4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Alikiba
Results: 1 to 1 of 1
  • Alikiba

    Country  Tanzania
    Genres pop
    Website /rockstar.alikiba
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Cinderella, (2007); Alikiba 4 Real (2008); Hands across the World (with R Kelly, Fally Ipupa, 2Face, Amani, 4x4) (2010); Dushelele (2011)

    Alikiba - Mwana (Official Music Video)

    Alikiba
    Alikiba

    Alikiba Saleh Kiba alizaliwa mwaka 1986. Ni mwanamuziki wa kitanzania, mtunzi, dansa na muigizaji. Ni mmoja kati ya wasanii nyota na umaarufu wake wa kimataifa unaendelea kukua kwa kasi.



    Albamu ya kwanza ya alikiba Cinderella ilishinda tuzo ya Kilimanjaro Music Award na ikawa rekodi yenye mauzo makubwa zaidi Afrika Mashariki mwaka 2008. Alifuatishia hii na Alikiba 4 Real ambayo ilijumuisha nyimbo kubwa kabisa za Nakshi Mrembo, Nichuum na Usiniseme. Mafanikio ya albamu yake hii ya pili yaliimarisha jina la Alikiba katika ulimwengu wa umaarufu Tanzania.
     


    Hadi kufikia hapo, hata mashabiki wake huko Mashariki ya Kati walikua hawajatosheka na kazi nzuri za msanii huyu kijana. Alikua akivunja rekodi na kuvuka mipaka. Wakati kazi yake ya kimuziki ikikua, Alikiba alipokea ofa za kucheza katika timu za Tanzania za mpira wa miguu. Alizikataa na badala yake kuamua kuingia katika maonesho ya mavazi, kwa vile hili halikichukua muda wake mwingi wa muziki.



    Mnamo mwaka 2010 Alikiba alishirikiana na muimbaji-mtunzi na prodyuza wa Marekani R Kelly katika mradi wake uliopata mafanikio makubwa wa One8 pamoja na Fally Ipupa, 2Face na wasanii wengine wakiafrika. Rkelly alimpa sifa za kipekee Alikiba kwa uzuri na upekee wa sauti yake, na kumfanya muimbaji mkuu katika nyimbo ya mradi huo, Hands across the World.



    Ukija katika uwaniaji na ushindi wa tuzo, Alikiba anazo tele. Alikiba alichaguliwa kuwania nafasi ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki (African Music Awards), Mshindi wa nyimbo bora ya Zouk/Rhumba pamoja na Mwandishi Bora Tanzania, Msanii Bora wa Kiume (Kili Music Awards). Mwaka 2010 London, alishinda Tuzo ya BEFFTA katika kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa ambapo alikua akichuana na Msanii wa Nigeria 2 Face Idibia, Beyonce na Akon. Katika shindano hilo hilo aliweza kuondoka na tuzo ya Msanii wa Kiume mwenye Mvuto Zaidi.



    Mwaka 2011 Alikiba aliachia Dushelele wimbo ambao alishiriki kuutengeneza pamoja na kuuongoza. Kwa wakati mwingine tena akithibitisha kwamba ana mguso mkali ukija katika masuala ya muziki. Dushelele ilishinda tuzo ya Kilimanjaro Music Award kama nyimbo bora ya Zouk. “SingleBoy/Single Girl” ilifata muda mfupi baadae; ikiwa ni ushirikiano na Lady Jaydee ambayo pia iliongoza katika chati. Ali Kiba alitumia muda wake mwingi katika mwaka 2012 kushirikiana na wasanii tofauti na kuanza  uzalishaji wa muziki, mafunzo ya kuigiza pamoja na uandishi wa filamu.
     


    Mwaka 2013 Alikiba alisaini mkataba na Sony Music Africa. Albamu yake ya tatu inayosubiriwa kwa hamu itakayojumuisha ushirikiano na Fally Ipupa ipo mbioni kutoka.



    Kama ilivyo kwa wasanii wenzake wengi katika tasnia ya bongo flava Tanzania, Alikiba kwa kawaida hutumbuiza kwa njia ya ‘playback’. Ingawa haina shaka kwamba kwa onesho hili la nadra na aina yake katika tamasha la Sauti za Busara 2015, Alikiba atatumbuiza na wasanii wa kweli, full mzuka 100% live!