Jarida hili limetumwa kwa watu 65,578

Emeil yako huioni vizuri, ifungue kwenye brauza

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Wiki tano tu hadi tamasha
Orodha ya wasanii
Ratiba ya tamasha - Pata tiketi yako sasa
Santuri Safari
Movers & Shakers Kutana na wataalamu
Taarifa kwa wageni
Kibali kwa wanahabari
WOMEX the World Music Expo
Pumzika Peponi
Wadhamini na wahisani
Wasiliana nasi

Tamasha la 11 la Sauti za Busara: Wiki tano tu hadi tamasha

Juu

Salamu kutoka Zanzibar ambapo Timu ya Busara imechachamaa katika maandalizi. Zikiwa zimebakia wiki tano tu hadi kufikia tamasha, msisimko unaanza kuhisika katika mitaa ya Mji Mkongwe; hoteli zinajaa na tiketi zinanyakuliwa. Kuongezea katika msisimko wa wasanii watakaotumbuiza ambao wako katika harakati za mwisho za kujiandaa kuja Zanzibar, pia tunatambulisha mpango kabambe wa ki DJ unaoitwa Santuri Safari fuatilia taarifa katika tovuti yetu na maeneo ya mjini.

audiences
audiences
 

Orodha ya wasanii

Juu


Katika jarida (newsletter) letu lililopita tulitangaza idadi kubwa ya wasanii maridadi watakaotumbuiza. Wengine wachache ambao wamethibitisha baada ya tangazo hilo ni:

Ashimba (Tanzania / Finland)   Majestad Negra (Puerto Rico) Street Rat and Body Mind & Soul (Malawi)Moyize (Rwanda)   Ricky na Marafiki (Kenya) Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali (Zanzibar / Turkey / Germany)  Kazimoto (Tanzania / Germany).

Kwa orodha kamili fungua: www.busaramusic.org

Angalia video

   
340ml
Waldemar Bastos
 
Angola / PortugaL
mlimani Park Ochestra
Noumoucounda Cissoko
Senegal
340ml
Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble
South Africa
 

Ratiba ya tamasha - Pata tiketi yako sasa

Juu

THUR, 13 FEB

FRI, 14 FEB

5:00pm 

Baladna Taarab 5:00pm  Ricky na Marafiki

6:10pm 

Pungwa  6:00pm  Abantu Mandingo

7:00pm 

Tritonik 7:00pm  Tarabband

8:10pm 

Joel Sebunjo ft. Lenna Kuurmaa 8:10pm  Hoko Roro

9:10pm 

Jhikoman 9:00pm  Waldemar Bastos

10:15pm 

Seven Survivor 10:00pm  HAJAmadagascar and The Groovy People ft. Werner Puntigam

11:15pm 

Kara Sylla Ka 11:00pm  Noumoucounda Cissoko

12:20am 

Wunmi 12:05am  Kazimoto
    1:00am  Jupiter & Okwess International
SAT, 15 FEB SUN, 16 FEB
5:00pm  Street Rat and BodyMind & Soul 5:00pm  Moyize
5:55pm  Tausi Women's Taarab 6:00pm  Swahili Vibes
7:00pm  The Nile Project 7:00pm  Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali
8:10pm  Swahili Encounters 8:10pm  Addis Acoustic Project ft Melaku Belay
9:05pm  Majestad Negra 9:10pm  Segere Original
10:00pm  Ashimba 10:10pm  Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble
10:55pm  Oy 11:15pm  Sona Jobarteh
11:55pm  Joe Driscoll and Sekou Kouyate  
1:00am  Ebo Taylor  

Kwa Ratiba kamili fungua hapa

Zaidi ya wasanii 200 watakaopiga muziki wa moja kwa moja (live) muziki wa Kiafrika chini ya anga la Afrika, uhitaji kuchelewa pata tiketi yako sasa kwa punguzo maalum la asilimia 10 mpaka mwiki wa mwezi januari.

Kama upo Zanzibar, unaweza kupata fursa hii vile vile kwa kupata tiketi yako sehemu mbalimbali kama Mercury’s Restaurant, Zanzibar Curio Shop, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, Memories of Zanzibar na Kaya Shop and Tea room. Huna sababu ya kuchelewa wahi tiketi yako sasa.

Wekesha tiketi yako mtandaoni kwa kutumia njia mbalimbali zifuatazo.

multiple method banner

Tiketi na pasi zitapatikana kila siku Ngome Kongwe kuanzia siku ya jumatano saa 4:00 asubuhi. Angalia beu hapa : http://busaramusic.org/festivals/tickets/

 

Santuri Safari

Juu

Mwaka huu Busara Promotions inawaletea program mpya ya ubunifu wa kazi za MaDj katika kupiga muziki wa Afrika Mashariki.
Sauti za Busara 2014 inawakutanisha Madj, waandaaji wa muziki na wataalam mbalimbali wa tasnia ya muziki katika kuanzisha mfumo mpya wa upigaji wa muziki wa Afrika Mashariki. Kufurahia na kuutangaza muingiliano wa muziki wa Afrika Mashariki, Santuri Safar inawaletea fursa mbalimbali za uhalisia wa upigaji wa muziki kutoka kwa Madj wa Afrika na kwingineko.

