Jarida hili linatumwa kwa wanachama 69,123

Lifungue jarida kwenye browser

Usijibu kwa anuwani hii ya barua pepe : Kwa mawasiliano tuma kwenda busara@busara.or.tz

Sauti za Busara Newsletter

Soma jarida kwa: English / Français

 

Lifungue jarida kwenye browser

Sauti za Busara 2016 halitafanyika.
Kutokana na uhaba wa fedha, Busara Promotions inasikitika kutangaza kuwa Sauti za Busara 2016 halitafanyika.
Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions, amesema leo “Uamuzi huu haukuchukuliwa kwa wepesi. Tulijiwekea malengo ya kukusanya dola za kimarekani 200,000 kabla ya Julai, wakati tulipokuwa na matumaini ya kutangaza tarehe za Sauti za Busara 2016. Baada ya mikutano mingi na wadau, tulisogeza muda wetu wa kutafuta fedha hadi Agosti 20. Kiasi cha fedha ambacho tumefanikiwa kukusanya ni kidogo sana, hivyo tumeshinda kuendelea na maandalizi.
Shinikizo zaidi, tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa watu duniani kote wakitaka kujua tarehe za tamasha ili kufanye mipango yao ya safari. Mauzo ya tiketi za Sauti za Busara haijawahi kuwa tatizo, lakini hii inasaidia kulipa 30% tu ya gharama za tamasha ".

Yusuf anaendelea kusema "Tangu mwaka 2004 hatujawa na msaada wowote wa kifedha kutoka serikali ya Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na jitihada nyingi, msaada kutoka kwa wahisani, balozi na wafanyabiashara unazidi kupungua siku hadi siku. Busara Promotions ni shirika lisilo la kiserikali; tamasha haliko kibiashara.Marafiki wa Busara walipendekeza tujaribu kuomba pesa kupitia mitandao. Hata hivyo, kwa kweli ili kuwa endelevu zaidi, kipaumbele chetu kabla ya toleo la 2017 kitakuwa ni kujenga ushirikiano wa muda mrefu na wadhamini na wafadhili ambao wanakubaliana na mtazamo wetu. Mtu yeyote anaesoma ujumbe huu na ana nia ya kusaidia kuiweka Sauti za Busara hai, kukuza ajira nchini, wakati tunaendelea kuung’arisha muziki wetu wenye utajiri wa mila na kukuza utalii wa kiutamaduni Zanzibar na Tanzania, tafadhali awasiliane na Busara Promotions."
“Kila mwaka wiki ya pili ya Februari kwa miaka kumi na mbili, Busara imewavutia maelfu ya wageni kutoka kila pembe ya dunia kuja Zanzibar, wakati ambayo hakuwa msimu wa wageni wengi Hata makadirio yanaonyesha tangu mwaka 2004 tamasha limekiingizia kisiwa mapato ya kiasi dola za kimarekami milioni 70. Wakati huo huo, Shirika la Utangazaji la BBC limeiweka Sauti za Busara kama moja ya "matamasha ya muziki bora na ya kuheshimika zaidi Afrika ". Pia limeingizwa kwenye CNN's Matamasha 7 ya muziki ya kiAfrika unayotakiwa kuyaona" na kileleni kwenye orodha ya Afro-Tourism's ya "Matamasha bora ya Muziki”

Yusuf Mahmoud hatimaye alisema " Wakati mwingine ni muhimu kupiga hatua moja nyuma, kabla ya kusonga mbele. Bodi na uongozi wa Busara itafanya kazi kwa bidii zaidi miezi ijayo, ili kuhakikisha kuanzia mwaka 2017 tamasha linarudi kuwa na nguvu zaidi. Inawezekana itamaanisha kuhama eneo, au kulifanya kila baada ya miaka miwili . Hakika vipaumbele vyetu vitakuwa kulifanya tamasha litoe nafasi zaidi kwa wananchi , wakati tunaelendea kuomba kujenga ushirikiano wa muda mrefu , na sekta za umma na binafsi".

