4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Angola
Results: 1 to 1 of 2
  • Aline Frazão

    Country  Angola
    Genres roots fusion
    Website /oficialalinefrazao
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Clave Bantu (2011 ); Movimento (2013)

    Aline Frazão
    Aline Frazão

    Akiwa na wazazi kutoka Angola, bibi na babu kutoka kutoka Cape Verde, Brazil na Ureno, Aline Frazã alizaliwa na kukulia Luanda. Alianza kuonekana jukwaani akiwa na umri wa miaka tisa, tangu akiwa ameanza kujifunza kupita njia ya miziki ya asili ya Angola na Cape Verde, bossanova kutoka Brazil, fado kutoka Ureno pamoja na jazz. Alipofikia umri wa miaka 15 tu, alimsikia kwamara ya kwanza Ella Fitzgeral na kugundua sauti ya jazz: ‘nilijisikia kama nimegundua mwelekeo mpya, sauti kama chombo…Jazz ilifungua milango katika akili yangu’.

     

    Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Aline alihamia Ulaya kwa ajili ya masomo ya Mawasiliano chuo kikuu. Lisbon, Barcelona kisha mjini Madrid. Aliboresha ujuzi wake wa mziki, uandishi na kutumbuiza peke yake katika migahawa na baa. Akiwa anataka kuunganisha mapenzi yake mawili ya kusafiri na kuimba, Aline alifanya kazi Paris, Dublin, Lisbon, Luanda, Brussels, London na Buenos Aires. Hivi sasa ainaishi Santiago de Compostela, ambapo anafurahia maisha ya taratibu na anaweza kuweza weka mazingatio zaidi katika muziki wake.

     

    Bado katika akili ya Aline, Luanda inazidi kumuita. “Mambo hayaishi kubadilika Luanda, ubunifu na watu; vitu vyote vinabadilika haraka. Utasikia kuduro mpya kila siku, msanii mpya, dansi mpya…Kwa msanii yeyote, Luanda ni sehemu ya kuvutia iliyokua na tofauti na kushawishi”. Kwa Aline, Luanda pia ni nyumbani,“hapawezi kuwa pabaya”, ni jiji linalomsisimua kifikra na kiubunifu, sehemu ambayo angependa kurudi na kuishi mwishowe. Mnamo mwezi wa tisa 2011, Aline Frazão aliingia studio kurekodi albamu yake ya kwanza. ‘Clave Bantu’ inahusisha nyimbo kumi na moja ambazo amezitunga mwenyewe katika miaka yake minne alivyokuwa safarini. Nyimbo iliyobeba jina la albamu lilipewa ari wakati Aline aliposikia mtangazaji wa Kihispania akielezea jinsi muziki kutoka Congo na Angola ulisafiri kuvuka bahari ya Atlantiki na jinsi ulivyozalisha aina tofauti ya muziki pamoja na kuathiri muziki wote wa Wamarekani weusi. ‘nilivutiwa na hilo kwa sababu hiyo ndio ilikua asili yangu, mizizi yangu, na miondoko ambayo inanifanya nijisikie hai.

     

    Hivyo niliandika ‘Clave Bantu’ kama kushukuru miondoko hii yote – sio nyimbo tu, sio muziki tu ila ni mwenendo wa maisha; ni tamaduni; ni kuhusu miondoko ya kuishi maisha yako’. Mwaka 2013, alirekodi na kutengeneza albamu yake “Movimento’. Mwaka 2014, DJ maarufu na mtangazaji wa BBC Rita Ray alikutana na Aline Frazão katika Atlantic Music Expo mjini Praia, Cape Verde.

     

    Aline alieleza kuwa yeye ni sehemu ya kizazi cha wanamuziki baada ya mapinduzi wanaochukua mila zao na mazungumzo ya mabadiliko endelevu ya muziki kwa waafrika waishio nchi za nje na wakati huo huo akiwa anafyonza ushawishi mwingine katika sehemu tofauti duniani ili kutengeneza aina ya muziki wa kipekee. Aline anaendelea kusema, ‘Muziki ni njia nzuri ya kuingia katika hisia zako na kuweza kuwasiliana na kitu na kuelewa kwamba wakati mwingine lugha pekee haitoshi. Naandika nyimbo za mapenzi na nyimbo za huzuni pamoja na nyimbo za kumbukumbu:hii pia ni hisia yenye kuendelea katika muziki’.

    lusophone_film_festival
    with support from Lusophone Film Festival Nairobi