Jarida hili limetumwa kwa watu 68,000+

Emeil yako huioni vizuri fungua kwenye brauza

Soma Jarida hili kwa: Français / English

Usijibu barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz

busara newsletter
Wito wa Mwisho kwa Wasanii
Wito wa Filamu zinazohusu Muziki
Wito kwa Washiriki katika Udhamini
Nafasi ya Kazi: Finance & Admin Manager
Matamasha mengine: ZIFF 2014
Pumzika kwa Amani Babu Emerson.
Mfuko wa Kumbukumbu wa Bi. Kidude
Penda ukurasa wa Sauti za Busara facebook

 

Sauti za Busara ni moja kati ya matamasha yaliyo juu Afrika, linalofanyika Februari ndani ya Mji Mkongwe, Zanzibar. Linaandaliwa na Busara Promotions, taasisi isiyo ya kiserikali.

Sauti za Busara imejipatia umaarufu sana kwa mashabiki wa ndani ya nchi pamoja na kuvutia wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Katika miaka 11 dhumuni letu limekua kuonesha muziki mbalimbali na maridadi kutoka bara la Afrika na Waafrika wanaoishi nje. Kuanzia mwaka 2015, programu itahusisha pia muziki kutoka ulimwengu wa Uarabuni pamoja na Bahari ya Hindi.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Sauti za Busara ikiwemo picha tofauti, video za matukio muhimu, uenezo wa vyombo vya habari na ziada, tazama www.busaramusic.org

Video za Matukio Muhimu katika Tamasha

 
Audiences

Sauti za Busara 2012 (25')

Audiences

Sauti za Busara 2012 (2'36")

Audiences

Sauti za Busara 2011 (15')

 

Wito wa Mwisho kwa Wasanii

Juu

Call for Artists

Call for Artists 2015

Zanzibar vibes

Safi Theatre Group (Tanzania) at Sauti za Busara 2013

Kwa wasanii wa tamasha, tamasha litalipa ada ya onyesho pamoja na gharama zingine ukiwa Zanzibar, ikiwemo malazi, usafiri, visa na pesa ya chakula. Wasanii kutoka nje ya nchi wanaweza kuhitajika kujitafutia wadhamini wao binafsi wa kuwasafirisha.

Tunapochagua wasanii, tunatoa kipaumbele kwa:

 • Muziki wa Afrika Mashariki
 • Muziki wa Bara la Afrika na Waafrika wanaoishi nje ya nchi, Ulimwengu wa Uarabuni na Bahari ya Hindi
 • Ubora wa kazi za Kisanii
 • Uwiano wa Kijinsia
 • Sauti za Busara (mfano. Muziki wenye ujumbe)
 • Uhalisi, ubunifu na uvumbuzi
 • Vipaji vipya na vichanga
 • Muziki wenye ladha mbali mbali (“wa asili” na umeme, wa vijijini na mjini)
 • Wasanii wasiopata muonekano wa kutosha na waliotengwa
 • Wasanii wenye majina ili kuvutia wahudhuriaji wengi zaidi.

Tarehe ya mwisho ya kupokea Fomu ya maombi ni 31st Julai 2014

 

Wito wa Filamu zinazohusu Muziki

Juu

Sauti za Busara inatafuta aina tofauti za filamu ndefu na fupi zenye ubora kutoka barani Afrika na Waafrika wanaoishi nje, ulimwengu wa Uarabuni pamoja na Bahari ya Hindi. Hizi zinaweza kuwa vipande vya muziki,dokumentari au matamasha yaliyorekodiwa.

Filamu zenye lugha ngeni zinatakiwa kuwa na tafsiri (subtitle) katika Kiingereza au Kiswahili. Filamu yako itazingatiwa tu kama itapokelewa na fomu iliyojazwa, kikamilifu ikiwa pamoja na kopi 2 za DVD za filamu hiyo kabla ya tarehe 30th Novemba 2014.
 