Wakati tamasha likiwa kwenye mapumziko, Busara Promotions itaendelea na shughuli zake za kawaida za kukuza muziki wa kiAfrika, kuimarisha uelewa wa watu na kuboresha sekta ya muziki. Kwa mwaka mzima, Busara itahakikisha wasanii wa Afrika Mashariki wanapata mialiko kwenye matamasha mengine ya kimataifa na kuwezesha kujenga ujuzi kwa wasanii wa ndani na wafanyakazi wa tamasha, kwa njia ya kubadilishana na mafunzo ya uongozi wa sanaa, masoko, habari na ujuzi wa kiufundi . Kazi hii , ambayo inadhaniniwa na Ubalozi wa Norway , Dar es Salaam , haitotetereshwa na uamuzi wa kufuta Sauti za Busara 2016 .

Habari zaidi: www.busaramusic.org  |  www.facebook.com/sautizabusara

Shukrani kwa Ubalozi wa Norway, Dar es Salaam

Shukrani za dhati ziwaendee wale wote waliokubali kudhamini tamasha la Sauti za Busara 2016, kama wafuatao; Zanlink, Inaya Zanzibar, Memories of Zanzibar, Kendwa Rocks, Emerson Spice, Emerson on Hurumzi, Unguja Lodge, Archipelago, Stone Town Café, Colors of Zanzibar, Blue Banana, Mercury’s na Coral Rock Hotel. Asanteni sana! Tafadhali kuwa nasi kwa tamasha la Sauti za Busara 2017 na kuendelea.

Vacancy: Fundraising Manager

Busara Promotions seeks to recruit a committed, professional full-time fundraiser to further develop financial sustainability for the NGO and Sauti za Busara:

  • To secure funding and technical resources for Sauti za Busara festivals 2017-2021,
  • To build long-term partnerships with local and international donors,
  • To negotiate sponsorships with local and international commercial sponsors,
  • To advise and assist in growing self generated revenues.

The successful applicant will be based in Zanzibar. S/he will be computer literate, fluent in oral and written English, with Swahili proficiency also preferred. Salary negotiable, based on experience. Please send CV and letter of motivation if you are interested, to reach busara@busara.or.tz before midnight on Sept 6th.

"Matamasha yanahamasisha vijana kupenda utamaduni wao, hutoa fursa kwa wasanii na wataalamu wa muziki kukutana na kujifunza , yanashawishi uhai wa tamaduni, pia yanatoa nafasi za ajira kwa watu wa ndani na kutoa mifano ya utalii ambayo inathamini na kuheshimu utamaduni wa ndani”. Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi Mtendaji

“Kwa nini wafanyabishara hawasaidii, wakati ndege zote zinazokuja Zanzibar kipindi cha tamasha zinajaa, hoteli na migahawa vinajaa, maduka yaliyopo maeneo ya Mji Mkongwe yanapata wateja wengi zaidi? Kama benki, mashirika ya ndege, hoteli na makampuni ya simu vikichangia hata dola moja tu ya kimarekani kutokakwa kila mtalii mmoja anaeingia kisiwani, bajeti ya Sauti za Busaraingepatikana!”
Julia Bishop, mjumbe wa Bodi ya Busara

“Tunatamani kuona viongozi wa serikali wakiwekeza katika Sauti za Busara na matukio mengine makubwa ambayo yanaitangaza Zanzibar kimataifa, yanaajiri na kujenga ujuzi kwa Watanzania na yanayoweza kuendelea kuleta mapato kwa kupitia utalii wa kiutamaduni kwa miaka mingi ijayo”.

Ally Saleh, mjumbe wa Bodi ya Busara

 

Salif Keita ndani ya Zanzibar


Habari njema kwa wapenzi wa muziki, Nguli la muziki kutoka Mali Salif Keita a.k.a Golden Voice, atakuwepo Zanzibar ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe ijumaa hii. Asante na hongera ziwaendee tamasha la Jahazi Jazz and Literary kwa kulifanikisha hili!

Wasiliana nasi

Busara Promotions
P O Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania
Find us off the airport road, Maisara
Tel: +255 24 223 2423
or +255 773 822 294

Like and follow Sauti za Busara

Thumbs up and “like” Sauti za Busara on www.facebook.com/sautizabusara
Follow the sounds of wisdom on twitter www.twitter.com/sautizabusara

facebookyoutube logotwitter  flickr icon

facebook like button
>
Tafadhali tuma ujembe huu kwa wale watako penda. kwa kujiunga au kujiungua kwenye jarida letu, andika anuani yako ya barua pepe kwenye kisanduku kwenda www.busaramusic.org