Jarida hili limetumwa kwa watu 68,262

Fungua jarida kwenye browser

Usijibu kwa kutumia anuani hii. Kuwasiliana nasi tafadhali tumia barua pepe hii busara@busara.or.tz

Sauti za Busara Newsletter

Soma jarida kwa: English / Français

 

Fungua jarida kwenye browser

Festival Poster

Sauti za Busara:
ni moja kati ya matamasha bora yanayopendwa Afrika”.

DJ Rita Ray, BBC.

Blitz the ambassador audience

Kuanzia tarehe 12 –15 Februari 2015, Sauti za Busara iliwaleta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali duniani kusheherekea utajiri wa muziki wa Afrika. Ukumbi wa tamasha ujulikanao kama Ngome Kongwe ulijawa na watu kwa siku zote nne za tamasha.

Dhima ya tamasha hili la 12 ilikuwa ni  “Together as One, Amani Ndio Mpango Mzima!
Ujumbe ulipokelewa ipasavyo; Amani na Umoja, Afrika yenye mtazamo Chanya!

festival parade
Festival parade

Siku ya ufunguzi, mitaa ya Mji Mkongwe ilipambwa na umati wa watu waliojumuika katika matembezi ya tamasha. Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika siku hizo nne za tamasha ni Blitz the Ambassador (Ghana/USA), Djmawi Africa (Algeria), Liza Kamikazi and band (Rwanda), Sarabi (Kenya), The Brother Moves On and Ihhashi Elimhlophe (South Africa), Tcheka (Cape Verde), Mim Suleiman (Zanzibar/UK), Tsiliva and Mpamanga (Madagascar), Thaïs Diarra ft. Noumoucounda Cissoko (Switzerland/Senegal/Mali), Aline Frazão (Angola), Octopizzo and band (Kenya), Isabel Novella(Mozambique), Alikiba , Msafiri Zawose , Leo Mkanyia, Tunaweza Band , Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta , Rico Single & Swahili Vibes andCocodo African Music (Tanzania).

Blitz the ambassador
BLITZ THE AMBASSADOR (GHANA/USA)
Sarabi
SARABI (KENYA)
Djmawi Africa
DJMAWI AFRICA (ALGERIA)
Liza Kamikazi
LIZA KAMIKAZI (RWANDA)
The Brothers Moves On
THE BROTHER MOVES ON (SOUTH AFRICA)
Ihhashi Elimhlope
IHHASHI ELIMHLOPE (SOUTH AFRICA)
Mim Suleiman
MIM SULEIMAN (ZANZIBAR/UK)
Tcheka
TCHEKA (CAPE VERDE)
Tsiliva
TSILIVA (MADAGASCAR)
Thais Diara
THAÏS DIARRA (SENEGAL /MALI/ SWITZERLAND)
Aline Frazao
ALINE FRAZAO (ANGOLA)
Isabel Novella
ISABEL NOVELLA (MOZAMBIQUE)
Octopizzo
OCTOPIZZO (KENYA)
Msafiri Zawose
MSAFIRI ZAWOSE (TANZANIA)
Alikiba
ALIKIBA (TANZANIA)
Cocodo African Music
COCODO A MUSIC (TANZANIA)

Upande wa Amphitheatre haukuwa nyuma nao ulijawa na watu kwa siku zote nne ambapo wenyeji na wageni walipokuwa wanafurahia ratiba ya filamu za muziki wa kiafrika, ikiwemo The Last Song before the War, Maramaso, 100% Dakar na ujio mpya wa filamu ya Bi Kidude iliyoandaliwa na Andy Jones’ I Shot Bi Kidude’.

Wakati huo huo wataalamu wa tasnia ya muziki wakiwemo mameneja, waandishi wa habari, waandaaji wa muziki na wasanii wenyewe walijumuika pamoja katika mkutano ujulikanao kama Movers & Shakerskwa ajili ya kujadiliana mbinu za kuusukuma mbele muziki wa kiafrika ulimwenguni.

Vikundi 15 vilishiriki kwenye shindano la utunzi wa nyimbo za Amani Songs for PeaceKama ilivyoelezewa na kiongozi wa jopo la Majaji bwana Tabu Osusa; ‘‘Shindano la nyimbo za Amani lilikuwa ni wazo zuri. Nimeshangazwa na utajiri wa muziki wa Tanzania kutoka kwa washiriki wa shindano hilo.’’

Washindi wa shindano hilo kama ifuatavyo:-

Culture Musical Club (Zanzibar) - na nyimbo yao Amani Tanzania.
Tunaweza Band (Tanzania) -na nyimbo yao Amani.
Rico Single (Zanzibar) - na nyimbo yao Amani Ndio Furaha Yetu.
Leo Mkanyia (Tanzania) –alitambulika kwa onyesho la kipekee na nyimbo yake Linda Amani.

Zawadi ya pesa taslim 10,000,000/- TSh ilitolewa kwa washidi wote wanne, kwa ajili ya kugharamia malipo ya studio kwa utengenezaji wa nyimbo zilizoshinda.

Songs for peace

Together as One; Amani Ndio Mpango Mzima!

Tamasha linatoa shukrani za dhati kwa wasanii wote, wafanyakazi, wahisani na wadhamini, waandishi wa habari na mashabiki wote, ambao walifanikisha tamasha la 12 la Sauti za Busara kufanyika kwa mafanikio zaidi.

Sauti za Busara 2015 inapenda kutoa shukrani za dhati kwa  :

MAIN DONORS

Norwegian EmbassyHivos

SPONSORS

Zanlink Maru Maru Hotel Zanzibar ASK Barzangy

DONORS & PARTNERS

US EmbassyCEFA TZGermany Embassy Dar es salaam SDC womex ACRACCS African Synergy Logo Oslo world music festival DCMA AMDP

MEDIA PARTNERS

Times FM
fROOTS
Music in Africa
 
Chuchu FM
HITS FM
 

... na shukrani ziende kwa:

www.zanzibar.net, Southern Sun DSM, Zanzibar Grand Palace Hotel, Alliance Française de Dar, Chuchu FM Radio, SMOLE II, Monsoon Restaurant, Mercury's Restaurant, Archipelago Restaurant, Doctor Mehta, Embassy of Germany, Embassy of France, Association Franco Zanzibarite (AFZ), Stone Town Café and Marafiki wa busara

facebook like button

Contact us

Wasiliana nasi
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Njia iendayo uwanja wa ndege

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Tafadhali peleka/sambaza jarida hili kwa watu ambao watavutiwa. Ili ku kujiunga au kujitoa katika jarida hili, andika tu email yako ndani ya boksi katika www.busaramusic.org