4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Bob Maghrib
Results: 1 to 1 of 1
 • Bob Maghrib

  Country  Morocco
  Genres fusion reggae
  Website bobmaghrib.com
  FestivalSauti za Busara 2017
  Recordings

  2012 So Much Trouble in the World (Single); 2013 Africa Unite (Single)

  BOB MAGHRIB@KORSA LIVE-2MTV-OFFICIAL

  Bob Maghrib
  Bob Maghrib

  Bob Maghrib ni kikundi chenye mseto wa wanamuziki kilichoundwa mwaka 2011.  Kikundi hichi kinakusanya wale wanamuziki chipukizi na wanawakilisha muziki wa kisasa wa Morocco.  Wanaimba nyimbo za Bob Marley zile zenye ujumbe wakimapinduzi.  

  Waliunda kikundi hichi kusherehekea miaka 30 tangu kifo cha Bob Marley, japo kuwa yeye ametanguliambele ya haki lakini nyimbo na kazi zake bado zinatunzwa na kuheshimikaduniani kote. Muziki wao unakutanisha na kuchanganya mahadhi, ngoma na mashairi ya“Bob Marley and The Wailers”na muziki wenye asili ya Morocco.  Jitihada kubwa inatumika kutobadilisha muziki wa Bob, bali kuhakikisha maadili haya mawili ya muziki yanaoana kwa vile asili ya miziki hii ni kutoka bara la Africa.

  Baada ya kuwa ziarani nchini Morocco, Egypt, na Ulaya, Kikundi cha Bob Maghrib kimo kazini kuandaa albamu yao ambayo ni utunzi wao wenyewe.  Albamu hii itachanganya nyimbo zenye mahadhi ya kimorocco kama “Gnawa” na “Berber”na muziki kutoka visiwa vya Jamaika.

   

  with thanks to Africa Art Lines and Afrikayna