Jarida hili limetumwa kwa watu 65,578

Emeil yako huioni vizuri, ifungue kwenye brauza

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Sauti za Busara 2014
Picha
Vyombo vya Habari
Tarehe ya Sauti za Busara 2015
Wito wa wasanii 2015
Wito wa Filamu 2015
Buriani Bi Kidude: Mwaka mmoja
Shukrani kwa wadhamini na wahisani

Soma jarida hili: Français / English

Sauti za Busara 2014

Juu

Jua linazama na mikiki mikiki ya tamasha la Sauti za Busara! Kwa siku nne mfululizo kuanzia tarehe 13 – 16 February zenye mchanganyiko wa ngoma mbalimbali kutoka vikundi takribani 32. Ngome Kongwe ilipambwa na wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani, muziki wa asili wenye vionjo vya kisasa. Ala za muziki ijulikanayo kama Kora ni maarufu sana Afrika ya Magharibi, ilipigwa na msanii kutoka Senegal – Noumoucounda Cissoko, na mwanadada adimu kabisa duniani katika upigaji wa Kora maarufu Sona Jobarteh kutoka Gambia, na wa mwisho alikuwa Joel Sebunjo kutoka Uganda msanii pekee wa Afrika Mashariki aliyejipatia umaarufu wa upigaji Kora.

Audiences
Audiences

Tamasha lilionyesha filamu ndefu nne za muziki wa kiafrika kama Jupiter’s Dance, HomeGrown: HipLife in Ghana, Mama Goema: The Cape Town Beat in Five Movements, na As Old as My Tongue, filamu ya Bi Kidude. Filamu zilionyesha taswira za utajiri na hazina ya muziki wa kiafrika na kuleta mabadiliko chanya ya muziki katika jamii.

SHUKRANI kwa watu wote waliotoka sehemu mbalimbali duniani waliojumuika nasi Zanzibar kwa ajili ya kupata radha tofauti za muziki wa kiafrika, katika kipindi chote cha mvua na jua. Tunatumai mtakuwa nasi tena 2015!

Busara inatoa shukrani zake kwa wafanyakazi wote kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha ratiba ya muziki inafana kikamilifu. Na shukrani za pekee ziende kwa wasanii wote:

Jupiter & Okwess International (DRC)  Ebo Taylor (Ghana / Germany)  Joe Driscoll and Sekou Kouyate (USA / Guinea)  Waldemar Bastos (Angola / Portugal)  Sona Jobarteh (Gambia / UK)  The Nile Project (Nile Basin)  Noumoucounda Cissoko (Senegal)  Wunmi (Nigeria / UK / USA)  Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble (South Africa)  Addis Acoustic Project ft Melaku Belay (Ethiopia)  OY (Ghana / Switzerland)  Tausi Women's Taarab (Zanzibar)  Seven Survivor (Tanzania)  Street Rat and Body Mind & Soul (Malawi)  Tarabband (Egypt / Sweden / Iraq)  Baladna Taarab (Zanzibar)  Majestad Negra (Puerto Rico)  HAJAmadagascar and The Groovy People ft. Werner Puntigam (Madagascar / France / Austria)  Jhikoman (Tanzania)  Hoko Roro (Tanzania)  Ashimba (Tanzania / Finland)  Swahili Vibes (Zanzibar)  Tritonik (Mauritius)  Kara Sylla Ka (Senegal / Switzerland)  Joel Sebunjo (Uganda)  Abantu Mandingo (Tanzania)  Segere Original (Tanzania)  Moyize (Rwanda)  Ricky na Marafiki (Kenya)  Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali (Zanzibar / Turkey / Germany)  Kazimoto (Tanzania / Germany)  Swahili Encounters Group (Zanzibar / Tanzania / Various)  Pungwa (Zanzibar / Tanzania) 
 

Picha

Juu

Angalia picha za tamasha la mwaka 2014 hapa
Ebo Tailor

Ebo Taylor (Ghana/Germany)

Noumoucounda Cissoko (Senegal)

Wunmi (Nigeria/UK/USA)

The Nile Project(Nile Basin)

Jhikoman (Tanzania)

Tarabband (Egypt/Sweden/Iraq)

The Nile Project(Nile Basin)

Majestad Negra(Puerto Rico)

Jupiter & Okwess International (DRC)

 

Vyombo vya Habari

Juu

Kipindi cha Sauti za Busara kulikuwa na waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali duniani. Unaweza kutembelea Media Coverage kwa taarifa mbalimbali.

