Jarida hili limetumwa kwa watu 64,677

Emeil yako huioni vizuri fungua kwenye brauza

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Wito wa mwisho kwa wasanii SzB 2014
Wito wa wafadhili na wahisani
Wito kwa filamu za muziki wa kiafrika
Maonyesho ya Busara ya Mikoa
Kalenda ya matamasha Zanzibar
Kumbukumbu ya Bi Kidude
Siku ya Kuzaliwa kwa Nelson Mandela
Wasiliana nasi

Wito wa mwisho kwa wasanii SzB 2014 Mwisho wa maombi 31/07

Top

Je wewe ni msanii wa muziki wa kiafrika? Mwisho wa maombi kwa ajili ya tamasha la 11 la Sauti za Busara ni tarehe 31/07 kwa wasanii wote wa ndani na wa kimataifa. Tamasha litakuwa kwa siku nne kuanzia tarehe 13-16 Februari 2014. Fomu ya maombi kwenye tovuti yetu ipo HAPA au unaweza fika ofisini kwetu iliyopo Maisara mkabala na Golf Club.

Vikundi zaidi ya 250 vimeshafanya maonyesho yao katika Tamasha la Sauti za Busara, na vyote vikifanya maonyesho ya moja kwa moja (100% Live).

Zingatia tunapokea maombi mengi kila mwaka na tunaangalia na kusikiliza kila moja kwa umakini. Tafadhali kuwa mstahamilivu kwani jopo la uchaguzi litakaa mwanzoni mwa mwezi wa nane na kuwataarifu wasanii wote waliochaguliwa na wasiochaguliwa.
Maombi yako lazima yawe :

  • Umejaza fomu kwenye tovuti yetu au kwenye fomu ya karatasi, na kuambatanisha maelezo ya kikundi yasiyozidi maneno 1000.

  • Nakala zako mpya 1 au 2 (CD au DVD)

  • Picha 1 au 2 (JPG au za karatasi)

Tafadhali tuma nakala zako, Picha an au nyaraka nyingine zozote kwa anuani ya ofisi yetu hapo chini:


BUSARA PROMOTIONS PO BOX 3635 STONE TOWN, ZANZIBAR, TANZANIA


Tafadhali zingatia hatutapokea maombi baada ya tarehe 31/07. Hakikisha unakamilisha maombi yako yaliyoambatanishwa na nyaraka zako zote muhimu. Kwa maelezo zaidi tembelea www.busaramusic.org/callforartists

Zanzibar vibes Zanzibar vibes

Cheikh Lo (Senegal) at SzB 2013

Sousou & Maher Cissoko (Senegal + Sweden) at SzB 2013

 

Wito wa wafadhili na wahisani

Top

top 25 festival

Sauti za Busara inajulikana kuwa moja ya Tamasha kubwa na muhimu barani Afrika. Kwa miaka mitatu mfululizo limetajwa kuwa moja ya matamasha 25 bora ya kimataifa kwenye jarida la Songlines. Tamasha linajiendesha kwa kutegemea wadhamini na wahisani ambapo tiketi moja huuzwa kwa shilingi 3000 kwa Mtanzania.

Kuna njia nyingi ambazo kampuni au mtu binafsi anaweza kuwa miongoni mwa waliofanikisha tamasha, kwa kutoa shukrani kabla, baada ya kipindi cha tamasha, Ngome Kongwe na sehemu husika iliyofadhiliwa/saidiwa, kwenye TV, Radio, na kwenye vyombo vya habari vyote.

Mwaka 2013 tovuti yetu imetembelewa mara 2,000,000. Kama

unapendelea kuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha, tafadhali wasiliana na Cynthia marketing@busara.or.tz

 

Wito kwa filamu za muziki wa kiafrika

Top

Sauti za Busara inatafuta filamu za muziki aina tofauti ndefu na fupi, Makala ya muziki au Makala ya matamasha.
Tunatafuta filamu zifuatazo:-

  • Ambazo zinazungumzia masuala ya muziki au mwanamuziki

  • Filamu yenye muonekano mzuri, ubora wa sauti, na iliyochukuliwa katika mazingira yenye utamaduni wa kiafrika.

