4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Asia Madani
Results: 1 to 1 of 1
 • Asia Madani

  Country  Sudan Egypt
  Genres roots traditional spiritual
  Facebook /Asia-Madani-187059958001209
  FestivalSauti za Busara 2019
  Recordings

   Al Zoul, 2018

  Asia Madani AfriCairo - Mandy | Sofar Cairo

  Asia Madani
  Asia Madani

  Asia Madani ni muimbaji nampiga ala mwenye asili ya Sudani anayeishi mjini Kairo, Misri. anafanya muziki wa Sudan fok na kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika. Asia amejiwekea alama dunia nzima.

  Asia anajivunia muziki wake unaoakisi urithi kama Muafrika na mwanamke shupavu mwenye sauti. Asia ameanza muziki akiwa na umri mdogo ambapo alizungukwa na familia ya wanamuziki, Baba yake alikuwa anapiga Oud and kaka alikuwa mahiri katika kupiga ala za muziki. Asia alihamia Misri mwaka 2001 na akafanikiwa kuwa maarufu katika tasnia na muziki kwa kufanya maonyesho katika kumbi mbalimbali kama Cairo Opera House, Salah El Din Castle, Bibliotheca Alexandrina, Damanhur Opera House, Darb 1718, Cairo Jazz Club na nyingine nyingi.

  Mwaka wa 2015, Asia ilijiunga na Nile Project, muungano wa wasanii takriban 30 kutoka katika nchi zinazopitiwa na Mto Nile, ikiwa na lengo la kuwaunganisha watu wanaoishi katika Mto Nile.

   Mwaka 2016 alijumuika katika ziara ya kimuziki ya Afrika Tour, 2017 US Tour na Europe Tour. Mbali na muziki, Asia anafanya mambo muhimu katika jamii, anajitolea katika kituo cha Mtakatifu Andrew katika mambo ya kijamii.

  Anafundisha muziki na kucheza kwa wakimbizi katika nchi mbalimbali za Afrika. Vilevile ameanzisha kwaya ya watoto katika jamii ya wasudan. Asia huacha ujumbe katika kazi zake za kisanii na kuchukua nafasi katika albamu mbalimbali ikiwemo albamu ya tatu ya Nile Project, Tana. Mwaka 2018 alitengeneza albamu yake ya kwanza, Al Zoul.

  With thanks to Al Mawred Al Thaqafi
  With thanks to Al Mawred Al Thaqafi