Wito kwa Washiriki katika Udhamini

Juu

Tamasha linatoa package karimu yenye manufaa ya kimasoko kwa wote wanaotusaidia. Ili kuomba kutumiwa Package ya Tamasha mwaka 2015, tafadhali tuma barua pepe kwenda busara@busara.or.tz

Audience

Festival Audiences

Audiences

Festival Audiences

 

Nafasi ya Kazi: Finance & Admin Manager

Juu

Tunatarajia kuajiri Finance and Administration Manager ambaye ni mtaalam na mchapakazi ili kusaidia katika kutekeleza ’ Mpango wa Mkakati, 2014 – 2019 wa Busara Promotions.

 • Je una uzoefu juu ya miaka 3 katika Uandaaji, Usimamizi wa Rasilimali Watu na fedha?
 • Utaweza kuishi na kufanya kazi Zanzibar kwa muda usiopungua miaka miwili?
 • Una ufahamu kamili kuhusu kompyuta? (Word, Excel, Adobe, internet)
 • Ufasaha kamili katika lugha ya kiingereza? (Mazungumzo na Maandishi)
 • Uwezo wa kuwasiliana kwa Kiswahili?
 • Makini, mwenye ari, unayejiamini kufanya kazi mwenyewe na kuongoza kama sehemu ya timu?

Ili kuomba nafasi hii, tafadhali tuma CV yako kwenda busara@busara.or.tz pamoja na barua ya maombi, inayoonesha uwezo utakaoleta Busara Promotions, itufikie ofisini kabla ya tarehe 19 Juni 2014.

 

Matamasha mengine: ZIFF 2014

Juu

Tamasha la 17 la Zanzibar International Film Festival linaahidi uchaguzi bomba wa filamu, maonyesho, warsha na mengineyo. Litafanyika Mji Mkongwe Zanzibar kuanzia tarehe 12 – 22 Juni 2014, unaweza kuangalia programu hapa http://www.ziff.or.tz/program-2014/

 

Pumzika kwa Amani Babu Emerson.

Top

Audience

Emerson D Skeens

Emerson D. Skeen ni miongoni mwa waanzilishi wa tamasha la kimataifa la filamu (Ziff), Chuo cha Muziki Zanzibar (DCMA), Busara Promotions pamoja na mipango kadhaa ya utunzaji wa urithi wa Zanzibar, alifariki tarehe 31 May 2014 baada ya kuugua kipindi kirefu na maradhi ya kansa. Ukarimu na ucheshi wake utakosekana sana kwa Wazanzibar na na watu kutoka nje. Babu Emerson kazi yako inaonekana hapa na historia na urithi wako utazidi kuendelea. Pumzika kwa Amani.

 

Mfuko wa Kumbukumbu wa Bi. Kidude

Juu

Baada ya mikutano mingi na maongezi na ndugu wa familia ya Fatma Baraka Khamis, anayefahamika kimataifa kama Bi Kidude (Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi), tunafurahi kuwaarifu juu ya mradi wenye lengo la kuheshimu kumbukumbu ya gwiji huyu wa Muziki Zanzibar.

Audience
 • Nyumba ya Bi Kidude itakarabatiwa na kuwa Makumbusho ya Bi Kidude, ikiwa na picha, vipande vya filamu, rekodi za muziki, ala, taarifa, nguo pamoja na kazi nyingine za sanaa
 • Sehemu ya mapato yatakayokusanywa kutokana na malipo ya tiketi, pamoja na manufaa mengine yatakayopatikana kutokana na mauzo na matangazo ya rekodi zake yatarudi katika Mradi wa Makumbusho wa Bi Kidude na kusaidia wanawake na wasichana katika tasnia ya muziki.
 • Kamati itakayohusisha ndugu wa familia na marafiki wa Kidude utasimamia mfuko huu
 • Kwa taarifa zaidia fuatilia kurasa yetu ya facebook.
 

Penda ukurasa wa Sauti za Busara facebook

Juu

Audience   Audience

Tu LIKE kwenye facebook www.facebook.com/sautizabusara

 

Tu FOLLOW kwenye twitter: https://twitter.com/sautizabusara

 

 

Ramadan Karim!

Juu

Mwisho kabisa, kwa kaka na dada zetu wa Kiislam duniani kote, tunawatakia Mwezi Mtukufu wenye amani na Baraka. Ramadhan Karim!

Call for Artists

Sunset Session at Sauti za Busara 2014

Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar)

 
Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana Mkabala na Golf Club, Njia inayoelekea Uwanja wa Ndege

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Tafadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org