Do not reply to this email address. If you would like to get in touch please use busara@zanlink.com |

|
BUSARA NEWSLETTER |
October 2008 |
| In this edition: |
English version |
| |
Mtanange wa sita wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 12 hadi 17 Februari 2009; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya machweo.
Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.
Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea. |
|
|
|
 |
Tusikia fahari kutangaza kwamba Samba Mapangala amethibitisha kushiriki akiambatana na bendi yake ya Orchestre Virunga. Kwa hakika yeye ni mmoja wa wasanii mahiri na wanaopendwa sana hapa Afrika Mashariki. Katika muda wa miaka 25 ameweza kutamba na vibao mbalimbali, vikiwemo Virunga, Ahmed Sabit, Vunja Mifupa, Sungura, Vidonge, Dunia Tunapita na Nyama Choma. |
|
Samba Mapangala & Orchestre Virunga (DRC/Kenya/USA), Msondo Ngoma Band (Tanzania), Omar Pene & le Super Diamono (Senegal), Mangala Camara (Mali), Nawal (Comoros/France), King Ayisoba (Ghana), TY (UK), Meta and the Cornerstones (Senegal/USA), The Moreira Project (South Africa), Comrade Fatso and Chabvondoka (Zimbabwe), Jagwa Music (Tanzania), AY (Tanzania), Joh Makini (Tanzania), Elemotho (Namibia), Segere Original (Tanzania), Best of WaPi (Pan Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar), Bi Kidude (Zanzibar), Iddi Achien'g (Kenya), Khethi with Kibo Sounds (South Africa/Tanzania), Rachel Magoola (Uganda), Wahapahapa Band (Tanzania), Omega Bugembe Okello (Uganda/USA), Aron Nitunga (Burundi/Canada), Safar (Zanzibar), Kiumbizi (Pemba), Zinduka Ngoma (Zanzibar), Dj Side (Zanzibar), and more to be announced |
 |
 |
Kama ilivyo ada kutakuwa na matembezi ya ufunguzi wa tamasha siku ya tarehe 12 Februari, matembezi hayo yataambatana na burudani za Beni, Mwanandege, Ngongoti, wachezaji na wanasarakasi. Mkusanyiko huo utawasili maeneo ya Forodhani nyakati za saa kumi na moja alasiri na kuingia ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe.
|
|
Kuanzia siku ya Alhamisi mpaka Jumapili, kutakuwa na burudani ya vikundi kumi kila siku. Wasanii wakubwa wataonyeshana kazi na wale wanaochipukia. Kwa pamoja tuna mseto wa vikundi thelathini kutoka Zanzibar, Tanzania bara na Afrika Mashariki. Vikundi hivi ni mchanganyiko wa vile vya muziki wa asili, vionjo mchanganyiko na ule wa kileo. Vilevile kuna vikundi vingine kumi kutoka Komoro, Zimbabwe, Afrika Kusini, Mali, Senegal, Ghana, Nigeria na Uingereza. Kwa taarifa zaidi kuhusu tamasha wasanii washiriki, na yatakayojiri kwenye tamasha lijalo basi tembelea katika tovuti yetu mara kwa mara, na utajionea picha, filamu, taarifa mbalimbali na mengineyo mengi.
Mtiririko wa maonyesho ya muziki ni wa “Bandika Bandua” yaani ni onyesho moja baada ya lingine. Maonyesho yote huanza wakati wa jioni, muda ambao joto la jua linapoanza kungua, mara nyingi kundi la mwisho hupanda stejini nyakati za saa sita ya usiku. |
 |
|
Jukwaa kuu la burudani lipo eneo la Mji Mkongwe, ndani ya ukumbi wa kihistoria wa Ngome Kongwe (upande wenye majani) na juu upo wazi. Kipindi cha tamasha ukumbi huu hupambwa kwa rangi mbalimbali, na pia kunakuwa na karibu vibanda ishirini kwa ajili ya huduma za vinywaji, chakula, uuzaji wa nguo, bidhaa za kisanii, pamoja na kanda na CD za wanamuziki mbalimbali.
