Jarida hili linatumwa kwa watu 57,789

Email not displaying correctly, view it in your browser

Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Mwisho wa wito kwa wasanii: Sauti za Busara 2013
Pati ya shukran kwa marafiki wa busara
Wito wa wahisani & wadhamini wa tamasha
Nafasi za kazi
Uzinduzi wa CD: Bongo Hotheads
Kalenda ya matamasha Zanzibar
Wasiliana nasi
 

Mwisho wa wito wa wasanii: Sauti za Busara 2013

Top

Sauti za Busara ni tamasha la muziki namba 1 Afrika Mashariki. Tamasha la 10 litafanyika Zanzibar ndani ya mji mkongwe katika ukumbi wa Ngome Kongwe kuanzia tarehe 14 - 17 februari 2013.

Sheherekea hazina ya muziki wa kiafrika, tamasha litaonyesha wasanii bora, wanaofanya maonyesho yao moja kwa moja kwa asilimia 100 (live), kutoka ijumaa mpaka jumapili, saa 11 mpaka saa 7 usiku. Na mengineyo zaidi ikiwemo filamu za muziki wa afrika, vyakula kutoka kwa wenyeji na maduka ya sanaa, warsha kwa ajili ya kuongeza ujuzi, mikutano ya wataalam wa sanaa, na vilevile Matukio ya ziada ya busara yahusuyo muziki na mambo ya utamaduni yatakayoandaliwa na wenyeji na kufanywa katika sehemu mbalimbali za mji wa Zanzibar.

Wanamuziki wa kiafrika kutoka sehemu yoyote duniani wanakaribishwa kufanya maombi ya ushiriki kwa ajili ya kufanya maonyesho yao katika jukwaa la sauti za busara, kwa kukamilisha maombi kwenye mtandao na kutuma nakala za kazi ambazo zitufikie kabla ya tarehe 31/7/2012. Kamati ya uchaguzi itafanya uteuzi mwezi wa nane na mwezi wa tisa wasanii wote waliochaguliwa watajulishwa.

Sauti za Busara 2013 postcard

Sauti za Busara 2013 postcard

 

Pati ya shukran kwa Marafiki wa Busara

Top

Kwa kuwashukuru marafiki wa busara na wale wote waliosaidia tamasha la busara 2012, tunaandaa pati katika ofisi za busara siku ya ijumaa ya tarehe 22 ya mwezi wa sita. Kutakuwa na nakala ya filamu “More than a festival” bila shaka tamasha linaleta mapinduzi ya kimuziki, shamrashamra na mkusanyiko wa watu.

Kwa mualiko tu! Barua pepe busara@busara.or.tz kama unahitaji mualiko.

Nighttime Audience (photo: Robin Batista)

Nighttime Audience (photo: Robin Batista)

 

Wito kwa wahisani & wadhamini wa tamasha

Top

Busara on stage (photo: Stephanie-Tinga-Baron-Wilson)

Busara on stage (photo: Stephanie-Tinga-Baron-Wilson)

Tiketi za tamasha kwa kila siku ni shilingi 3000 kwa mtanzania. Katika kusaidia uwepo wa tamasha tunategemea michango kutoka kwa wahisani na wadhamini.

Tamasha linathamini  wahisani na wadhamini wote waliopo katika tovuti ya sauti za busara (mwezi wa januari tu tovuti ya www.busaramusic.org ilitembelewa mara milioni 3.4) vilevile na jarida (kutumwa kwa watu 57,000 dunia nzima) na kitabu cha tamasha, mabango ya matangazo, matangazo ya jukwaani, taarifa kwa vyombo vya habari na mengineyo…

Kama unapendelea kuwa rafiki na tamasha, barua pepe marketing@busara.or.tz kwa taarifa zaidi

 

Nafasi za kazi

Top

Mkurugenzi mtendaji, Busara Promotions

Muda wote, mkataba wa miaka miwili, kuanza tarehe 6/8/2012. Kutoka taifa lolote (mwenye uzoefu angalau wa miaka 3 kwenye NGO / uongozi wa sanaa). Mwenye kuwajibika katika shughuli za utawala na fedha wa NGO. Tuma barua na CV yako kwa director@busara.or.tz kabla ya tarehe 30/06/2012.

