, Jubilee Insurance, Roger Fenstein,
na Zanzibar.NET
Jiunge kama unaweza
|
Tamasha hili halitawezekana kufanyika bila msaada mkubwa kutoka kwa wafadhili na wadhamini.
Kwa wafadhili na wadhamini
muhimu, tumeandaa kifurushi cha ushirika wa msaada wa fedha kinachojumuisha,
video ya matangazo, maazimio ya tamasha, bajeti ya tamasha pamoja na orodha
nzuri ya jinsi tutakavyoweka jina lako ili lionekane kama sehemu ya mafanikio
ya tamasha. Kama una nia ya dhati kusaidia hili, tafadhali wasiliana
nasi.
Kama unayo nafasi kutangaza tamasha la Sauti za Busara tutafurahi sana kupata msaada wako. Labda unayo orodha ya barua pepe, website, ubao wa matangazo au nafasi ya matangazo ya biashara, maneno machache ya mapendekezo kuhusu tamasha letu ukifungamanisha na website yetu, kwa vyovyote vile tutathamini mchango huo. Kwa kulipa fadhila tutakuunganisha katika kurasa zetu za mahusiano ya kiofisi. Pia tutaweza kukusambazia karatasi kubwa zenye ujumbe wa tamasha la Sauti za Busara, kama jambo hilo halitatugharimu sana.
|
Bi Kidude na Magwiji wa Taarab ziarani
Ulaya– Novemba 2006
Mshindi wa tuzo ya
WOMEX kwa mwaka 2005, Bi Kidude anarudi tena Ulaya mwezi Novemba akiwa
pamoja na muunganiko wa magwiji wa kupiga muziki wa taarabu kutoka Zanzibar.
Malkia huyu wa taarabu
na balozi wa muziki wa Zanzibar kimataifa atafanya maonyesho yapatayo
saba katika miji mbalimbali maarufu nchini Uholanzi, Ujerumani na Ubeligiji.
Angalia ratiba hapo chini kwa ufahamu zaidi juu ya maonyesho yake Ulaya.
|
Akiwa
Ulaya Bi Kidude pia ataongelea kuhusu filamu yake ijayo inayoitwa"
As Old as My Tongue" iliyotengenezwa na ScreenStation
UK. Filamu hii ni kielelezo
halisi cha Bi Kidude, ngao inayoishi na kuna uwezekano kuwa ndiye mchezaji
mzee kuliko wote katika dunia muziki wa jukwaani hivi sasa. Bi Kidude
hujipatia marafiki wengi kila anaposafiri.lakini nyumbani Zanzibar anaendeleza
majadiliano kupata heshima, tabia yake ya kutoa changamoto kwa mtazamo
wa nafasi ya wanawake katika jamii ya kiislamu."As Old As My Tongue"
inaonyesha mwonekano wa aina yake katika maisha ya mwanamuziki huyu
na uhusiano wake na miaka mia moja ya muziki wa Waswahili. |
Maulidi Ya Homu (Mtendeni) kufanya onyesho ndani ya Paris, January 2007
|
Hapana! si filamu kamili,
lakini tunazo filamu fupifupi, picha na maelezo ya tamasha katika tovuti mbalimbali:
Hizi ndizo mpya kabisa ambazo unaweza kuziona:
| Tazama kwa dakika 5 tu filamu ya |
||
| Tazama kwa dakika 7 tu mfano wa filamu ya Bi
Kidude |
Routes In
Rhythm – Best of The World – Top 20, 2006
|
Looking for some music suggestions?
Here’s DJ Yusuf's pick of the year:
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
compiled
by DJ Yusuf, (djyusuf@mailcity.com) |
Utabiri wa hali
ya hewa kwa siku 5 – Zanzibar – Februari 2007
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
November
Competition |
Hey guess what? Here's a
chance to win a striking Sauti za
Busara t-shirt and a bunch of other goodies (including a brief video on
SzB2006)… All you have to do is answer
the following question: The name of the festival, "Sauti za Busara" roughly
translates into English as "Sounds of Wisdom", but from which
language? Send us the answer, along
with your name before the end of November. Each correct entry will be
attached individually to a coconut and placed in an enormous, old,
brass-studded, brown-coloured, wooden Zanzibari
chest which will be shaken vigorously. The winning entries will be the first
five drawn from the chest (assuming the coconuts have not leaked) – and the
winners will be informed by email and listed on our website. Ready to enter? Then send
us an email with "November
Competition" in the subject. |
Wasiliana
nasi |
|
Busara Promotions, PO Box 3635,
Zanzibar, Tanzania +255 24 223 2423 or +255
777 428 478 Find us
in |
Unfortunately
there was a problem in the mail service we were using, and some of our friends
were swamped with numerous messages which became intolerable. We apologise for
the irritation and annoyance this might have caused and would like to reassure
you that we have now changed our mail service – so hopefully it will never
happen again. Thank you for bearing with us.