4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > J
Results: 1 to 1 of 17
 • Jackie Akello

  Country  Uganda
  Genres band pop fusion
  Website akellomusic.com
  Facebook /Akello-448633765309735
  FestivalSauti za Busara 2019
  Recordings

   Akello, 2016

  Jackie Akello- Apwoyo. (Official Video)

  Jackie Akello
  Jackie Akello

  Jackie Akello ni mwimbaji na mtunzi kutoka kaskazini mwa Uganda, ambaye anaimba ka lugha ya Acholi, Luganda, Swahili na Kiingereza.

  Akello anajulikana kwa nyimbo kadhaa kama "Amari" (a love ballad), "Samanya" (gospel hit) na "Apwoyo", ambayo inaelezea mateso ya watu wa Acholi katika mapambano na LRA (Lord's Resistance Army).

  Akello alifanya kazi na bendi kadhaa kabla ya kwenda solo. Aliwahi kuwa na Bendi ya Janzi, The Sundowners na sasa akiwa na Amari Band. Alifanya kazi na Levixone kwenye nyimbo ya injili iliyopata umarufu "Samanya". Pia ameshawahi kushirikiana na Kaweesa, Suzan Kerunen, Lilian Mbabazi, Maurice Kirya, Myko Ouma, Tshila na Kinobe Herbert.

  Akello anaamini "ndoto ya mwanamke ni mwanzo wa ukuu". Ni kutokana na hili anapata tumaini la kuonyesha ukuu wa msichana wa bara la Afrika.

  Mpaka sana ameshafanya maonyesho kadhaa ikiwemo Music Days 2014 na 2017 jijini Kampala, Blankets and Wine, Bayimba festival na shughuli mbalimbali na vilevile kufanya ziara ya kimuziki Nchini Ufaransa.