Pilika pilika ni nyingi kila siku ya tamasha ndani ya ukumbi huu, wenyeji na wageni wa rika, tamaduni na jinsia mbalimbali hujazana kwa wingi. Muda wa jioni kunakuwa na watoto na familia nyingi katika hali ya furaha na bashasha, wadau mbalimbali wa sanaa na utamaduni kutoka kona mbalimbali hubadilishana mawazo. Giza linapoingia wapenda muziki nao hujifaragua na kujirusha kutokana na mirindimo ya muziki na burudani mahiri.

Kila mtu anakubali kwamba kipindi nyoyo ya kila mhudhuriaji hukongwa kutokana na mandhari ya tamasha, na Sauti za Busara huthibitisha kuwa ni “tamasha rafiki zaidi duniani!” |
|
Kiingilio ni bure kila siku kuanzia saa kumi jioni hadi machweo. Baada ya hapo utahitajika kuwa na tiketi au pasi maalum ya kuingilia. Bei zinatofautiana baina ya wageni, wakaazi na. Kwa wanaopendelea kukaa kwenye viti kuna tiketi maalum za VIP.
|
 |
Kwa mahitaji yako yote ya usafiri na malazi hapa Zanzibar pamoja na usafiri wa anga kwa Afrika, tunafurahi kukufahamisha kuwa wasiliana na Tabasam Tours iliyopo Zanzibar. Wao wanatoa huduma za uhakika za usafiri wa kwenda na kurudi uwanja wa ndege, maandalizi ya malazi na pia unaweza kupata pasi ya siku nne ya tamasha kupitia kwao.
Na zaidi ni kwamba kutakuwa na punguzo la asilimia 5 kwa wale watakaowatumia Tabasam Tours kufanya taratibu zao za malazi. Ulizia "Busara Discount".
Usafiri Na Malazi>>>
|
|
Siku ya mwisho wafanyakazi wa tamasha, baadhi ya wasanii na wale wote wanaopenda kwa pamoja tutaelekea katika moja ya fukwe murua Zanzibar. Huko kutakuwa na ma-DJ, wacheza sarakasi, vikundi mbalimbali vya muziki na hivi ndivyo tutakavyohitimisha karamu yetu kwa mwaka 2009.
Shughuli hii imepangwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 17 Februari, Kendwa Rocks.
Sherehe ya kumalizia tamasha>>>.
|
 |
|
|
|
Wiki moja kabla ya kuanza tamasha, baadhi ya wasanii kutoka sehemu mbalimbali hualikwa na kukutanishwa pamoja. Lengo ni kuhamasisha mijadala pamoja na kujifunza baina yao, wasanii hawa hatimaye huzalisha kitu cha pamoja ambacho baadaye huonyeshwa katika jukwaa la tamasha.
Pamoja na DCMA |
 |

|
Warsha hizi ni kwa wasanii na wadau wa masuala ya muziki wa Afrika Mashariki tu. Iwapo unaamini kuwa warsha na semina hizi zinakulenga wewe basi wasiliana nasi kwa taarifa zaidi. |
|
Mafunzo haya pia ni kwa wasanii na wadau wa masuala ya muziki wa Afrika Mashariki tu. Iwapo unaamini kuwa warsha na semina hizi zinakulenga wewe basi wasiliana nasi kwa taarifa zaidi. |
 |
|
|
 |
Kumbukuka kuwa, siyo sisi pekee. Zanzibar ina maeneo mengine mengi ambako matukio kedekede hufanyika kwa mfano katika mahoteli, migahawa na kumbi mbalimbalii. Hii tumeibatiza jina la “Busara Xtra” na tutafanya kila jitihada kukufahamisha yale yote yatakayojiri.