  • Lugha za kigeni lazima zitafsiriwe kwa kingereza/Kiswahili

Maombi yako yatafanyiwa kazi na kamati ya uchaguzi kama umekamilisha maombi yako ikiwemo nakala za DVD mbili kabla ya Tarehe 30 Novemba 2014
Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea kwenye tovuti yetu www.busaramusic.org/callforfilm

 

Maonyesho ya Busara ya Mikoa

Top

Sauti za Busara imeamua kuongeza maonyesho zaidi katika kalenda yake ya mwaka! Maonyesho ya kila mkoa yatafanyika mwezi wa tisa yatakutanisha wasanii mbalimbali kutoka Zanzibar. Tarehe rasmi bado haijapangwa lakini itatangazwa rasmi kwenye tovuti yetu, facebook na twitter. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na journey@busara.or.tz

 

Kalenda ya matamasha Zanzibar

Top

Busara Promotions inapenda kushirikiana na matamasha mengine yanayofanyika Zanzibar. Soma zaidi:

•JAHAZI LITERARY & JAZZ FESTIVAL 2013 – tunapenda kukujulisheni tamasha la Jahazi litafanyika tena kwa mara ya tatu sasa kuanzia tarehe 30/08 mpaka 1/09 2013. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti yao http://www.jahazifestival.com. tamasha la mwaka huu litawaleta Sousou na Maher Cissoko, wasanii waliopata kufanya maonyesho yao katika tamasha la Sauti za Busara mwaka 2011 na 2013, usikose kuwaona ndani ya Jahazi.

ziff

Jahazi Literary and Jazz Festival

•FASHION WEEK ZANZIBAR – tamasha jipya kinakuja visiwani Zanzibar! Fashion Week Zanzibar litafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 25-26 Octoba 2013, Sauti za Busara itashirikiana na Fashion week Zanzibar.

ziff

Fashion Week Zanzibar

 

Kumbukumbu ya Bi Kidude

Top

Ni majonzi yasiyoelezeka kuondokewa na bibi yetu kipenzi ajulikanaye kama Fatma Baraka Khamis kwa umaarufu Bi Kidude tarehe 17/04/2013. Tutamkumbuka daima hasa kutokana na mchango wake katika tasnia ya sanaa na muziki hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Mungu amuweke mahali pema peponi.


Kaa tayari kwa ajili mengi zaidi kutoka Screen Station na Busara Promotions kuhusu sherehe za kumbukumbu ya Bi Kidude zitakazofanyika mwezi wa nne mwakani.


Kwa habari zaid kuhusu Bi Kidude tunapendekeza tembelea hapa:
- Kurasa ya Bi Kidude katika tovuti ya Busara http://www.busaramusic.org.
- Buriani ya Bi Kidude iliyochapishwa kwanye gazeti la Citizen (TZ) na Nation (KE) http://www.nation.co.ke

Zanzibar vibes Zanzibar vibes

Bi Kidude (Zanzibar)

Bi Kidude video

 

Siku ya Kuzaliwa kwa Nelson Mandela

Top

SAIDIA KUSHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA KWA NELSON MANDELA
Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela ambayo atatimiza miaka 95. Tunatumai utaungana na Busara na watu wengine zaidi kumtakia heri na Baraka.

mandela

Nelson Mandela(South Africa)

 

Wasiliana nasi

Top

Last but not least, to all our Muslim brothers and sisters around the world, we take this opportunity to wish you all a peaceful and blessed Holy Month. Ramadan Mubarak!

For more information please visit our http://www.busaramusic.org, LIKE us on www.facebook.com/sautizabusara, and FOLLOW us on https://twitter.com/sautizabusara.

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Find us on the airport road, opposite Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Please forward this mail to friends who may be interested. To subscribe or unsubscribe to our newsletter – just type your email address in the box at
www.busaramusic.org