4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Festival Line-up > 2022
Results: 1 to 1 of 19
 • Sampa the Great

  Country  Zambia
  Genres hiphop fusion
  Website www.sampathegreat.com
  Facebook /sampathegreat
  FestivalSauti za Busara 2022
  RecordingsThe Great Mixtape, 2015; Birds And The BEE9, 2017; The Return, 2019.
  On stage Feb 2022

   Sat 12,  9:20pm Old Fort Main Stage

  Sampa The Great - Final Form (Official Video)

  Sampa the Great
  Sampa the Great

  Sampa The Great huteremsha mashairi yenye kufikirika na kusisimua. Muziki wake una muunganiko wa ushairi, Rap na bluz huonyesha utofauti kwa vijana na kupenya mipaka yote.

  Mzaliwa huyu wa Zambia aliyekulia Botswana, alianza kupata umaarufu baada ya kutoa nakala zake mbili, The Great Mixtape (2015) na Birds and the BEE9 (2017), na baadae mwaka 2019 kutoa albamu yake ya kwanza ‘The Return’.

  The Return ilikuwa albamu bora ya mwaka ya Busara Promotions mwaka 2019. Albamu imesheheni ubunifu na imechanganya hiphop, neo-soul, injili, afrobeat na jazz. Ilifungua mjadala wa Uhuru, kujielezea, urithi na uhamiaji. Ni hatua ya kujitambua iliyochochewa na maisha ya Sampa nchini Australia, kifikra, kiroho na utamaduni kutoka kwa mababu zake, Zambia. 

  Sampa ameweza kujikusanyia mashabiki dunia nzima kutokana na maonyesho yake ya laivu. Sampa ameshafanya maonyesho kwenye matamasha mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Glastonbury, Splendour in the Grass, Sugar Mountain, Vivid Live, Dark Mofo, Love Supreme Jazz Festival, Down the Rabbit Hole, BRIC Celebrate Brooklyn, Bushfire na mengineyo. Vilevile ameshafanya maonyesho ya ufunguzi wa wasanii wakubwa kama Burna Boy, Kendrick Lamar, Ms Lauryn Hill, Thundercat, Ibeyi na Little Simz.