4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > South Africa
Results: 1 to 1 of 16
  • BCUC

    Country  South Africa
    Genres urban acoustic spiritual
    Website blackmajor.co.za
    Facebook /bantucontinua
    FestivalSauti za Busara 2019, 2023
    Recordings📼Our Truth, 2016; Emakhosini, 2018; The Healing, 2019

    BCUC 'Nobody Knows' official video

    BCUC
    BCUC

    Muziki wa watu na kwa watu . Bantu Continua Uhuru Consciousness (BCUC) ni kikundi kutoka Soweto, Afrika Kusini. Kwa muziki wao, moja kwa moja kutoka kwa mababu, BCUC inahoji mtazamo wa kawaida wa ulimwengu juu ya Afrika ya kisasa. Kama inavyoonekana katika Sauti za Busara 2019 na matamasha mengine duniani kote, BCUC hukonga hadhira, kimwili na kihisia, kwa mlipuko wa shauku, furaha na mahadhi yenye kuvutia

    Wakitumia filimbi ya kitamaduni, midundo, besi na gitaa la kutikisa. Ikiongozwa na sauti mbichi ya upambanaji ya Jovi, rapu zinazotiririka za Luja na Hloni, sauti tamu na za wazi za Kgomotso - mwanamke pekee katika bendi - na nyimbo za wote wanne kwa mvuto wa kipekee.

    BCUC inachukua mashabikii kwenye safari ya kuvutia kwa ulimwengu wa siri wa Afrika ya kisasa. Wanapinga mawazo ya kimagharibi na kuonyesha Afrika Kusini baada ya ubaguzi wa rangi kutoka kwa mtazamo changa, wenye nguvu na wa kisasa. Katika lugha kumi na moja, BCUC inaingia katika ulimwengu wa roho unaowavutia. Wakati huo huo, wanajadili hali halisi mbaya ya mahali ambapo mfanyakazi asiye na kazi anakaa chini milele. Hatimaye tunatambua Afrika ya BCUC si maskini hata kidogo, bali ni tajiri wa mila, desturi na imani.

    "Tunajiona kama wapigania uhuru wa kisasa ambao wanapaswa kuelezea hadithi ya zamani, sasa na ya baadaye ya Soweto kwa ulimwengu." – ‘Jovi’ Nkosi, mwimbaji