4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2015
Results: 1 to 1 of 36
 • Ahamada Smis ‘Origines’ Trio

  Country  Comoros France Zanzibar
  Genres traditional hiphop fusion
  Website www.colomberecords.com
  FestivalSauti za Busara 2015
  Recordings

  Origines (2013); Etre (2010); Hip Hop Live (2006); Ou Va Ce Monde? (2003); Gouttes d'eau (2001)

  Ahamada Smis trio "Origines" live @ Babel Med Music 2014

  Ahamada Smis ‘Origines’ Trio
  Ahamada Smis ‘Origines’ Trio

  Ahmada Smis, ni muimbaji na muandishi wa nyimbo kutoka visiwa vya Comoro na amekua akiishi Marseilles tangu alipofika Ufaransa akiwa na miaka 10. Rapa na msanii huyu wa maneno amekua akichanganya muziki wa Comoro na ushairi wa mjini katika hisia za afro-ngoma.
  Hadithi ya Ahmada Smis inaundwa na maneno na muziki, ambao wengine wanauelezea kama ushairi wa mashindano. Kati ya Misukumo na ushawishi wake mwingi, anataja Marseille, imani, ushairi, hadithi za watu kutoka pande zote za dunia pamoja na asili yake.


  Ahmada Smis amejenga mchanganyiko wa kipekee wa muziki wa kufoka foka na muziki wa ulimwengu. Akiwa kijana Marseille, wakati marapa wakifaransa walipopata ukubali kama majambazi, Ahmada alikua akiongelea kuhusu amani na matone ya maji. Tangu mwanzo alisaidiwa na 3e Oeil (Jicho la tatu), kikundi cha eneo hilo ambacho kilithamini ulaini na nguvu ya utambulishi wake. Muonekano wa Ahmada ulizidi na mwaka 2001 alitoa nyimbo yake ya kwanza ya mchanganyiko Gouettes d’eau (Matone ya Maji) katika lebo ya muziki ya Colombe ambayo alianza mwaka huo huo. Mnamo mwaka 2003 alitoa kazi yake ya nyimbo 6 Ou Va Ce Monde? (Dunia inakwenda wapi) na albamu yake ya kwanza, Etre (kuwa).


  Ahmada Smis hakutaka kufanya pupa. Alitumia muda kwa manufaa yake. Baada ya miaka ya kazi ngumu na uvumilivu, alitoka katika kutunga mashairi yake katika chumba cha kiwanda cha chuma na kufikia kuandika katika studio za kitaalam za muziki. Alijitengeneza kwa umakini ulimwengu wake na kila mtu alitarajia atoke na mashairi ya maisha ya mtaani, alishangaza kila mtu na ukweli wake. Albamu ya Etre (kuwa) ilishirikisha wasanii kama Pierre-Laurent Bertolino, Cyril Benhamou, David Walters, Sibongile Mbambo, Miquu et Baltazar Montanaro, Mike Aub, Bawuta Kin na Staff Benda Bilili. Kupitia ushirikiano huu, albamu yake ilitokea kua ya kutoa heshima kwa mabadilishano ya tamaduni.  Mradi mpya anaoufanya Ahmada Smis ‘Origines’, iliyotoka mwaka 2013, iliyotengenezwa katika warsha ya kuunda muziki huko Mayotte, Grand Comore, Anjouan, Dar es Salaam, Zanzibar na visiwa vya Reunion. Ni makutano kati ya miziki na ala za asili.


  Wakati akiwa katika eneo la Bara la Hindi, Ahmada Smis alipata ushawishi kutoka katika asili ya sambe, twaraba, mgodoro, maloya, deba (vyote vikiwa sehemu ya mchanganyiko wa urithi wa tamaduni kati ya Wabantu na Waarabu).


  Kwa maonesho ya laivu ya ‘Origines’ katika Sauti za Busara, Ahmada Smis atasindikizwa na wapiga ala tofauti wawili ambao walishawahi kushiriki hapo awali. Akiwa na asili ya Grand Comore, Soubi anapiga gaboussi na dzenze. Mohamed Issa Matona, mwalimu wa muziki na mwanachama wa vikundi vya Zanzibar, anapiga uud, violin na qanun.