Do not reply to this email address. If you would like to get in touch please use busara@busara.or.tz
Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

Busara symbol - click for home page

BUSARA NEWSLETTER

March 2011

Katika toleo hili :
SzB logo

>>> Kiswahili hapa
>>> English here

Tamasha la Sauti za Busara 2011

topback to the top

Muziki wa Kiafrika chini ya Anga ya Kiafrika

carnivalparade
Carnival Parade around Zanzibar Photo by: Peter Bennett

Tamasha la nane la Sauti za Busara lilifanyika Zanzibar kutoka tarehe 9 – 13 Februari  2011. Tamasha hilo lilianza na maandamano ya ufunguzi yaliyovutia kila mmoja yakipita barabarani mjini Zanzibar, katika maandamano hayo vikiwemo vikundi vya sanaa kama  Beni, watembeaji, wachekeshaji wa kiitalia,wacheza mchezo wa copoeira,  pamoja na wanadada wa kienyeji wenye miamvuli yenye mapambo, wote hao wakifuatana na kimbunga cha msimu kuosha ufunguzi wa tamasha na kulibariki tamasha kwa mtindo wa kiafrika.


Kwa mara nyingine tena, tamasha liliendelea na sifa yake kwa muziki wa laivu kwa siku tano kutoka kwa kile kilichobora ambacho Afrika inakitoa. Kila siku watu wazidio elfu tano walikusanyika katika makuta ya zamani ya mji mkongwe, wakiwemo wasanii, mapromota, waandishi wa habari wa kitaalamu, wasafiri, watalii, na hata wenyeji wa kizanzibar, tulikutana kama taifa moja – ndani ya handaki la Afrika.


Nje ya Ngome Kongwe, mji wote ulikuwa umavuma kwa vidokezeo vya Busara: madarasa ya uchezaji, mazoezi ya taarab, mafunzo ya uandishi wa habari, mikutano na wataalamu, maonyesho ya filamu za muziki, makongamano ya wasanii wenyeji na wale wa kimataifa, maonyesho ya mitindo, na mazoezi ya yoga ya kujikunjuwa na kuwa tayari kwa kudansi.
Pongezi nyingi na shukurani kwa kila mmoja ambaye alisaidia kulifanya hili tamasha kuwa furaha kubwa na kivutio na pia tamasha hilo kuwa ndo lilifanikiwa zaidi mno. Maoni kutoka kwa watembezi na watalii, wapya na wa tangu mwanzo, wamekubali kuwa tamasha la nane la mara hii lilikuwa tamu sana, wakilisifu tamasha hilo, kuongezwa kwa burudani nyengine, na taasisi bora inayosimamia, sauti za muziki zenye kiwango cha juu.

 

Ni wa kuthaminiwa sana Zantel, wahisani na wadhamini wote, wasanii wote, watazamaji, bodi ya wadhamini, wafanyakazi wote, na vyombo vyote vya habari vya ndani na nje ya nchi ambavyo viliendelea kutoa habari za Busara. Shukrani kwako wewe pia, marafiki wote, na wote wanaotutakia mema  Sauti za Busara ulimwenguni kote miaka yote.

Wasanii Bora 2011

Hawa ni wasanii waliopendwa na watazamaji wetu.

Orchestre Poly Rythmo de

Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin) Photo by: Eirik Folkedal

Sinachuki Kidumbaki

Sinachuki Kidumbak (Zanzibar) Photo by: Peter Bennett

Culturemusic
Bi Kidude (Zanzibar) Photo by: Peter Bennett
MaulidiyaHomu
Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar) Photo by: Masoud Khamis

Christine Salem

Christine Salem (Reunion) Photo by:Anoop Singh

Jagwa Music

Jagwa Music (Tanzania) Photo by: Eirik Folkedal

Sousou Maher

Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden) Photo by: David Murphy

YaabaFunk
Yaaba Funk (UK) Photo by: Peter Bennett
Kwani Experience

Kwani Experience (South Africa) Photo by: David Murphy 

Sukiafrica
Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Africa/Far East) Photo by: Peter Bennett

Bismillahi

Bismillahi Gargar (Kenya) Photo by: Peter Bennett

Mlimani Park

Mlimani Park Orchestra (Tanzania) Photo by: Peter Bennett

Otentikk Street Brothers (Mauritius) Photo by: Anoop Singh 

Twanga Pepeta

African Stars Band (aka Twanga Pepeta) (Tanzania)  Photo by: Eirik Folkedal

Blick Bassy

Blick Bassy (Cameroon) Photo by: David Murphy 

     

Kwa habari za tamasha

Angalia picha bora za 2011 kwenye tovuti yetu.