Khaira Arby

7 African music festivals you really have to see
http://edition.cnn.com
By Lorraine Bgoya and Mazuba Kapambwe, CNN Inside Africa
February 21, 2014
(CNN) -- One of the most exciting things about the African... read more

   
Khaira Arby

It was Sauti za Busara without Bi Kidude
http://www.thecitizen.co.tz
February 21, 2014
It was a weekend of love with Valentine's Day coming in handy, but just across the ocean in the Spice Islands ... read more

   
Khaira Arby

Retaining local sounds only way to success for some
www.dailynews.co.tz
March 06, 2014
JUST to make sure that there is a selection of local musical flavour around Hassan Mahenge, a teacher at the Dhow ... read more

 
Khaira Arby

De Berlin a Zanzibar pasando por el Nilo
http://cultura.elpais.com
Que la música (igual que la palabra) va por delante perfilando un mundo sin fronteras ha quedado claro en el festival Sauti za Busara (“sonidos del conocimiento” en suajili) de Zanzíbar ...read more

   
Khaira Arby

Sauti Za Busara festival // Zanzibar // DJ & Workshop Announcement
http://www.gillespetersonworldwide.com/
February 26, 2014
Stone Town, Zanzibar - The Santuri Project, a three-year plan to revitalize the music industry in East ... read more

 

Tarehe ya Sauti za Busara 2015

Juu

Sauti za Busara 2015

Tunapenda kuwajulisha kwamba tamasha la 12 la Sauti za Busara litafanyika kuanzia tarehe 12 – 15 Februari 2015. Kama kawaida litawaletea wanamuziki mahiri kutoka Afrika na kwingineko. Jipange sasa kuwa nasi Zanzibar na kusheherekea muziki wa kiafrika chini ya anga la Afrika kwenye ukumbi wa kihistoria. Kwa habari zaidi mpya tembelea tovuti.

 

Wito wa wasanii 2015

Juu

Wito wa wasanii 2015 – mwisho wa maombi tarehe 31 july 2014
Je muziki wako ni wa moja kwa moja asilimia mia (100% live)?
Je muziki wako ni wa Afrika?
Je unahitaji kufanya onyesho Zanzibar?

Maombi yamesha anza kupokelewa kwa ajili ya tamasha la 12 la Sauti za Busara. Hii ni fursa pekee ya kufanya maombi ili upate nafasi ya kushiriki tamasha la mwaka 2015. Kwa kawaida tuna angazia kukuletea muziki wa Afrika chini ya anga la Afrika, kwa sasa Sauti za Busara inakaribisha maombi kutoka nchi za kiarabu ikiwemo Oman, Yemen, Iran na ukanda wa bahari ya Hindi.

Wasanii wote wanatakiwa kujaza fomu ya maombi kwenye mtandao kutuma nakala kabla ya tarehe 31 July 2014. Jopo la uchaguzi litakutana mwezi wa nane na waombaji wote watataarifiwa mwezi wa tisa.

Tafadhali zingatia tunapokea maombi mengi kila mwaka – ili maombi yako yashughulikiwe hakikisha unakamilisha mahitaji yote.

Miaka 11 iliyopita, zaidi ya vikundi 380 vimeshafanya maonyesho yake, miongoni mwao ni Ebo Taylor, Jupiter and Okwess International, Wunmi, Sona Jobarteh, Joe Driscoll & Sekou Kouyate, OY, Cheikh Lo, Mokoomba, Samba Mapangala & Orchestra Virunga, Nneka, Natacha Atlas, Jagwa Music, Fredy Massamba, Thandiswa, Culture Musical Club na zaidi. Tamasha linafanya muziki wa moja kwa moja na sio wa kutumia Cd.

 

Wito wa Filamu 2015

Juu

Wito wa filamu 2015- mwisho tarehe 30 Novemba 2014

Sauti za Busara inatafuta filamu za muziki, fupi au ndefu, makala au matamasha yaliyorekodiwa Afrika.

