Jarida hili linakwenda kwa watu 60,401

Email not displaying correctly, view it in your browser

Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Sauti za Busara 2013
Orodha ya wasanii
Wito kwa wachangiaji na wadhamini
Wito wa mwisho wa filamu za muziki
Tiketi & Pasi
Rafiki wa Busara
Movers & Shakers
Maduka & Wafanyabiashara
Matukio tofauti
Taarifa kwa wageni
Wachangiaji na wadhamini
Wasiliana nasi
 

Sauti za Busara 2013

Juu

Sauti za Busara 2013
Februari, jua linachomoza katika ukanda wa bahari ya Hindi, mawimbi yanatiririka katika mchanga mweupe. Vua viatu vyako na jiachie katika kisiwa cha marashi ya karafuu.Tarajia chakula freshi kutoka baharini. Je utapendelea nini kati ya hivi, samaki aina ya changu au pweza?

Sauti za Busara huwaleta watu pamoja kusheherekea utajiri wa aina mbalimbali ya muziki wa Afrika. Sauti za Busara inafurahia sifa za kimataifa kutokana na ratiba zake na viwango vya muziki, hii  ikiwa pamoja na mafunzo ya ufundi, sehemu maridhawa  ya tamasha. Toleo la 10 la februari 2013 litawaleta wasanii bora walio wahi kushiriki miaka tisa iliyopita ambao walipendwa na watazamaji.

Tamasha litafanyika ndani ya Mji Mkongwe  Zanzibar, jukwaa kuu litakutanisha mamia ya wasanii kutoka bara la Afirka.Kutakuwa na filamu za muziki na wanamuziki wa Afrika  zitakazoonyweshwa amphitheatre ndani ya Ngome Kongwe.Wakati  huo huo katika viunga vya mji wa Zanzibar kutakuwa na matukio mbalimbali ijulikanayo kama Busara Xtra.

SzB logo SzB postcard Festival Audience
 

Orodha ya wasanii

Juu


340ml
CHEIKH LԴ
SENEGAL
340ml
MLIMANI PARK ORCHESTRA
TANZANIA
SUPER MAYA BAIKOKO
SUPER MAYA BAIKOKO
TANZANIA
ATONGO ZIMBA
ATONGO ZIMBA
GHANA / UK
340ml
PETER MSECHU
TANZANIA
340ml
WAKWETU JAZZ VIBES
TANZANIA
Wazimbo
WAZIMBO
MOZAMBIQUE
340ml
SOUSOU & MAHER CISSOKO
SENEGAL / SWEDEN
340ml
OWINY SIGOMA BAND
KENYA / UK
340ml
MOKOOMBA
ZIMBABWE
340ml
LUMUMBA THEATRE GROUP
TANZANIA
Nawal
NAWAL & LES FEMMES DE LA LUNE
COMOROS / FRANCE

Wasanii wengine zaidi watatangazwa baadae. Kwa habari zaidi usikose kuangalia ukurasa wa tamasha

 

Wito kwa wachangiaji na Wadhamini

Juu

Wito kwa wachangiaji na Wadhamini
Bei ya tiketi kwa watanzania ni shilingi elfu 3,000 ili kumrahisishia aweze kuhudhuria tamasha kila siku. Tunategemea viingilio vya wageni wa kimataifa, wachangiaji na wadhamini.

Marafiki wa Busara huwekwa kwenye jarida (e-newsletter) na katika kurasa mbalimbali kwenye tovuti yetu, kitabu cha tamasha, ukumbini (ngome kongwe), video, matangazo ya ukumbini, sahihi za barua pepe,  vyombo vya habari na mengineyo. Wachangiaji na wadhamini wa tamasha hupata pasi za kuingillia na mialiko ya VIP, mkutano wa wadau wa muziki na matukio mengine muhimu.

Kama unapendelea kuwa miongoni mwa marafiki wa Busara 2013, tafadhali tuma kwenda busara@busara.or.tz kwa taarifa zaidi.

