4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > spoken word
Results: 1 to 1 of 9
 • BCUC

  Country  South Africa
  Genres urban acoustic spiritual spoken word
  Website blackmajor.co.za
  Facebook /bantucontinua
  FestivalSauti za Busara 2019
  Recordings

   Emakhosini, 2018

  BCUC - Yinde (Live at Markon Recording Studio)

  BCUC
  BCUC

   Bantu Continua Uhuru Consciousness (BCUC) huwapagawisha watazamaji - kimwili na kihisia kutokana na aina ya maonyesho yao. Wanafanya muziki wenye nasaba kutoka kwa mababu, BCUC inahoji mtazamo wa ulimwengu kuhusu Afrika ya sasa. Vitu muhimu kwenye nyimbo za BCUC ni filimbi za jadi, ngoma na gitaa ya roki yenye kupambwa na sauti maridhawa ya Jovi, huku ikiunganishwa na rap ya Luja na Hloni, bila ya kusahau sauti ya kupendeza ya mwanadada pekee Kgomotso.

   

  BCUC maskani yake makuu yapo Soweto, wameubatiza muziki wao kama funky pekee ya kiasili. Huwasafirisha watu kimuziki kwenda katika maficho ya Afrika ya sasa. Wanahoji mitazamo ya magharibi na kuwaonyesha maisha baada ya ubaguzi wa rangi kutoka kwa vijana wenye nguvu na mitazamo ya kisasa. Katika lugha kumi na moja BCUC inaona mapungufu ya roho za kibinadamu.  Wakati huo huo wanajadili mambo magumu na halisi katika maisha ya kila siku, na mwishowe wanagundua Afrika sio masikini hata kidogo lakini tajiri kwa utamaduni na Imani. 

  With thanks to Concerts SA
  With thanks to Concerts SA