4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Guinea Bissau
Results: 1 to 1 of 2
 • Karyna Gomes

  Country  Guinea Bissau
  Genres acoustic fusion roots traditional
  Website /karyna.gomes
  FestivalSauti za Busara 2017
  Recordings

  Mindjer, 2014

  "Amor Livre", Karyna Gomes

  Karyna Gomes
  Karyna Gomes

  Karyna Gomes ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 21 alipokuwa mwanafunzi huko nchini Brazil.  Anasema kuwa muziki umo ndani ya damu yake, alipokuwa mdogo alikuwa amezungukwa na familia ambayo wakipenda kuimba na pia kusikiliza muziki ya aina tofauti.

  Karyna ameishi barani Afrika, pia Marekani na Ulaya, hivyo muziki wake unachanganya mahadhi ya sehemu zote hizo alizoishi.

  Mwaka 2005 Karyna alianzisha kikundi chake mwenyewe ambapo yeye ndio muimbaji mkuu.  Na mwaka huo akachaguliwa kushiriki kwenye tamasha la CPLP huko Bissau, ambapo aliimba na wasanii mashuhuri kama Tito Paris kutoka Lusophone.  Mwaka 2007 alichaguliwa kufanya ziara na kurekodi na kikundi mashuhuri cha Super Mama Djombo, ziara hiyo ilifanyika nchi nyingi. 

   

  Mwaka 2014 alitoa albamu yake ya mwanzo iitwayo ‘Mindjer” yenye maana ya mwanamke.  Nyimbo za albamu hiyo zinasima jinsi wanawake walivyo mashujaa na wenye ukakamavu kimaisha.  ‘Mindjer’ ilipata umashuhuri na sifa nyingi huko nchini Ureno, na Karyna akapokea tuzo tatu tofauti, tuzo ya sauti bora, tuzo ya mwanamuziki mwanamke aliyebora na tuzo ya albamu bora. 

   

  Karyna alianza ziara yake ya kutangazia albamu yake mpya hapo mwaka 2015, kwenye tamasha la Atlantic Music Expo na kuendelea na ziara kwa kushiriki matamasha mengine tofauti.

   

  with thanks to Gindungo Artist Development