4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Benin
Results: 1 to 1 of 1
  • Orchestre Poly Rythmo de Cotonou

    Country  Benin
    Genres afrobeat roots fusion
    Website www.polyrythmo.com
    FestivalSauti za Busara 2011

    Orchestre Poly Rythmo 2009 ep 1

    Orchestre Poly Rythmo de Cotonou
    Orchestre Poly Rythmo de Cotonou

    Kundi la Le Tout Puissant Orchestre Poly Rythmo De Cotonou ni moja siri kubwa iliyojificha ndani ya Afrika Magharibi. Kundi hili Gwiji la Muziki limeshafanya maonyesho na magwiji wa muziki Afrika kama vile Fela Kuti, Miriam Makeba, Manu Dibango na Orquesta Aragon. Mnamo mwaka 1969 ikitumia chanzo cha muziki wenye midundo ya kimuziki ya ngoma asilia ya sherehe za Vodoun kutoka nchini Benin. Ochestre Poly Rythmo iliundwa, kama vile haitoshi wana Poly Rythmo waliongezea vionjo muziki wao kwa kuuchanganya muziki wao na wakali wa miaka hiyo kama vile Johnny Hallyday ,Dalida na James Brown. Mchanganyiko huo wakibunifu uliunda aina ya muziki ya kipekee ulioiwezesha bendi kupokea heshima kubwa katika anga yakimuziki na kukubalika sana Afrika Magharibi kote. Hadi hii leo wamesharekodi zaidi ya nyimbo 500 vikiwemo vibao vyao vikali kama ‘Gbeti Madiro’ na ‘Mille Fois Merci’.

     

    “Tumeshafanya kazi mara nyingi tu na Fela Kuti kila alipofanya maonyesho yake Cotonou [mji Mkuu wa Benin] na mara nyingi tulikutana naye EMI Studio Lagos nchini Nigeria”alisema Clement mmoja wa viongozi wa Poly Rythmo. Mpaka kufikia mwaka 1980 bendi hii ilifanyikiwa kufanya maonyesho katika nchi mbalimbali barani Afrika kama vile Niger, Togo, Nigeria, Burkina Faso, Angola na Cote d’Ivoire. Lakini kutokana machafuko ya kisiasa na kuyumba kwa uchumi nchini Benin na vilevile kufariki kwa mpiga gitaa wao mashuhuri Bw Bernard Papillion Zoundegnon na Bw Yehousi Leopold ilifikirika kwamba kutokana na matatizo hayo ingekua ndio mwisho bendi hii. Lakini takribani miaka arobaini sasa tangu kuanzishwa kwa kundi hili, Orchestre Poly Rhytmo wapo tayari kabisa kukuletea burudani kwa mara ya kwanza ndani ya Africa Mashariki, wakiwa njiani kuelekea katika ziara yao ya kwanza yakimuziki nje ya bara la Afrika kuelekea nchi za Ulaya wakipitia Zanzibar.