Results: 1 to 1 of 1
Asia Madani
Country Sudan Egypt Genres roots traditional spiritual Website www.musicinafrica.net Facebook /asia.madani2 Instagram /asiamadaniband Festival Sauti za Busara 2019, 2023 Recordings 📼Al Zoul, 2018 Asia Madani ni mwimbaji wa Sudan anayeishi Cairo, Misri.
Anaimba nyimbo za kitamaduni za Sudan na kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika. Muziki wake unaonyesha fahari katika urithi wake kama Mwafrika na kama mwanamke mwenye nguvu na sauti ya kipekee na, yenye mvuto. Ni mtaalamu wa kuigiza Zar, ambayo ni ibada ya uponyaji inayojumuisha midundo tata, sauti na densi inayotumika kama matibabu ya kisaikolojia.
Asia alianza safari yake ya muziki akiwa na umri mdogo, akizungukwa na muziki akiwa na baba ambaye alicheza oud na kaka, ambaye ni mtaalamu wa percussion. Asia alihamia Misri mwaka wa 2001 na amekuwa mtu mashuhuri katika tasnia ya muziki ya Misri, akitumbuiza katika kumbi kama vile Cairo Opera House, Salah El-Din Castle, Bibliotheca Alexandrina, Damanhur Opera House na Cairo Jazz Club.
With thanks to Tadamon https://tadamonccmaadi.wpdevcloud.com/