  • Filamu zinazoelezea historia ya muziki au wanamuziki wa Afrika
  • Filamu zenye kiwango kizuri cha sauti na muonekano na ziwe zimerekodiwa katika mazingira ya Afrika.
  • Lugha za kigeni lazima zitafsiriwe kwa kiingereza au kiswahili

Maombi yako yatatiliwa mkazo iwapo utakamilisha mahitaji yote ikiwemo nakala za DVD mbili kabla yatarehe 30 Novemba 2014.
Kwa maelezo zaidi kuhusu maombi na fomu tembelea www.busaramusic.org/callforfilm

 

Buriani Bi Kidude: Mwaka mmoja

Juu

Buriani Bi Kidude: Mwaka mmoja

Bi Kidude

Bi kidude alikuwa kipenzi cha Sauti za Busara, ni msanii pekee aliyefanya maonyesho mara nane katika tamasha la Sauti za Busara. Huu ndio ulikuwa mwaka wa kwanza kukosa tamasha tangu umauti umfike, na kwa hakika watu wengi walimkosa na kumkumbuka sana. Bodi ya udhamini ya Busara Promotions ilipanda

jukwaani kwa ajili ya kutoa heshima zake pamoja na Tausi Women Taarab kikundi ambacho alikuwa anafanya nacho maonyesho enzi za uhai wake. Mwandishi, Mtunzi na Mjumbe wa Bodi ya Busara Promotions alitoa ushairi kwa ajili ya kumkumbuka na kumpa heshima yake. Baada ya shoo ya Tausi Women’s Taarab kipande kifupi cha filamu ya muendelezo ya Bi kidude (As Old as My Tongue) kilionyeshwa.

Miaka ya 1980 Bi Kidude alianza kufanya maonyesho ya kimataifa. Alifanya maonyesho mbali mbali katika nchi za Afrika, Ulaya na Asia, akitumia sauti yake vizuri na kukonga nyoyo za mashabiki wake. Mwaka 2005 alipata tuzo ya WOMEX (World Music Expo).

Wakati huo huo nyumbani kwake alikuwa anachukuliwa kama muhuni. Alikuwa mvutaji wa sigara na nadra sana kumuona amevaa viatu, pamoja na yote hayo alikuwa ni mtu wa watu ambapo muda mwingi alipenda kuutumia na majirani zake kufurahi.

Andy Jones, Mkurugenzi wa makala ya filamu ya Bi Kidude ijulikanayo kama, "As Old As My Tongue", anasema “Sehemu nyingi duniani watu huchukulia na huamini kwamba mzee ni mtu tegemezi na hana lolote, lakini Bi Kidude ametufunza kupingana na dhana hiyo. Natumai hii itabaki kuwa kumbukumbu tosha kwenye vichwa vya watu jinsi Bi Kidude alivyokuwa anajali utu kuliko kitu (Pesa). Mtu ambaye Maisha yake aliyatumia kwenye uimbaji. Lengo letu lilikuwa kutengeneza filamu ambayo itasheherekewa na kila mtu, na kil a mtu kumkumbuka Bi Kidude kwa ukarimu na umahiri wake”.

Mungu amuweke mahali pema peponi.

 

Shukrani kwa wadhamini na wahisani

Juu

Shukrani kwa Wadhamini na Wahisani:

Norwegian Embassy   Hivos
 
  Goethe Institut   Embassy of US   Goethe Institut     Memories of Zanzibar    
  Zanzibar Unique   Azam Marine   Blue Bay Hotel   Alminar   Chavda Hotel   Mashariki Palace
          Zanzibar Hotel   Allience Francais        
                       
         

Vyombo vya habari wenza

       
 
   

Shukrani kwa Embassy of France, SMOLE II, Ultimate Security, Zanlink, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, Mercury's Restaurant, Emerson Spice, AllyKeys Car Hire, fROOTS, Southern Sun Hotel, Embassy of Germany, www.zanzibar.net

 

Wasiliana nasi

Juu

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana Mkabala na Golf Club, Njia inayoelekea Uwanja wa Ndege

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

facebook

Penda ukurasa wetu wawww.facebook.com/sautizabusara

afadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org