4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Cheikh Lô
Results: 1 to 1 of 1
 • Cheikh Lô

  CountrySenegal
  Genresroots spiritual
  Website

  http://www.worldcircuit.co.uk/#Cheikh_Lo

  FestivalSauti za Busara 2013
  Recordings

  Ne La Thiass, 1996 Bambay Gueej, 2001 Lamp Fall, 2006 Jamm, 2011

  Cheikh Lô
  Cheikh Lô

  Cheikh Lo ni mmoja kati ya wanamuziki mashuhuri wa Afrika, Mwandishi, Muimbaji, vile vile mpiga Gita mashuhuri na Mpiga Ngoma, amejizolea umaarufu Afrika Magharibi na Afrika ya kati kutokana na ubunifu wake wa kipekee katika kazi zake.

  Cheikh Lo alizaliwa mwaka 1955 katika kitongoji cha Bobo Dioulasso nchini Burkina Faso karibu na mpaka wa Mali, alikuwa anaongea kibambara lugha ya nchini Mali, Wolof lugha ya Senegal na kifaransa. Mapema alipokuwa mdogo aliweza kuonyesha kipaji chake cha muziki ambapo alikuwa anatoroka shule na kwenda kujifunza kupiga Gita na vifaa vingine vya muziki vya kuazima.

  Alipokuwa na umri wa miaka kumi alipendelea kusikiliza nyimbo za aina tofauti hasa nyimbo za Rumba kutoka Kongo ambazo zilikuwa maarufu Afrika nzima.

  Alipokuwa na umri wa miaka 21 alianza kuimba na kupiga vifaa mbalimbali vya muziki na bendi ya Orchestra Volta Jazz ambayo ilikuwa ikipiga aina tofauti ya muziki kutoka Burkina Faso na nchi za jirani na aina nyingine.

  Mwaka 1981 alihamia mjini Dakar nchini Senegar, alikuwa anapiga Ngoma na Mwimbaji mashuhuri wa Ouza kabla ya kujiunga na House Band katika Hotel ya Savanna, ambapo walikuwa wanaimba na kupiga ngoma za mataifa mbalimbali. Mwaka 1984 alikwenda ufaransa na kufanya kazi kwenye Studio kwa miaka miwili katika sehemu ya upigaji ngoma. Alikiri kuupenda muziki wa Kongo na Cameruni na kujifunza mengi katika muziki huo.

  Cheikh Lo albam yake ya kwanza aliitoa mwaka 1990 na kuipa jina la Doxandeme (Mhamiaji) alizungumzia hali ya kuwa mgeni kwenye nchi za watu. Licha ya ubora mdogo wa utengenezaji lakini ilifanikiwa kuuzwa vizuri na kumpatia tuzo ya “Nouvaea Talent” nchini Senegal.  Mwaka uliofuata aliendelea kutoa nyimbo kwa ajili ya albam yake ‘Ne La Thiass’.

  Mara ya kwanza kukutana na Youssou N’Dour ilikuwa mwaka 1989, ambapo Youssou mwenyewe alikiri kuvutiwa na sauti ya Cheikh Lo. “Nilipata kumjua kupitia kaseti yake ya ‘Doxandeme’ nilisikia sauti yake na kusema “Wow” niligundua kitu Fulani katika sauti yake”

  Cheikh aliendelea kufanya jitihada za kuboresha kazi zake ambapo mwaka 1995 Youssou N’Dour alikubali kumrekodia katika Studio yake nchini Senegal. Katika albamu ya Ne la Thiass alishirikiana na Youssou Ndour katika baadhi ya nyimbo kama (Guiss Guiss na Set) na wanamuziki kutoka katika kundi la Youssou. Mwimbo wake wa ‘Set’ ulitumika katika kampeni ya kuhamasisha usafi katika mitaa ya mji wa Dakar, kampeni hiyo ilifanywa na Waziri wa Afya na kuzunguka nchi nzima.

  Albam ya Ne La Thiass aliitowa katika ziara yake ya kimataifa mwaka 1996 ikifuatiwa na ziara nyingine ya bara la ulaya. Kutokana na ubunifu na kipaji katika maonyesho yake watu wengi walimbashiria kuwa mwanamuziki mkubwa duniani na wengine kumfananisha na Bob Marley.

  Mwaka 1997 alizawadiwa tuzo ya Kora nchini Afrika Kusini  na kufuatiwa na ziara nchini Marekani. Mwaka 1999 alipata tuzo ya ‘Ordre National de Leon kutoka kwa Rais wa Senegal. Albamu ya pili ya Cheikh Lo ‘Bambay Gueej’ iliitoa mwaka 1999, ilitengenezwa kwa ushirikiano wa Youssou N’dour na Nick Gold nchini Senegal na baadhi ya rekodi nyingine Havanna na Uingereza. Katika kuhukikisha kila mtu anafurahia aliongeza sauti kutoka Burkina Faso, Mali, na kutia vionjo vya Oumou Sangare, na kumuongeza Richard Egues ‘filimbi’ na James Brown katika "Sexophone".