4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Bonaya Doti
Results: 1 to 1 of 1
  • Bonaya Doti

    Country  Kenya
    Genres acoustic traditional
    FestivalSauti za Busara 2015

    Hot Sounds from Hot Climes - Spotlight Vol. 5.wmv

    Bonaya Doti
    Bonaya Doti

    Akiwa amezaliwa mwaka 1974 Marsabit, kaskini-mashariki mwa Kenya, Bonaya Doti alianza kazi yake ya muziki baada ya miaka kadhaa kua mwanaharakati wa masuala ya kijamii. Anatokea katika kabila la Konso, kundi ambalo liliasiliwa na jamii kubwa ya waBorana. Anaimba kwa lugha ya kiBorana, na aina kinzani yenye asili ya kiafrika na kiarabu yaki Cushi. Ikiwa kwa karibu kabisa inafanana na kiasi kikubwa cha muziki wa kati ya kusini mwa Ethiopia, ina uasili wa watu kutoka Konso.
    Baada ya uhuru mwaka 1963, waBorana walijikuta wakiingia katika mgogoro mkubwa kati ya maafisa usalama wa nchi na waasi waliofahamika kama Shifta ambao ulikula sehemu kubwa ya mkoa. Mgogoro mmoja ulizaa mwingine, katika miaka tele iliyofuata baada ya vita vya Shifta, wizi wa mifugo ulikua ndio sifa iliyotawala kwa muda mrefu ambao ukaongeza mivutano kati ya makabila, ukame pamoja na kusambaa kwa kutekelezwa kwa eneo zima.
    Ni kutoka katika historia hii ya Bonaya ambapo jukumu lake kwa harakati za kijamii na kujenga amani palipoanzia. Lakini pia alitengenezewa kumbukumbu binafsi ya kusumbua katika kipindi chake cha ujana.  Wakati ana umri wa miaka 14, muda mfupi tu baada ya kumaliza elimu ya msingi, alipata ajali ya gari ambayo ilimfanya alazwe hospitali jijini Nairobi. Operesheni katika mguu ilitakikana kufanyika lakini haikuweza kufanyika kwa vile hakukua na mtu wa kusaini ruhusa hiyo kwa ajili yake. Mama yake alikua amefariki na baba yake alimtelekeza. Wakati aliporuhusiwa kuondoka hospitali miezi saba baadae, hakuwa akiweza kutembea bila msaada. Aliweza kurudi kijijini nyumbani kwao na kufika kukuta kwamba baba yake hana habari tena na yeye.  Akiwa ameachwa kujitunza mwenyewe, aliamua kuhamia mji wa Marsabit ambapo alifanya kazi za ajabu – kitu chochote ambacho kilimsaidia aweze kupata kipato. Hii ndio historia katika nyimbo yake “Ayyof Abbo”, (Mama na Baba), uchungu wa mtoto ambao ameshindwa kuwazawadia wazazi wake.
    Baada ya muda alianza kupata nguvu zake tena na akawa na uwezo wa kupata kazi zenye malipo mazuri zaidi, kwanza kama mhudumu katika mgahawa, kisha mjenzi na baadae mfanyakazi katika duka la kutengeneza baiskeli. Aliweza kujipatia umaarufu kama mfanya kazi mwenye kujituma, mwaminifu na mtu wa kutegemewa, kitu ambacho kilimfanya azawadiwe na waajiri wake kwa kupandishwa vyeo pamoja na malipo bora.
    Bonaya aligundua mapenzi yake kwa muziki na kuimba akiwa shule ya msingi. Hivi sasa, akiwa na kipato cha uhakika, aliweza hatimae kupata uhuru wa kufata kitu anachokipenda. Alijiunga na wanamuziki popote pale alipoweza, iwe kwenye harusi, sherehe za asili ama shughuli za umma. Kadri wanamuziki walivyozoea kumuona yuko karibu na wakati mwingine walimualika aimbe pamoja nao. Punde alianza kutunga nyimbo zake mwenyewe na kutumbuiza wakati wowote alipopata nafasi. Kipaji chake kilitambuliwa na mwanasiasa mwenyeji ambae aliamua kutumia muziki wake kama katika kampeni zake. Hii ilienda vizuri kwa muda. Kwa mara ya kwanza, kijana mdogo Bonaya aliweza kupata pesa kutokana na muziki. Fursa hii ilidumu kwa muda mfupi tu hata hivyo na ilidumu kwa muda ule wa kampeni tu. Lakini kwa kupitia uzoefu huu Bonaya aligundua nguvu ya muziki. Aligundua kwamba watu watamsikiliza kwa kupitia muziki wake.
    Badala ya kua mwanamuziki na kujaribu kwenda na wimbi la umaarufu, uibukaji wa uwezo kimuziki wa Bonaya ulijiingiza katika masuala ya kijamii: migogoro na amani; Virusi vya UKIMWI, rushwa ya kisiasa; ukosefu wa ajira kwa vijana. Kwa njia tofauti, Bonaya alijikita katika uimbaji wa kutukuza tamaduni, akichomeka masuala ya kisasa katika fikira za kitamaduni ambazo zilikua zikijulikana kwa kiasi kikubwa na hadhira yake.
    Baada ya fujo za Kenya baada ya uchaguzi mwaka 2007/8, moja ya nyimbo za Bonaya iliyokua inahimiza amani ilichaguliwa na kituo cha redio ya kilugha na muda mfupi baadae kikawa maarufu katika eneo hilo. Baada ya amani kurudi Kenya, rafiki yake alimfuata na kumwambia “Bonaya, nadhani umetoa mchango wako”.  
    Bonaya anasindikizwa na mpiga gitaa mdogo ambaye anapiga katika mahadhi ya afro-arabic ambayo yalizaliwa nchini Ethiopia na Kaskazini mwa Kenya. Kazi yake ya kwanza ya kitaalamu kurekodi ilikua ni Nagai, iliyojumuishwa katika Spotlight on Kenya Music, Vol. 5: Focus on Northern Kenya compilation (2010), iliyorekodiwa katika studio za Ketebul Music ikisaidiwa na Alliance Francaise Nairobi