 

Zaidi tunawaalika baadhi ya wataalamu wa tasnia ya muziki kwa kubuni mbinu za kuiwezesha tasnia ya muziki pamoja na waandaaji mbalimbali kwa ajili ya kushiriki pogamm hiyo. Watakaokuja kwenye tamasha watapata fursa ya kuangalia matunda yatokanayo na program hiyo kwenye ratiba za kila jioni zitakazofanyika sehemu mbalimbali Mji Mkongwe (vile vile kurushwa moja kwa moja mtandaoni) na kuhusu pati yetu baada ya ratiba ya siku ya tamasha kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea. website
 

Movers & Shakers Kutana na wataalamu

Juu

Wewe ni mwanamuziki, meneja, mdau wa muziki, muaandaaji wa tamasha, mwandishi wa habari au mwanafani yoyote ya muziki? Movers & Shakers ni nafasi yako!

Sauti za Busara inawavutia wataalamu wa muziki kutoka maeneo ya karibu na mbali. Movers & Shakres inatoa nafasi ya wao kujumuika pamoja kuzungumza,  kubadilishana mawazo na taarifa. Ni kila siku mchana wakati wote wa tamasha (kwa mwaka huu itaanza saa 8-10 jioni, mahali patatangazwa baadae) ni fursa adhimu kwa wasanii, mamneneja, waandishi wa habari na wataalam wanaolingana na fani hizo.

Vipindi vyote ni bure na itakuwa kwa waalikwa binafsi. Wakati wa tamasha la 11 tutazungumzia ni vipi wataalam wa masuala ya utamaduni wanaweza changia katika suala la mazingira endelevu, utafutaji wa fedha na mikakati ya sanaa, uhuru wa kujieleza, na mengineyo. Tafadhali tujulishe kama una ushauri kuhusiana na mada ambayo ungependa kuiona kwa mwaka huu.

Ni kwa waalikwa tu: Kama ni mtaalamu na ungependa kushiriki tafadhali wasiliana na haji@busara.or.tz

 

Taarifa kwa wageni

Juu

audiences

Tunawajali wageni wanaofika kwa tamasha kutoka maeneo yote ya sayari; Hapa utapata taarifa zote utakazohitaji kujua wakati unapanga safari yako http://busaramusic.org/festivals/travel/
Kutakuwa na maeneo yanayouza nguo, chakula, na vitu mbalimbali vya tamasha. Kutakuwa na maeneo 3 ya kuzalisha upya takataka. Tafadhali tusaidia kwa kutupa taka taka zote humo. Taasisi ya Sustainable East Africa, imekuwa

ikishirikiana na  Sauti za Busara kuhakikisha usafi, tamasha la kijani, na pia kutakuwa na banda ambapo utawaona bidhaa zilizozalishwa upya vikiwemo vya mapambo ya mwili.
 

Kibali kwa wanahabari

Juu

Mwito wa mwisho wa vibali vya waandishi wa habar!! Kama unataka kuripoti tamasha la Sauti za Busara 2014, tumeongeza muda wa mwisho mpaka tarehe 17 Januari na tunahitaji kupata maombi yako. Watakaokuwa na vibali vya uandishi wa habari wataruhusiwa kufika kwenye mikutano ya waandishi wa habari, ofisi wa habari iliyopo Ngome kongwe na kwenye mikutano ya wasanii na waandaaji wa matamasha (Movers and Shakers). Soma zaidi na fanya maombi hapa here

audiences
audiences
 

WOMEX the World Music Expo

Juu

WOMEX “ni fursa muhimu ya masoko ya kimataifa katika Nyanja za muziki wa aina mbalimbali. Maonyesho haya huwakutanisha wataalam kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Huchangia kukuza mitandao na kutangaza muziki wa aina mbalimbali dunia nzima .

 
WOMEX ya 19 iliyofanyika Cardiff, UK, Wales, mwezi wa kumi 2013 ilikutanisha wajumbe zaidi ya 2,250 kutoka nchi zaidi ya 90, maonyesho 590, mikutano mbalimbali na maonyesho 60 na jukwaa . kwa maelezo zaid tembelea: www.womex.com

 

Pumzika Peponi

Juu

Tunaungana na dunia nzima katika kipindi hiki kigumu ambacho dunia ilipotelewa na mzee Nelson Rolihlahla Mandela ambaye aliishi kwa ukarimu na kusamehe ambayo tunaendelea kujifunza kutoka kwake.

Nelson Rolihlahla Mandela

18 July 1918 – 5 December 2013

 

 

Wadhamini na wahisani

Juu

Waandaaji wa tamasha wanayofuraha kuwashukuru wachangiaji na wadhamini, bila ya wao Sauti za Busara halitaweza kufanyika.

Norwegian Embassy   Hivos
 
  Goethe Institut   Embassy of US   Goethe Institut     Ultimate Security   Memories of Zanzibar
  Zanzibar Unique   Zanlink   Azam Marine     Alminar   e
                       
          Media Partners        
 
   

Shukrani kwa Embassy of France, SMOLE II, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, Mercury’s, AllyKeys Car Hire, fROOTS, Southern Sun Hotel, Embassy of Germany, www.zanzibar.net

 

Wasiliana na nasi

Juu

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana Mkabala na Golf Club, Njia inayoelekea Uwanja wa Ndege

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

facebook

penda ukurasa wetu wa www.facebook.com/sautizabusara

youtube logo
twitter

Angalia vitu vya ziada kwenye tovuti yetu Music Charts, Top African Music Festivals, East African Arts Events Calendar, photo galleries na video clips


afadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org