4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Hoko Roro
Results: 1 to 1 of 1
 • Hoko Roro

  Country  Tanzania
  Genres acoustic fusion
  FestivalSauti za Busara 2014

  Hoko Roro at Sauti za Busara 2014, Zanzibar - Tanzania

  Hoko Roro
  Hoko Roro

  Kundi la Hoko Roro limeanzishwa na kijana mwenye kipaji ajulikanaye Samuel Hoko Roro ambaye alizaliwa mwaka 1990 katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Samuel alianza kuimba alipokuwa na umri wa miaka minane, alikuwa anaimba Nyumbani, Shule na Kanisani.
  Samuel alikuwa anajiuliza mwenyewe ni lini ndoto yake ya kumiliki bendi itatimia. Mwaka 2006 alikwenda kwenye kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha “Dogodogo Center” alifanikiwa kupata mafunzo ya muziki ikiwemo kucheza na kupiga vifaa vya muziki. Hapo ndipo alipopata nafasi ya kujifunza kupiga Gitaa. Kwa kuwa Samuel alikuwa makini darasani aliweza kufanya vizuri kwenye masomo yake na tangu alipomaliza masomo yake mwaka 2008 aliendelea na masuala ya muziki kwa muda wote.
  Mwaka 2011 nyota yake ilianza kun’gaa alichaguliwa kushiriki kwa mara kwanza kwenye tamasha la “Visa2Dance” na mwaka huo huo alipata safari ya kimuziki nchini Unganda na Ujerumani na kundi la Lumumba theatre nako alipata mafunzo zaidi.
  IMwaka 2012 alijaribu kutaka kujiendeleza kwenye fani yake ya muziki alikwenda kwenye chuo cha muziki Zanzibar “Dhow Country Music Academy” (DCMA) lakini alishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukata wa ada ndipo alipoamua kurudi Dar es Salaam kuendelea na masuala yake ya muziki kama kawaida.
  Mwaka 2013 ndoto ilitimia kwa kuanzisha bendi yake ijulikanayo Hoko Roro pamoja na wasanii wenzake kama Mohammed Twaba, Ilali Mohammed na yeye mwenyewe.