Jarida hili limetumwa kwa watu 68,055

Lifungue jarida kwenye browza

Usijibu kwa kutumia barua pepe hii. Kwa mawasiliano nasi tumia busara@busara.or.tz

Sauti za Busara Newsletter

Soma jarida kwa English / Français

 

Lifungue jarida kwenye browza

Wito Kwa Wadhamini
Wasiliana nasi
Wito Kwa Wasanii

Sauti za Busara imeingizwa kwenye listi ya CNN ya matamasha 7 bora Afrika 7 African music festivals you really have to see, vilevile limeteuliwa kuwa miongoni mwa matamasha 25 bora ya kimataifa kwenye  Jarida la Songlines  Best 25 International Festivals na kwenye  Afro Tourism kama miongoni mwa matamasha nane bora 8 Best Music Festivals. Mwezi Februari 2015, BBC World Service ilizungumzia Sauti za Busara kama miongoni mwa tamasha bora la muziki one of Africa's best and most respected music events’.

Play video highlights

Sauti za Busara 2015: Together as One (2’12”)

Kila mwaka mwezi Februari, Sauti za Busara huwaletea muziki wa Afrika unaopigwa moja kwa moja. Mji Mkongwe huwa na pilika pilika za hapa na pale. Watu 5,000 huudhuria tamasha kila siku, au watu 20,000 kwa situ zote nne. Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali hujumuika pamoja, miongoni mwao asilimia 70 kutoka Afrika Mashariki, wageni  Nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya, Mashariki ya Kati, Amerika ya Kaskazini, Australia na Japan. Sauti za Busara huchangia ukuwaji wa uchumi wa Nchi, wakati inatoa ajira na mafunzo kwa vijana na kusaidia idara ya utamaduni.

Kiingilio ni bure kabla ya saa kumi na moja na baada ya hapo ni shilingi elfu 3,000/- za Tanzania na Dola 25 kwa wageni wa kimataifa.

Angalia Taarifa za habari, picha na video.

Festival audience Festival Audiences

Night audiences at SzB 2015 [photo Link Reuben]

Djmawi Africa (Algeria) audience at SzB 2015 [photo Peter Bennett]

Wito Kwa Wadhamini

Tarehe ya tamasha itatangazwa punde tu tutakapopokea udhamini.
Sauti za Busara inakusudia kuimarika kutokana na udhamini kutoka kwa wahisani wa kimataifa kwa asilimia 35 wafanyabiashara 40 na mapato ya ndani 25. Hata hivyo licha ya kufanya tamasha kwa mafanikio lakini upatikanaji wa wadhamini kwa ajili ya tamasha ni changamoto kubwa kila mwaka.

Wageni waingiao Zanzibar wameongezeka kwa asilimia 500% tangu Sauti za Busara ilipoanza. Hoteli zinajaa na wanafanyabiashara ndogondogo wanafurahi. Tunaamini wakati sasa umefika kwa wafanyabiashara mbalimbali kama Hoteli, Kampuni za Ndege, Simu,  Bank na wadau wengine ambao wanafanya kazi zao Zanzibar kusaidia tamasha ili liweze kuendelea zaidi.

Wasiliana nasi kama upo tayari kusaidia Sauti za Busara. Tutatangaza na kufanyakazi katika mazingira ya faida kwa pande zote mbili. Matangazo yanaanza mara moja kwa wadhamini wote pindi makubaliano yanafikiwa mpaka 31 Machi 2016. Udhamini wako utaonekana dunia nzima na mamilioni ya watu kupitia mtandaoni kwenye jarida letu, tovuti, kurasa yetu ya Facebook, Radio na TV, Magazeti na Jarida, na kwenye vipeperushi tunavyovisambaza Afrika Mashariki nzima.

Tuna viwango tofauti wa vya udhamini kuanzia dolla 1,000 mpaka laki moja. Vilevile unaweza kubofya hapa kwa ajili ya kutoa mchango wako unaoanzia dola 20 kwani kiasi chochote kinaweza kusaidia!

Donate Button

Tafadhali wezesha tamasha hili ili liendelee kuwepo kwa ajili ya waTanzania. Mchango wako unathaminiwa sana.

festival artist festival artist

Blitz the Ambassador (GhanaUSA) at SzB 2015 by Pernille Baerendtsen

Bassekou Kouyate Ngoni ba by Thomas Dorn

Wito Kwa Wasanii

Sauti za Busara inatangaza heshima ya utajiri wa utamaduni. Mpaka sasa tamasha limefanikiwa kuleta bendi kutoka Nchi zaidi ya 36 za Afrika, akiwemo  Bassekou Kouyate (Mali), Nneka (Nigeria), Blitz the Ambassador (Ghana/USA), Natacha Atlas (Egypt/UK), Thandiswa Mazwai (South Africa), Alikiba, Nadi Ikhwan Safaa and DDC Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Samba Mapangala (DRC), Tcheka (Cape Verde), Didier Awadi (Senegal), Orchestre Poly Rythmo (Benin), Tumi & the Volume (South Africa) na wengineo wengi.

Kawaida tunapokea moambi zaidi ya 500 kutoka kwa wasanii kila. Miongoni mwao, vikundi 40 huchaguliwa kufanya maonyesho yao kwenye tamasha. Asilimia 50 kutoka Tanzania na wengineo wakiwakilisha Bara la Afrika na kwingineko. Wasanii chipukizi na vijana hufanya maonyesho yao na wasanii wakubwa. Sauti za Busara huonyesha muziki bora wa Afrika uliochanganywa na vifaa kisasa, hutoa kipaumbele kwa muziki wenye utambulisho wa kiutamaduni, vifaa na miondoko ya asili.

Kuomba ushiriki wa ushiriki wa Sauti za Busara 2016, ni rahisi tu jaza fomu za maombi na tuma nakala yako ya muziki (CD na/au DVD) kwenda Busara Promotions kabla ya tarehe 31 July 2015. Kamati ya uteuzi itakutana kwa ajili  Kamati ya uteuzi itakutana kwa ajili ya uteuzi kama tamasha litafanyika na maombi yote yatajibiwa kwa barua pepe kabla ya  mwezi wa tisa.

Unaweza tembelea tovuti yetu na kurasa yetu ya facebook kwa taarifa mbalimbali. Listi ya wasanii watakaoshiriki Sauti za Busara 2016 watatangazwa mwezi wa kumi 2015: “Mungu akipenda!”

 Kama kawaida: karibuni sana, kusheherekea tamasha rafiki katika sayari.

facebook like button

Wasiliana nasi

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Tunapatikana njia ya Uwanja wa ndege , Mkabala na Golf Club

busara@busara.or.tz

Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Tafadhali tuma kwa mwenzio atakayependelea jarida hili. Kujiunga au kujitoa kupata jarida hili, weka barua pepe yako kwenye kiboksi hiki kupitia www.busaramusic.org