|
|
|
|
Iwapo una nafasi na uwezo wa kulitangaza tamasha la Sauti za Busara tunahitaji sana msaada wako. Labda una orodha ndefu katika mtandao wako wa barua pepe, tovuti, ubao au nafasi yoyote ya matangazo. Maneno machache kuhusu tamasha na kuitangaza tovuti yetu itakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu. Nasi pia tutakuweka katika kurasa zetu za mtandao. Tunaweza kukutumia vipeperushi pamoja na matangazo mbalimbali yahusuyo tamasha kama si ghali sana. |
|
Tamasha hili litawezekana tu kutokana na ufadhili na udhamini mkubwa wa hali na mali kutoka katika vyanzo mbalimbali
Kwa wafadhili na wadhamini mbalimbali wenye nia ya kushirikiana nasi kulifanikisha, tumeandaa maelekezo yanayoainisha utaratibu mzima. Tunazo njia mbalimbali za kulionyesha jina lako kuwa ni mmoja wa wale waliolifanikisha Tamasha. Iwapo una nia hiyo tafadhali wasiliana nasi |
|
Nafasi za matangazo ni chache, kuweka tangazo la shughuli yako katika programu ya tamasha ni njia bora ya kuonyesha kutuunga mkono katika tukio hili adhimu.
|
|
|
|
Ni tamasha linaloonyesha ngoma mbalimbali za asili kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na kwingineko.
13 hadi 18 Octoba 2008
www.sanaabagamoyo.com |
New World Cinema
10 hadi 30 Octoba 2008
Filamu inayozungumzia maisha ya Bi Kidude bint Baraka ijulikanayo kama
AS OLD AS MY TONGUE
The Myth and Life of Bi Kidude
itaonyeshwa pia siku ya jumatatu Oktoba 20, saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano (6.45pm) New World Cinema
|
 |
|
Visa 2 Dance
Tamasha la dansi ya kisasa ambalo litahusisha vikundi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini. Kutoka nje ya Afrika vikundi ni kutoka Sweden, Italia, Germany na Marekani
Tarehe 22 hadi 24 Oktoba, Diamond Jubilee, Dar es Salaam
|
|
28 hadi 30 Novemba 2008
www.tourism.go.ke
.jpg)
|
Makutano
Maonyesho ya sanaa bora za mikono kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani
Tarehe 21 hadi 22 Novemba, Diamond Jubilee, Dar es Salaam
www.makutanotz.com
|
Mashabiki wa mgombea wa uraisi wa marekana Seneta Barack Obama wafahamu kwamba mmoja wa wasanii mashuhuri kwenye tamasha lijalo Samba Mapangala ametunga wimbo wa kuunga mkono ambao unajulika kama Obama Ubarikiwe, ni wimbo mpya ambao umeimbwa kwa Kiswahili na ukihitaji bila ya malipo unaweza kuupata kwa kubonyeza hapa www.myspace.com/sambamapangala |
|
|

www.womex.com |
WOMEX ni kubwa ambalo huwakutanisha pamoja wadau mbalimbali wa muziki kutoka katika kila kona ya Dunia, maonyesho ya kazi za wasanii, pamoja na yale ya jukwaani hufanyika pia.
Zaidi ya washiriki 3000 pamoja na makampuni 1,400 yatawakilisha nchi tisini mwaka huu, WOMEX linabaki kuwa tukio pekee muhimu kwa wale wote wanaojihusisha na muziki wa kimataifa. Tukio la 13 limerudi tena katika mji wa Sevilla, Andalusia, Hispania kuanzia tarehe 29 October hadi 2 November 2008.
Busara Promotions watakuwa katika kibanda namba 1/ H14. |
|
|
Waandaaji wa tamasha wanapenda kushukuru imani, busara, maono na msaada mkubwa wa wafadhili na wadhamini, ambao kama si wao Sauti za Busara lisingewezeka. Katika kipindi hiki cha maandalizi, bajeti na mipango inatupa wakati mgumu sana. Tumepatiwa ahadi kadha wa kadha na bado tunahitaji misaada zaidi. Hadi hivi sasa, tamasha limewezeshwa na: |
|
Dhow Countries Music Academy, ZG Design, fROOTS Magazine, Zanlink, Mercury’s Restaurant, Archipelago Café & Restaurant, Stone Town Café, Kendwa Rocks, ScreenStation (UK), Tabasam Tours, Linear Velocity, Footcandles, and www.zanzibar.net
|
|
|
|
www.busaramusic.org |
Busara Promotions,
PO Box 3635,
Zanzibar,
Tanzania
busara@zanlink.com
Tel: +255 24 223
2423 or +255 784 925 499 or +255 773 822 294
Find us in
Stone
Town, between Africa House and Hotel
Serena, opposite Amore Mio. |
|