This newsletter is sent to 55,234 subscribers

      Email not displaying correctly, view it in your browser

Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Sauti za Busara 2012
Picha na Video muhimu 2012
Habari kuhusu tamasha la 2012
Wito wa mapendekezo WOMEX
Shukrani kwa Wafadhili na Wadhamini
Wasiliana nasi
Penda ukurusa wetu katika facebook

Sauti za Busara 2012

Top

“Hali ilikuwa nzuri sana … na maonyesho yalifana sana.” Brenda Wambui, Hii ni Afrika:  ujumbe huu umeungwa mkono na watu wengi kati ya 20,000 ambao walihudhuria tamasha la kihistoria la toleo la  9  la Sauti za Busara, Februari 2012.

Zaidi ya wasanii 400 walipanda katika  jukwaa kuu, hii ilipambwa na maandamano ya ufunguzi wa tamasha katikati ya mitaa ya Mji Mkongwe na kumalizikia Ngome Kongwe, tamasha lilionyesha uhalisia ,tofauti wa muziki kutoka bara la Afrika. Kila onyesho lilikuwa la kusisimua na kuvutia

2012 audience photo 2012 festival parade

Watazamaji wa usiku

Maandamano ya ufunguzi

Kwa sisi waandaaji wa tamasha, baada ya kuwa na kazi ngumu ya  utafutaji pesa kwa mwaka mzima, tunajivunia kwa jinsi tamasha lilivyofana. Watu ni wengi waliohudhuria kwa kila siku, wasanii walikuwa bora, na pamoja na  msaada kutoka kwa marafiki zetu kutoka Roskilde Festival Charity Society kuhakikisha tulikuwa na usalama bora na huduma za usalama kwa wageni wetu.

Busara Promotions inapenda kuwashukuru wafanyakazi wote na watazamaji wote kutoka mbali na karibu kwa kujumuika nasi, kushirikiana nasi katika uzoefu wa Tamasha la Muziki la Afrika chini ya Anga la Afrika.

Busara Promotions inatoa shukrani za dhati kwa wasanii wote walioshiriki: Nneka, Super Mazembe, Ary Morais, Camirata Group, Seven Survivor, Jagwa Music, Fredy Massamba, Lumumba Theatre Group, Utamaduni JKU, Leo Mkanyia, Mkota Spirit Dancers, Ndere Troupe, Shirikisho Sanaa,  Tunaweza Band, Tumi & The Volume, Swahili Vibes, Chébli Msaïdie, Kozman Ti Dalon, Tandaa Traditional Group, Jembe Culture Group,  Skuli ya Kiongoni, Wanafunzi wa SOS, Tausi Women's Taarab ft Bi Kidude, Juhudi Taarab, Ogoya Nengo, Kidumbak JKU, Qwela, Hanitra, Mashauzi Classic na FM Academia– wote walipanda jukwaani na kuimba muziki wa moja kwa moja( 100% live) katika maonyesho yao kupitia “Sauti za Busara”

 

Picha na Video ya Mambo muhimu 2012

Top

Muda mfupi mzuri kutoka Sauti za Busara 2012. Furahia uzoefu wa Sauti za Busara 2012

youtube play button

Picha za mwaka huu: picha kutoka kati ya watazamaji wetu pamoja na maonyesho.

Lumumba theater group Mkota spirit dancers Ndere Troupe

Lumumba Theatre Group (Tanzania)

Mkota Spirit Dancers (Pemba)

Ndere Troupe (Uganda)

Night time audience Night time audience Tumi and The Volume

Watazamaji wa usiku

Watazamaji wa usiku

Tumi & The Volume (South Africa)

Freddy Massamba ni mmoja wa wasanii walioshiriki katika tamasha la 2012, Ungana nae ili uone jinsi alivyokonga nyoyo za watazamani wa Sauti za Busara na Zanzibar kwa ujumla.

Fredy Massamba play button
 

Habari katika vyombo vya habari 2012

Top

Tamasha limeleta furaha na pilikapilika ndani ya Afrika Mashariki na kwengineko.
Haya ni baadhi ya maneno kutoka kwa wageni, wasanii na waandishi wa habari.