Kwa taarifa zadi bonyeza hapa

Meneja wa ufundi, Busara Promotions

Muda wote, mkataba wa miezi sita, kuanza tarehe 1/10/2012. Kutoka taifa lolote (mwenye uzoefu angalau wa miaka 5). Kuwa mwenye dhamana ya kutoa msaada wa kiufundi kwa Sauti za busara na miradi mingine. Tuma barua na CV yako kwa director@busara.or.tz kabla ya tarehe 31/07/2012.

Kwa taarifa zadi bonyeza hapa

Ofisa habari,Busara Promotions

Muda wote, mkataba wa miezi sita, kuanzia tarehe 1/10/2012. Kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. Tuma CV yako na barua kwa busara@busara.or.tz kabla ya tarehe 31/07/2012.

Kwa taarifa zadi bonyeza hapa

 
Lighting work (photo: Masoud Khamis)

Lighting work (photo: Masoud Khamis)

Backstage soundbooth (photo: Masoud Khamis)

Backstage soundbooth (photo: Masoud Khamis)

Busara Promotions inazingatia usawa wa kijinsia katika nafasi za kazi kwa wenyeji vyovyote iwezekanavyo. Tafadhali zingatia muombaji atakayekuwa makini pekee ndiyo.

 

Uzinduzi wa CD: Bongo Hotheads

Top

Jagwa Music Bongo Hotheads CD cover

Jagwa Music Bongo Hotheads CD cover

Kutoka katika kitongoji cha Mwananyamala ndani ya jiji la Dar es salaam, wanafahamika kwa jina Jagwa Music hufanya maonyesho yao ya kuvutia, mpiga kinanda huwapagawisha watu zaidi na kinanda chake  aina ya Casio na watu watatu wakiwa mbele, wachezaji wawili na muimbaji, akishusha nyimbo zinazoelezea maisha ya mjini, usaliti katika mapenzi na ushirikina. Tazama filamu kutoka YouTube hapa

Jagwa Music si tu wana umaarufu katika viunga vya Dar es Salaam lakini wameweza kuvuta hisia za watu katika tamasha kubwa la kimataifa barani ulaya Roskilde Festival. Kwa mara ya kwanza Cd yao inapatikana kimataifa, "Bongo Hotheads" wametoa utajiri wao wa mashairi. Pata nakala yako maridhawa sasa.

"A spirited, exuberant debut like nothing you’re likely to have heard before" (The Arts Desk)

 

Kalenda ya matamasha Zanzibar

Top

Tamasha letu si pekee ndani ya mji mkongwe:

ZIFF logo
15th ZIFF Festival of the Dhow Countries:
7 - 15 July, 2012

Tamasha kubwa la filamu na sanaa Afrika Mashariki, wanatoa wigo mpana wa ubunifu ndani ya Afrika na nje ya Afrika. Soma hapa

 

Jahazi logo
2nd Jahazi Literary and Jazz Festival:
31 Aug – 2 Sept, 2012

Mwisho wa wiki maridhawa wa ufunguzi wa tamasha la Jahazi, simulizi za hadithi, usomaji wa mashairi, semina za muziki na chakula cha join kwa VIP... Soma zaid

 

Daytime Audience (photo: Pernille Barendtsen)

Daytime Audience (photo: Pernille Barendtsen)

Angalia kalenda kwa Matukio ya sanaa Afrika Mashariki

Angalia kalenda kwa Matamasha ya Muziki Afrika

 

Wasiliana nasi

Top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana barabara iendayo uwanja wa ndege, mkabala na Golf Clubb

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

facebook

Tembelea ukurasa wetu wa facebook na waambie wale wote wanaopenda  kutembelea ukurasa wa Busara wa 2013.
Hongera Busara! Thumbs up na “ipende” busara kwenye www.facebook.com/sautizabusara

youtube logo  

Vitu vingine zaidi katika tovuti yetu ni Music Charts, Top African Music Festivals, East African Arts Events Calendar, photo galleries na video clips


Tafadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org