4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2017
Results: 1 to 1 of 35
  • Afrijam Band

    Country  Tanzania
    Genres fusion jazz reggae
    Website /Misoji-Nkwabi-and-Afrijam-1520448294936766
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    Utu wa Mtu 2009; Usawa 2014

    MISOJI AND AFRIJAM BAND PERFORMING AT MARAHABA FESTIVAL 2015

    Afrijam Band
    Afrijam Band

    Misoji Nkwabi alijinyakulia ushindi wa Bongo Star Search hapo mwaka 2008 na kurekodi albamu yake inayoitwa Utu wa Mtu.  Albamu hii ilikuwa na nyimbo kumi na mbili zikiwa zote zinagusia maisha ya kisasa yanayowakumba vijana wa kitanzania, hususan kwenye mambo ya kijamii na kiafya kama vile maambukizi ya virusi vya ukimwi.

    Misoji alianza kuimba akiwa mdogo sana kwenye kundi la kwaya la kanisani, ambapo mama yake alikuwa ni mpigaji wa ala ya muziki.  Baadae alianza kuimba nyimbo za wasanii tofauti na hatimae akawa ni mtunzi wa mashairi yake mwenyewe.

    Mwaka 2014 aliunda Kikundi cha mziki cha Afrijam, ambacho kilishiriki kwenye matamasha tofauti nchini Tanzania kama vile Karibu Music Festival, Marahaba Festival na Tamasha la Bagamoyo.

    Mwaka 2009, Misoji alishirikiana naMombots Production kwenye filamu ya muziki huko nchini Ujerumani. Yeye ana shahada ya sanaa ya maigizo ambayo alisomea chuo cha sanaa TASUBA huko Bagamoyo.

    Kwenye kikundi hichi, Misoji anaimba na wadogo zake wawili, Nsami na Nshoma.