“Kila tamasha linalofanyika Afrika ni bora. Kuleta vikundi mbali mbali na kutoka nchi mbali mbali za Afrika – mashariki , kusini kaskazini na magharibi na kuwaleta sehemu moja hii ni kazi ngumu. Hilo ni lazima lifanyike na tunahitaji kufanya zaidi ya hapo. Sio katika fani ya muziki ila kwa watu wa Afrika kwa ujumla. Hiki ni kitu tunachotakiwa kujifunza: Tunahitaji kuwa pamoja.”Nneka (Nigeria/Germany)

Nneka (Nigeria) audience pic

Nneka (Nigeria)

Watazamaji wa usiku

“ Lilikuwa onyesho la pekee kuhudhulia. Mke wangu na mimi sote tulijisikia furaha, upendo kwa muziki wa Kiafrika na watu wake. Tunaamini hisia hizi zitadumu hadi tamasha lijalo.” Nicolai Sosnowski mgeni wa tamasha.

Kwa habari zingine, magazetini na tovuti, tembelea moja kati ya hizi:

Mambo magazine
This is Africa
The East African
the-star.co.ke

 

 
 

Wito wa mapendekezo WOMEX

Top

WOMEX

WOMEX ni soko muhimu la kimataifa la aina ya muziki wote duniani. Soko hili la kimataifa huwakutanisha pamoja wataalam kutoka pande zote duniani katika muziki wa folk na muziki wa asili na hujumuisha maonyesho , mikutano na maonyesho ya filamu. Hii itachangia mtandao kwa maana ya kutangaza muziki na aina zote za utamadun ." UNESCO Global Alliance for Cultural.

Toleo la 17 la WOMEX lilifanyika Copenhagen, Denmark mwezi wa  Oktoba 2011 kulikuwa na washiriki zaidi ya 2,250 kutoka zaidi ya nchi 98, maonyesho 700,  mikutano na washiriki 60 katika majukwaa 6. Kama ungependa kushiriki katika mikutano au filamu yako kuonyeshwa WOMEX 12, mwisho wa kutuma mapendekezo ni Ijumaa tarehe 13 April 2012.
http://lnk.womex.com/how-to-propose

Kama una mpango wa kushiriki, kuwa wa mwanzo kujiandikisha ili kufanya matumizi yako kupungua.
http://lnk.womex.com/register

 

Shukrani kwa Wafadhili na Wadhamini

Top

Busara Promotions inapenda kukiri kwa imani, maoni na msaada mkubwa wa wahisani na wadhamini, bila ya hawa Sauti za Busara 2012 isingewezekana.

Principal Donors
Norwegian Embassy

Main Donors
hivos   GoeTheInstitut Roskilde festival

Sponsors
Grand Malt logo Toyota logo cba logo
African Leisure Centre memories of Zanzibar zanzibar grand palace hotel
Maru maru Fly540  

Donors
GoTheInstitut logo   from the american people   French Embasy Tz
Media Partners
fROOTS   Times Radio FM

Thanks to:
SMOLE II, Zanlink, Azam Marine,  ZanAir, Kendwa Rocks, Hotel Serena, Multi-Color Printers, Ultimate Security, Tabasam Tours, Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Mercury's, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, Zanzibar Insurance Corporation, Ally Keys, Rumaisi Hotel, zanzibar.net
With special thanks to Chris Bowden, Rajesh Vohra


 

Wasiliana nasi

Top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Find us on the airport road, opposite Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Like us on facebook

Top

facebook

Kwa habari motomoto na picha , tutembelee katika ukurasa wetu wa facebook na ungana nasi kwa wakati mnono wa tamasha. Kama bado hujapenda  basi ni wakati wako sasa kupenda ukurasa wetu kupitia www.facebook.com/sautizabusara
Tafadhali tuma barua pepe hii kwa mtu yeyote ambae angependa kusoma habari hii.

youtube logo

Angalia vitu vyengine vya ziada kwenye Music Charts, Top African Music Festivals, East African Arts Events Calendar, photo galleries na video clips


Please forward this mail to friends who may be interested. To subscribe or unsubscribe to our newsletter – just type your email address in the box at
www.busaramusic.org