Jarida hili limetumwa kwa watu 62,735

Emeil yako huioni vizuri fungua kwenye brauza

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Tarehe ya Sauti za Busara 2014
Wito kwa Wasanii Sauti za Busara 2014
Picha na Video Sauti za Busara 2013
Nafasi za kazi za Busara
Muendelezo wa filamu ya Bi Kidude
DOADOA East African Performing Arts Market
Wito kwa wadhamini, wahisani na Marafiki
Wasiliana nasi
Penda kurasa yetu ya facebook
 

Tarehe ya Sauti za Busara 2014

Juu

Kwa mara nyingine tena ndani ya mji wa Zanzibar katika ukumbi ule ule wa Ngome Kongwe patafanyika tamasha la Sauti za Busara. Tamasha la 11 litachukua nafasi yake kwa kuwaleta wasanii bora wenye vionjo vya muziki wa kiafrika kutoka Afrika na kwingineko. Wakati umewadia wa kupanga ratiba yako ya kujumuika nasi Zanzibar kwenye mazingira mwanana ya marashi ya karafuu huku ukifurahia miziki ya kiafrika chini ya anga la kiafrika. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu website

Zanzibar vibes Zanzibar vibes

Zanzibar vibes

Zanzibar vibes

 

Wito kwa Wasanii Sauti za Busara 2014

Juu

Is your music 100% live?
Is your music connected to Africa?
Are you interested in performing next February in Zanzibar?
If you can answer yes, yes, yes – then please read on...

 Maombi sasa yanapokelewa kwa ajili ya ushiriki wa tamasha la 11 la Sauti za Busara
Miaka iliyopita wanamuziki zaidi ya 350 wamefanya maonyesho yao wakiwemo:- Cheikh Lo, Khaira Arby, Mokoomba, Samba Mapangala, Nneka, Didier Awadi, Bassekou Kouyate, Jagwa Music, Tumi & the Volume, Fredy Massamba, Thandiswa, Culture Musical Club, na wengineo tamasha linasisitiza upigaji wa moja kwa moja na si playback. Zingatia: tunapokea maombi mengi kila mwaka. Wasanii wote lazima wajaze fomu ambazo zinapatikana kwenye tovuti yetu na kututumia nakala ambazo inabidi zitufikie kabla ya tarehe 31/07/2013. Jopo la uchaguzi litakaa mwezi wa nane na waombaji wote kujulishwa kwa njia ya mtandao mwezi wa Tisa.
Tafadhali tuma nakala, picha na kitu kingine chochote kupitia anuani aliyotolewa hapo chini

 

Picha na Video Sauti za Busara 2013

Juu

Angalia  video na picha mambo muhimu ya Sauti za Busara 2013, ujionee kwanini ni tamasha la muziki namba 1 Afrika Mashariki

official video promo documentary film

Official Promo Video

10th Edition Festival Documentary

cheikh lo khaira arby

Cheikh lo (senegal)

Khaira Abry (Mali)

 

Nafasi za kazi za Busara

Juu

Njoo kufanya kazi Busara Promotions
Je wewe ni mchapa kazi, mwenye kuhamasika na shauku ya muziki wa kiafrika? Je una uzoefu wa miaka mitatu katika uongozi wa matamasha, uchangishaji na masoko? Tungependa ufikirie kujiunga nasi. Busara Promotions ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo inaandaa tamasha la kimataifa la muziki lijulikanalo kama Sauti za Busara, linatangaza nafasi mbili za kazi. Kwa maelezo zaidi soma

Meneja masoko na mtafuta Fedha, Busara Promotions

Mkataba wa miaka miwili, kuanzia 1/06/2013. Maombi kwa mataifa yote (miaka mitatu ya uzoefu)
Mwenye majukumu ya kutafuta pesa, masoko, uandishi wa Habari na msanifu wa michoro.
Tuma CV yako na barua kwa md@busara.or.tz kabla ya tarehe 1/5/2013
Kwa maelezo zaidi bofya hapa