 

Mwisho wa wito wa filamu za muziki

Juu

Tamasha huonyesha filamu za muziki na video ngome kongwe. Upande wa pili wa ngome kongwe (Amphitheatre) watazamaji hupata nafasi ya kuangalia filamu kutoka sehemu zote za Afrika.

Filamu ndefu, video za muziki, makala za muziki, matamasha na filamu za uchunguzi.
Tunatafuta filamu ambazo:

  • Zinaelezea kuhusu muziki au wanamuziki kutoka bara la Afrika na kwingineko.
  • Zinazoelezea thamani na utofauti wa muziki wa Afrika Mashariki na nje
  • Filamu za muziki zenye kupendwa na watazamaji wenyeji na wageni.
  • Filamu zenye muonekano bora, sauti yenye ubora na muziki wenye asili ya Afrika.
  • Filamu mpya na ambazo hazijawahi kusikika, na wasanii chipukizi.
  • Kwa lugha ya kigeni ni bora ikatafsiriwa kwa Kiswahili au kingereza

Maombi yako yatafanyiwa kazi na kamati ya uchaguzi kama umekamilisha maombi yako ikiwemo nakala za DVD mbili kabla ya Tarehe 16 Novemba 2012

 

 

Tiketi & Pasi: Sasa zinapatikana

Juu

buy ticket button

Ngome kongwe ina idadi maalum, kwa hiyo ili kuepuka usumbufu unaweza kuwekesha tiketi yako mapema. Vile vile tiketi zitauzwa ngome kongwe siku ya Alhamisi ya tarehe 14 februari.

 

Rafiki wa Busara

Juu

Rafiki wa Busara
Tafadhali sadidia Sauti za Busara ikuwe zaidi. Saidia tamasha la muziki la Afrika Mashariki na peleka ujumbe wako kwa wadau wa muziki,  tamaduni na wadau wa sanaa kutoka dunia nzima. Kwa kiasi cha dola za kimarekani 600, tutakupatia uwezo wa kutembelewa katika biashara yako (link) kutoka katika kurasa yetu ya tamasha na jarida letu (e-newsletter). Nafasi ya kujitangaza inapatikana kwenye nakala ya kitabu.

 

Movers & Shakers

Juu

Tamasha linahodhi mkutano wa wadau na wataalam wa sanaa ambao hufanyika kila siku mchana na kutoa nafasi maridhawa kwa wasanii, mameneja, vyombo vya habari na wadau wengine katika kubadilishana mawazo na kutafakari jinsi ya kuimarisha soko la muziki.

 

Maduka na wafanyabiashara

Juu

Nafasi za maduka na wafanyabiashara ni chache kwa mfano vyakula, sanaa, vinyago Bofya hapa kwa maelezo zaidi.

 

Matukio mbalimbali

Juu

Xtra

Kipindi cha tamasha kunakuwa na matukio tofauti: ngoma za asili, maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa na maonyesho ya taarab asilia yanayoandaliwa na wenyeji.

 

Taarifa kwa wageni

Juu


Hapa kuna kila kitu utakachohitaji kwa ajili ya kupanga safari yako:          

Kwa video na vyombo vya habari bonyeza hapa

                                                   

 

Wadhamini na wachangiaji

Juu

Waandaaji wa tamasha wanayofuraha kuwashukuru wachangiaji na wadhamini, bila ya wao Sauti za Busara halitaweza kufanyika. Tumeshapokea ahadi nab ado tunahitaji zaidi.


Mpaka sasa Sauti za Busara 2013 linawezeshwa na:

Norwegian Embassy Hivos
GotheInstitut Grand Malt Memories of Zanzibar

With thanks to Zanlink, Embassy of France, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, AllyKeys Car Hire www.zanzibar.net

 

Contact us

Juu

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3535
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Find us on the airport road, opposite Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

facebook

Thumbs up and “like” us at www.facebook.com/sautizabusara

youtube logo  

See more on our website including Music Charts, Top African Music Festivals, East African Arts Events Calendar, photo galleries and video clips


Please forward this mail to friends who may be interested. To subscribe or unsubscribe to our newsletter – just type your email address in the box at
www.busaramusic.org