 
   
Facebook logo

Sauti za Busara

tunapatikana katika

Facebook

Vidokezo vya tamasha 2011

 

Kwa uhondo wa video za tamasha tembelea
YouTube logo
Sauti za Busara 2011 video

 

Sauti za Busara 2012

topback to the top

 

blackroots

Tarehe za 2012

... Tarehe iliyopangwa kwa tamasha la 9.

JUMATANO - JUMAPILI

8 - 12 February 2012

 

Wito kwa Wasanii – Sauti za Busara 2012

Wito kwa wanamuziki wote wa kiafrika. Kamati ya uchaguzi wa wasanii hukutana ogasti mwanzoni kuamua mpangilio wa wasanii kwa 2012. Ukiambatanisha maombi yako tunahitaji nakala za rekodi yako moja au mbili za hivi karibuni(CD or DVD) picha na maelezo mengine. Tuma maombi sasa hivi kabla ya tarehe 31 Julai 2011

Wito kwa filamu za muziki wa Afrika

Tunatafuta vipengele vifupi vya filamu kutoka pande zote za Afrika na kwingineko duniani. Hii  inaweza kuwa sehemu ya muziki na video, kumbukumbu ya matamasha, taarifa za au filamu zaidi za  majaribio. Tuma maombi wakati wowote kuanzia sasa  kabla Septemba 30, 2011

 

JagwaMusic
Jagwa Music (Tanzania) Photo by:Peter Bennett

WOMEX - Wito kwa Mapendekezo

topback to the top

Womex Call for Proposals

WOMEX – the World Music Expo / Copenhagen, Denmark / 26 – 30 Oct 2011

WOMEX ni " Soko muhimu la kimataifa na duniani kwa muziki wa kila aina.  Soko hili la kimataifa huleta pamoja wataalamu kutoka ulimwenguni kote na watu wa aina zote, muziki wa makabila ya jadi na pia ni pamoja na matamasha na mikutano, na filamu. Huchangia kwa mitandao kama. njia bora ya kukuza muziki na utamaduni wa kila aina katika mipaka. "UNESCO Global Alliance for Cultural Diversity

Kufanywa katika Berlin na kusafiri katika bara la Ulaya: Toleo la 16 la WOMEX Copenhagen, Denmark Oktoba 2010 kutakuwa na zaidi ya wajumbe 2,440 kutoka nchi zaidi ya 90, maonyesho 650, mikutano na maonyesho ya tamasha 59 katika majukwaa 6.

Kama ungependa kuonyesha au kushiriki katika Mkutano au uoneshaji wa filamu katika WOMEX 11, mwisho wa kuwasilisha maombi ni Ijumaa 15 mwezi wa nne 2010.
http://lnk.womex.com/how-to-propose

Kama una mpango wa kuhudhuria, kuwa wa mwanzo kujiandikisha mapema.

http://lnk.womex.com/register

 

Shukrani kwa wadhamini wetu

topback to the top

Waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara wanayofuraha kuwashukuru kwa moyo mkunjufu wadhamini na wafadhili wetu kwani bila wao sisi peke yetu tusingeweza.

Tamasha laSauti za Busara 2011 limedhaminiwa na:


Principal Sponsor

Zantel

Main Sponsors

Norwegian Embassy
hivos GoeTheInstitut from the american people ACP Music Festivals network

Logo Sponsors

Memories of Zanzibar
cultures france
Gallery Tours logo
Zanzibar Grand Palace Hotel
Grand Malt

Media Sponsors

fROOTS zg-design Times FM

Shukrani kwa:

British Council, The German Embassy, SMOLE II, Southern Sun Dar es Salaam, Coastal Aviation, Ultimate Security, Azam Marine, Fly 540, Tabasam Tours, Stone Town Traders, Stone Town Café, Mercury’s Restaurant, Archipelago Café & Restaurant, Monsoon Restaurant, Zanlink, ZG Films, Capital TV, Dhow Countries Music Academy, Linear Velocity, Footcandles, www.zanzibar.net

Wasiliana nasi

topback to the top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana njia ya Uwanja wa Ndege, mkabala na Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294


Tafadhali tuma ujumbe huu kwa marafiki ambao wangependa kusoma ujumbe huu.Kujiunga au kujitoa katika orodha yetu – andika barua pepe yako katika kiboksi kupitia
www.busaramusic.org