4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Cape Verde
Results: 1 to 1 of 2
 • Ary Morais

  Country  Cape Verde Norway
  Genres acoustic dance traditional
  Website /arymorais
  FestivalSauti za Busara 2012
  Recordings

  Ka bo bayembora (1999); Abraço Tradicional (2008)

  Ary Morais
  Ary Morais

  Unapozungumzia suala la muziki huwezi kuacha kuzungumzia kisiwa kijulikanacho kwa jina la Cape Verde hasa kutokana na umaarufu wa mwana mama Césaria Évora.

  Akiweka maskani yake ndani ya Norway mpiga gita, mwandishi wa mashairi na mwimbaji si mwingine bali ni Ary Morais ambaye kwa sasa anawakilisha vyema kuusambaza utamaduni na muziki wa watu wa Cape Verde.

  Ary Morais amekulia katika muziki na mashairi. Alipokuwa na umri wa miaka 15 ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda jukwaani mwaka 1990. Mwaka 1995 alihamia Norway akitokea Cape Verde. Mwaka 1999 aliachia albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ka Bo Bayembora na akaanza kufanya maonyesho mengi sana katika bara la ulaya. Ary anakiri kwamba safari yake kwenda Cape verde imempa changamoto nyingi sana kama mwanamuziki lakini anashukuru kwamba sauti yake kuwepo Norway inaaanza kukomaa. Albam yake ya karibuni yenye jina la album Abraço Tradicional aliitoa mwaka 2008.

  Alishirikiana na mwimbaji mwenye kuheshimika na mwenye asili ya Cape Verde, muziki wake ni wa hisia na mchanganyiko wa uhalisia tofauti. Pamoja na bendi yake katika maonyesho yao wanakuthibitishia kukuletea ladha halisi ya muziki wa Cape Verde.

  Norwegian-Embassy-artists-sponsor
  Thanks to Norwegian Embassy