Habari hii itatumwa kwa watu 54,020 waliojisajiri

     Emeil yako haifunguki sawasawa, fungua hapa

Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Tamasha linakuja
Tiketi na Pasi
Taarifa kwa wageni
Maandamano ya ufunguzi
Mualiko wa ufunguzi wa tamasha
Matukio ya ziada ya busara
buy ticket button 
Movers & Shakers
Pati baada ya tamasha
Habari motomoto
Vibali kwa waandishi wa habari
Shukrani kwa wadhamini wetu

Tamasha linakuja

Top

Mambo yote yapo tayari kwa ajili ya shamrashamra za kufurahia muziki wa kiAfrika katika tamasha la tisa la sauti za busara  ambalo litaanza tarehe 9-12 ndani ya mji mkongwe wa Zanzibar. Zaidi ya wanamuziki 300 (vikundi 31) vitafanya maonyesho Ngome Kongwe. Angalia ratiba ya tamasha festival timetable au pata kopi yako ya programu ya tamasha  (pdf 20MB) hapa

 

Tiketi na Pasi

Top

festival parade

Tiketi zinauzwa kwa kasi! Ukumbi wa ngome kongwe una idadi kamili. ili kuwa na uhakika wa kuwepo katika tamasha tunapendekeza kuwekesha tiketi yako ya tamasha zima kwenye mtandao (mwisho kupatikana tarehe 31/01/2012) kwa kila tiketi ya tamasha zima au ya VIP utapata zawadi ya kitabu cha maelezo (festival Program)
Wekesha tiketi yako hapa: :ZANZIBAR-ISLANDS.COM

 
 

Taarifa kwa wageni

Top

say no to drugs models

Hali ya hewa ya Zanzibar katika kipindi kuanzia tarehe 8-12 mwezi wa pili ni Joto. Ni Muda wa kuwa tayari kwa ajili ya safari yako. Angalia ukurasa huu  Visitor Info ili upate taarifa na upange safari yako na kuwa rahisi, tafuta punguzo kwa malazi na safari.

Songlines Festival Tours (Europe) or Zanzibar Festival Tours (North America) vilevile watakusaidia kupanga safari yako mpaka kwenye tamasha. Kwa maelezo ya malazi kwa hotel za Zanzibar tunapendekeza Tabasam Tours

 

Maandamano ya ufunguzi

Top

say no to drugs models

Maandamano makubwa  ya ufunguzi yataanza saa 10 jioni siku ya Al hamisi ya tarehe 9februari katika viwanja vya kisonge, karibu na michenzani. Yataelekea mji mkongwe katika ukumbi wa ngome kongwe! Vaa kinyago au manyoya, chora uso wako. Au ungana na kikundi cha reki kwa kupaka mafuta meusi mwili mzima!! Vyovyote itakavyokuwa, usikose kushiriki maandamano ya ufunguzi!

street parade
 

Mualiko wa ufunguzi wa tamasha

Top

Shukrani ziwaendee wanachama wetu wote wa newsletter, tunakualikeni katika siku ya ufunguzi bure na rahisi kupata bofya hapa ili utoe nakala yako.

 

Matukio ya ziada ya busara

Top

busara xtra logo

Si kwamba tamasha linafanya maonyesho. Ni mseto wa matukio tofauti ambayo yatafanyika Zanzibar nzima. Siku ya Jumatano ya tarehe 8/02/2012 kumbi tofauti zitafungua milango yao kwa ajili ya kukaribisha tamasha, ikiwemo Nadi Ikhwan Safaa (aka Malindi Taarab), Maulidi ya Homu ya Mtendeni, Black Roots, Culture Musical Club na wengi zaidi.

Black Roots   Maulidi ya homu ya mtendeni
 

Movers & Shakers

Top

kila siku ya tamasha, tamasha linaendesha kongamano lijulikanalo kama Movers & Shakers, lengo kuu la kongamano hili ni kuwapa fursa wataalamu wa muziki kujadili maswala tofauti yahusuyo muziki, kubadilishana mawazo na ubunifu kwa wanamuziki wa afrika mashariki na kwengineko. Vikao ni bure kwa wasanii waalikwa wageni na wenyeji, mameneja, mapromota, waandaaji wa matamasha, waandishi wa habari na wataalamu tofauti. Mwaka huu tunaangazia katika kufikia malengo ya maendeleo ya sanaa na mbinu mpya.
Kama ni mtaalamu na unahitaji kushiriki, wasiliana nasi kwa busara@busara.or.tz
Kwa taarifa zaidi angalia Movers & Shakers

 

Pati baada ya tamasha

Top

finale party poster

Jumuika na wasanii na wafanyakazi wa tamasha katika fukwe maridhawa, kaskazni mwa Unguja, Kendwa Rocks siku ya Valentine Day ,tarehe 14 ferbruari  kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 10 asubuhi kwa ajili ya pati.

kendwa rocks full moon party
 

Habari motomoto

Top

facebook icon
twitter icon

Katika kipindi cha tamasha, timu ya Busara itakuletea taarifa tofauti, picha na video, habari na mahojiano. Fuatilia tamasha katika twitter@sautizabusara na penda katika facebook.
Jiunge na mazungumzo katika Twitter, tumia #sautizabusara na kuwa rafiki wa Sauti za busara katika Facebook, rafiki atakaependa busara katika facebook atapata zawadi kutoka Busara.

 

Vibali kwa waandishi wa habari

Top

photographer

Tunakaribisha maombi kutoka kwa waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi ili kushiriki kwenye tamasha. Angalia press accreditation katika tovuti yetu na mwisho wa maombi ni 30 januari 2012.

parade
 
 

Shukrani kwa wadhamini na wafadhili

Top

Waandaaji wa tamasha wanayofuraha ya kukiri kwa imani yao yote ya msaada kutoka kwa wadhamini na wachangiaji, bila wao tamasha namba moja afrika mashariki lisingekuwepo. Sauti za Busara 2012 linawezeshwa na

Principal Donors
Norwegian Embassy

Main Donors
hivos GoeTheInstitut Roskilde festival

Sponsors
Grand Malt logo Toyota logo cba logo
African Leisure Centre memories of Zanzibar zanzibar grand palace hotel
Maru maru Fly540  

Donors
GoTheInstitut logo   from the american people   French Embasy Tz
Media Partners
fROOTS   Times Radio FM

Shukrani kwa:
SMOLE II, Zanlink, Azam Marine, Embassy of France, ZanAir, Multi-Color Printers, Ultimate Security,  Tabasam Tours, Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Southern Sun Dar es Salaam, Mercury's, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, www.zanzibar.net


Kama ungependa nembo yako kuwa katika  tovuti yetu na muendelezo wa habari, bonyeza hapa

 

Wasiliana nasi

Top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

facebookyoutube logo

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana njia ya Uwanja wa Ndege, Mkabala na Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Angalia mengi katika tovuti yetu ambayo inajumuisha Chati za Muziki, Matamasha bora ya Muziki Afrika, Kalenda ya matukio ya sanaa Afrika Mashariki, Picha  na video fupi


Tafadhali tuma barua pepe hii kwa watu ambao wangependa kupata habari hii. Kujiunga au kujitoa tafadhali andika barua pepe yako katika kiboksi hiki katika www.busaramusic.org