4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Addis Acoustic Project ft Melaku Belay
Results: 1 to 1 of 1
  • Addis Acoustic Project ft Melaku Belay

    Country  Ethiopia
    Genres acoustic jazz traditional
    FestivalSauti za Busara 2014
    Recordings📼

    Tewesta, 2011

    Addis Acoustic Project by Girum Mezmur "Yetintu Tiz Alegn"

    Addis Acoustic Project ft Melaku Belay
    Addis Acoustic Project ft Melaku Belay

    Addis Acoustic Project ni kikundi cha vijana wenye vipaji wanaopatikana katika viunga vya mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia, wanafanya muziki ambao ulikuwa unapigwa kwenye miaka ya 1950 mpaka 1960, wanaoufanyia ubunifu wa uchanganyaji wa ala mbalimbali kama Mandolin, Accordion na nyinginezo.
    Addis Acoustic linaongozwa na mpiga Gitaa Girum Mezmur ambaye anauenzi muziki wa zamani kwa kuurudisha tena na ubunifu wa kisasa. Muziki wake huvutia pande nyingi za Afrika na Dunia kwa ujumla, bendi inamchanganyika wa wakongwe na kizazi kipya na hivyo kuwa sababu tosha ya kutoa burudani isiyo kifani kila wapandapo jukwaani.

    Kiongozi na Muasisi wa Addis Acoustic Project ameshafanya maonyesho na wasanii mbalimbali kama Aster Awoke, Teddy Afro, Ali Birra na Mahmoud Ahmed. Mahusiano yake kimuziki na Mahmoud Ahmed yalimpelekea kupata zaira za kimuziki dunia nzima kuanzia Afrika, Asia, Ulaya mpaka Amerika. Girum ameshafanya onyesho kwenye matamasha makubwa ya kimataifa kamaWOMAD, The Montreal Jazz Festival, Roskilde Festival na kadhalika. Girum alipata nafasi ya kushiriki katika tuzo ya Dunia ya BBC Radio World Music Award mwaka 2007 akiambatana na Mahmoud Ahmed kama mpiga Gitaa wake, na hapo ndipo Mahmoud Ahmed alipochaguliwa kama Msanii Bora kwa upande wa Afrika. Girum ameshafanya maonyesho na wasanii mbalimmbali maarufu kama Angelique Kidjo, Ray Leman na Brice Wassi.
    Tangu kuonekana kwake mwaka 2008 Addis Acoustic imekuwa kama ndio safari yake ya mafanikio. Kwa sasa Addis wanafanya maonyesho yao kila wiki katika ukumbi maarufu “Jazzamba” mjini Addis Ababa. Addis wameshatoa albamu yao ya kwanza mwaka 2011 waliyoipa jina la “Tewesta” (kumbukumbu)
     

    ET-Master-logo-with-Star
    With thanks to Ethiopian Airlines