Meneja wa Tamasha, Busara Promotions

Mkataba wa miezi minane, kuanzia tarehe 1/07/2013. Maombi kwa mataifa yote (uzoefu wa miaka mitatu)
Mwenye majukumu ya kusimamia tamasha la Sauti za Busara 2014.
Tuma CV yako na barua kwa md@busara.or.tz kabla ya tarehe 15/5/2013
Kwa maelezo zaidi bofya hapa

Busara Promotions inajitahidi kutoa usawa wa kijinsia katika nafasi za ajira kwa wenyeji vyovyote itakavyowezekena. Tafadhali zingatia muombaji atakayefanikiwa ndiye tutakaye wasiliana naye.

crew in the office Lighting setup

Front desk reception of festival venue

Office crew

Lighting setup

 

Muendelezo wa filamu ya Bi Kidude

Juu

DOADOA

Marafiki zetu kutoka kampuni ya Screen Station walikuja tena Zanzibar kwa ajili ya muendelezo wa filamu ya Bi Kidude. Kama hukumuona katika tamasha la mwaka huu, na hukupata nafasi ya kuona filamu kipindi cha Busara Xtra unaweza pata nakala yako ya DVD kupitia tovuti hii http://www.amazon.co.uk/ au http://www.sternsmusic.com/ Timu nzima kwa sasa ipo katika harakati za uandaaji wa muendelezo wa filamu, na kuchunguza hali halisi ya vichwa vya habari vya miezi kadhaa iliyopita.

Tutakufamisha zaidi lakini kama huwezi kusubiri unaweza kutembelea katika kurasa www.facebook.com/screenstation

 

DOADOA East African Performing Arts Market

Juu

DOADOA Toleo la pili la DOADOA- The East African Performing Arts Market- litafanyika kuanzia tarehe 6-11/5/2013 Jinja, Uganda.
Usahili umeshaanza!
DOADOA ilianzishwa kama jukwaa la kimtandao la wataalam na ushirikiano wa kujifunza kwa wadau mbalimbali mashirika na wafanyabiashara ili

kuongeza soko la Muziki na Sanaa ya Afrika Mashariki. Lengo kuu la DOADOA ni kuongeza ufanisi na mtandao kwa njia ya Majadiliano, Semina na masomo, na kutafuta masoko mapya kwa njia ya kutoa majukwaa kwa ajili ya mitandao, maonyesho na matangazo. Toleo la pili la DOADOA litafanyika Jinja nchini Uganda kuanzia tarehe 6 mpaka 11/5/ 2013. Kwa maelezo zaidi na Ratiba tembelea tovuti yetu www.doadoa.org na kwenye kurasa yetu ya facebook

 

Wito kwa wadhamini, wahisani na Rafiki wa Busara

Juu

Tiketi kwa mtanzania ni shilingi 3000. Ili kulisaidia tamasha liweze kuendelea tunategemea misaada kutoka kwa wahisani na wadhamini.
Kuna njia nyingi ambazo kampuni yako inaweza kuonekana kama mfanikishaji wa tamasha. Kama unapendelea kusaidia tamasha, tafadhali tuma ujumbe kwa md@busara.or.tz au busara@busara.or.tz

 

Wasiliana nasi

Juu

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Pia tunapatikana barabara ya airport(uwanja wa ndege), mkabala na club ya Golf Maisara

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Penda kurasa yetu ya facebook

Juu

Kwa kupata picha za karibuni, tembelea kurasa yetu ya facebook na changia ulivyofurahia tamasha. penda ukurasa wetu hapa www.facebook.com/sautizabusara na ifuatilie Sauti za Busara kwenye twitter www.twitter.com/sautizabusara

facebook

Penda ukurasa wetu hapa www.facebook.com/sautizabusara

youtube logo
twitter

Tafadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org