4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Cocodo African Music Band
Results: 1 to 1 of 1
  • Cocodo African Music Band

    Country  Tanzania
    Genres acoustic band fusion traditional
    Website www.cocodoafricanmusic.com
    FestivalSauti za Busara 2015, 2017
    Recordings📼

    Massawe, 2013; Agwe Mwana, 2013; Mambo, 2013; Shomari, 2013; Mdundiko, 2015;  Imbange, 2015

    Gwe Mwana-Cocodo African Music Band Band-Sunshine Soundtrack

    Cocodo African Music Band
    Cocodo African Music Band

    Muziki wa kikundi cha COCODO ni mchanganyiko wa muziki wa kiafrika na muziki wa jazz, aina ya mziki wao wanauita Panyenje.  Kikundi kiliundwa mwaka 2010 huko Dar es Salaam na kina wachezaji wa dansi wawili ambao ndio watumbuizaji wao wazuri.

    Nyimbo zao siku zote zina ujumbekwa jamii kuhusiana na masuala ya afya, kama vile maambukizi ya virusi vya ukimwi, Malaria na hata Autism.COCODO ni wana harakati na pia wanajivunia kuwa waafrika na watanzania hili linaonyesha wazi kwenye nyimbo zao ambazo huimba kuhusu bara la Afrika. Wanatumiasana marimba, ngoma zenye asili ya Tanzania, Djembe kutoka Afrika ya Magharibi, zeze na ala za muziki wa dansi kama gita na kinanda.

    COCODO waliwahi kushiriki kwenye tamasha la ZIFF na pia kwenye kongamano la Smart Partnership Dialogue huko Dar es Salaam na Sauti za Busara 2015.

    Nyimbo yao inayoitwa ‘Gwe Mwana” ilipata umaarufu mkubwa nchini na hata ilitumika kwenye filamu ya ‘Sunshine”.  Na mwaka 2014 nyimbo hiyo ilipendekezwa kama ni nyimbo bora ya muziki wa asili kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award.  Video ya Mpola Mpola, ilipendekezwa na kuonyeshwa kwenye matamasha tofauti ya filamu, nchini.Wanakikundi hichi ni cha wanafunzi katika chuo cha CEFA, Tanzania.  Wanasomea muziki kwa muda wa miaka mawili.