Jarida hili limetumwa kwa watu 62,735

Emeil yako huioni vizuri fungua kwenye brauza

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Sauti za Busara 2013
Picha za tamasha 2013
Movers & Shakers
Vyombo vya Habari
Tafiti za watazamaji
Shukrani kwa Wahisani & Wadhamini
Wasiliana nasi
Penda kurasa yetu kwenye Facebook
 

Sauti za Busara 2013

Top

“Ilikuwa ni siku za mwishoni mwa wiki wakati wapenzi wakipata hewa mwanana wakati wakiwa pamoja wakijumuika katika kusheherekea siku ya wapendandao. Pamoja na kutokuwa na wadhamini wa kutosha hali ilihatarisha uwepo wa tamasha, kila kitu kilikuwa sawa kuhakikisha kwamba tamasha la 10 linafana bila ya matatizo yoyote.” Gazeti la Citizen la Tanzania
Kutoka tarehe 14-17 ya mwezi wa February, maelfu ya wapenzi wa muziki kutoka sehemu mbalimbali za dunia walifika Mji Mkongwe, Zanzibar kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara, tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki. Watu waliohudhuria tamasha wanakisiwa kufikia 15,000 ambao walihakikisha wanafika katika tamasha linalojulikana kama tamasha rafiki katika sayari.
Vikundi 24 na zaidi ya wasanii 200 walipanda katika jukwaa kuu na katika maonesho ya mitaani na barabarani ambayo yalipita maeneo mbalimbali, pamoja na kutoa tiketi za bure kwa Wazaznzibar. Kila kitu kilichofanyika Ngome Kongwe (Olf Fort) kilikuwa vya asili, kusisimua na kutoa kitu tofauti na kipya au sauti za kitamaduni, yote haya yalionesha utamaduni wa tamasha: Sauti za Busara.

Night audiences cheikh lo

Watazamaji 2013

Cheikh Lo (Senegal)

Tamasha pia lilionesha filamu ndefu tatu za muziki wa Afrika: ambazo ni Omar Sosa’s Souvenirs from Africa,Benda Bilili! na United States of Africa. Ni filamu ambazo zimeonesha njia tofauti ya kuthamini utajiri mkubwa au mchanganyiko wa muziki wa Afrika, na kupelekea mabadiliko chanya katika jamii kuhusiana na urithi wa muziki.
Busara Promontions inatoa shukrani za dhati kwa wafanyakazi wote na watazamaji kutoka maeneo ya jirani na hata wale waliotoka mbali ambao walifika kufurahi, kushirikiana na kuonesha uzoefu wa muziki wa Afrika chini ya Anga ya Afrika.

Cheikh Lô (Senegal)  Mlimani Park Orchestra (Tanzania)  Khaira Arby (Mali)  Comrade Fatso & Chabvondoka (Zimbabwe)  Culture Musical Club (Zanzibar / Tanzania)  Atongo Zimba (Ghana / UK)  N'Faly Kouyaté (Guinea)  Nathalie Natiembe (Reunion)  Zanzibar Unyago (Zanzibar / Tanzania)  Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte)  Owiny Sigoma Band (Kenya / UK)  Mokoomba (Zimbabwe)  Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania)  Mani Martin (Rwanda)  Burkina Electric (Burkina Faso / USA)  Lumumba Theatre (Tanzania)  Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden)  Super Maya Baikoko (Tanzania)  Peter Msechu (Tanzania)  Wakwetu Jazz Vibes (Tanzania)  Safi Theatre Group (Tanzania)  Wanafunzi wa SOS (Zanzibar / Tanzania). DCMA Young Stars (Zanzibar / Tanzania).

 

Picha za tamasha 2013

Top

Furahia kipindi muhimu kutoka toleo maalumu la kusherehekea miaka 10, Sauti za Busara 2013:
Eneo la picha: picha kutoka kwa baadhi ya watazamaji na maoneosho yaliyovutia zaidi

cheikh lo

Owiny Sigoma Band (Kenya + UK)

Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania)

 

Movers & Shakers

Top

Mwaka huu kipindi cha Movers and Shakers kwa vyombo vya habari na wasanii ilikuwa na lengo maalumu juu ya uhuru wa kujieleza. Chini ya kichwa cha habari “Speaking Truth to Power,” au (“Ongea ukweli wenye nguvu”), waimbaji na wasanii walipata muda wa kujadili masuala ya censorship, changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanamuziki pale wanaposema maovu ya watu waliopo kwenye madaraka katika nchi zao, na umuhimu wa kulinda wasanii na uhuru wa kujieleza.
Msanii wa muziki wa kufokafoka na mshauri Comrade Fatso kutoka nchini Zimbabwe ambae muziki wake umefungiwa kupigwa katika radio na television ya taifa nchini Zimbabwe, alishiriki katika majadiliano siku ya Jumamosi na ambae alifanya onesho kabambe siku ya Jumapili.

movers and shakers

Movers and shakers at Sauti za Busara 2013

 

Vyombo vya habari

Top

 Sauti za Busara inathamini kwa kiwango cha juu mchango wa vyombo vya habari vya aina zote za vya kawaida na vyombo vya habari vya online. Vimefanya tamasha limeenea Afrika Mashariki  na kwengineko.

Tamasha la kimataifa la sauti za Busara,limefanyika kisiwani Zanzibar.
bbc.co.uk/swahili
15 Februari, 2013
Tamasha la kimataifa la sauti za Busara, limefanyika kisiwani Zanzibar. Tamasha hilo liliwashirikisha wanamuziki chipukizi na wakongwe. Tamasha hilo limepata .... read more

audiences 2013

Night audiences

Comrade Fatso (Zimbabwe)

Khaira Arby (Mali)

Kwa habari zaidi,uchambuzi na blog, angalia kwenye kurasa ya Media Coverage.

 

Tafiti za watazamaji

Top

Busara Promotions inawaomba watu wote waliofika katika tamasha kukamilisha maoni/uchambuzi wa watazamani kwa ufupi kupitia online katika http://busaramusic.org/feedback/feedback_2013.php . Hii itatusaidia kuboresha tamasha la mwakani. Tafadhali kamilisha mpaka tarehe 17 ya mwezi March 2013

 

Shukrani kwa Wahisani na Wadhamini

Top

Busara Promotions inapenda kutambua imani, mawazo na mchango na msaada kutoka kwa wafadhili, bila ya wao Sauti za Busara 2013 isingefanikiwa au kuwepo
Sauti za Busara 2013 ilidhaminiwa na:

Norwegian Embassy Hivos
GotheInstitut     American Embassy
         
Precision Air   Memories of Zanzibar   Zanzibar Unique
         
DTB   ChemiCotex   Azam
         
Embassy of Frince   fROOTS
         
Times FM Pride FM CHUCHU FM

With thanks:
Ultimate Security, Monsoon Restaurant, Alliance Francaise,  Zanlink,  SMOLE II, Emerson Spice, Allykeys,  Archipeligo Restaurant, Mercury’s, Stone Town Cafe and ALL journalists and media who attended.

 

Wasiliana nasi

Top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Pia tunapatikana barabara ya airport(uwanja wa ndege), mkabala na club ya Golf Maisara

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Penda kurasa yetu kwenye facebook

Top

Kwa kupata picha za karibuni, tembelea kurasa yetu ya facebook na changia ulivyofurahia tamasha. penda ukurasa wetu hapa www.facebook.com/sautizabusara na ifuatilie Sauti za Busara kwenye twitter www.twitter.com/sautizabusara

facebook

Penda ukurasa wetu hapa www.facebook.com/sautizabusara

youtube logo
twitter

Tafadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org