4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Somaliland
Results: 1 to 1 of 1
  • Sahra Halgan Trio

    Country  Somaliland
    Genres traditional pop fusion
    Website athosbook.com
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    Somaliland, 2009; Faransiskiyo Somaliland, 2015

    Sahra Halgan Trio
    Sahra Halgan Trio

    Sahra Halgan ni muimbaji mwenye sauti nyororo kabisa.  Nyimbo zake zina mahadhi ya kisomali ambayo yanakaribiana sana na mahadhi ya kisudani na nchi nyengine za uarabuni. 

    Takriban Sahra Halgan huwa anaimba na kupiga makofi tu bila ya kinanda cha aina yoyote.  Lakini hivi karibuni amekuwa akishirikiana na wanamuziki wawili wanaotoka Ufaransa, ambao ni Aymeric Krol na Mael Saletes na wanapiga muziki wanaouita ‘Muziki mchanganyiko kutoka Somaliland’

    Sahra aliondoka Somalia wakati wa vita vya mwaka 1993 na kukimbilia Ufaransa.  Wakati huo nchi iligawanyika kati ya wale waliokuwa wakampinga Siad Barre na wale waliokuwa wanamuunga mkono.  Watu wa kaskazini ya nchi wakajibagua na kujiita Somailand.  Na huko ndipo kwao Sahra Halgan.

     “Nilianza kuimba nikiwa nina miaka kumi na tatu, wakati huo Somalia ilikuwa ni nchi ya amani kabisa” alisema Sahra. “Na wakati vita vilipoanza nilijitolea kama ni mhudumu msaidizi wa madaktari, japo kuwa sikuwa nina elimu ya udaktari, nikitumia sanaa yangu kuwaliwaza waliojeruhiwa.” Aliendelea kusema

    Wakati wa utawala wa Siad Barre, watu walikatazwa kuimba na kupiga ngoma.  Halgan akaanza kuimba nyimbo za kimapinduzi.  Halgan alianza kuimba nyimbo za kumpinga dikteta Barre, na akienda kutembelea kambi zilizopo misituni, ambapo majeruhi walikuwa wanatibiwa.  Akenda huko kuimba nyimbo za kimapinduzi na kuwahamasisha wapiganaji.

    Baada ya kuishi Ufaransa kwa miaka mingi, Sahra Halgan alirudi Hargeisa, mji mkuu wa Somaliland na kufungua studio ambazo ndio za pekee mjini humo, na wasanii wote wanatumia studio hizo.  “Madhumuni ya studio hizi ni kulitangaza jina la Somaliland lijulikane kote, tukumbukwe na watu wote duniani kama Somaliland ni nchi tofauti na Somalia. Na ni nchi ya amani, ina wananchi million nne”. Alisema Sahra Halgan 

     

    travel sponsor Sahra Halgan
    with thanks to Baam Productions and CNV