4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Isabel Novella
Results: 1 to 1 of 1
  • Isabel Novella

    Country  Mozambique
    Genres roots pop fusion
    Website /isabelnovellaOfficial
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Isabel Novella (2012)

    Introducing Isabel Novella

    Isabel Novella
    Isabel Novella

    Akiwa amezaliwa Maputo, Msumbiji na kukulia katika majukwaa ya muziki sehemu tofauti duniani, Isabel Novella amebarikiwa na kipaji kutoka kwa mungu: sauti ya kuimba, pamoja na kuwa muimbaji na mwandishi mzuri, ana uwezo wa kutosha wa kumiliki jukwaa. Akiwa na staili na utumbuizaji wa kipekee, Isabel amejitengenezea nafasi yake kama mtumbuizaji na msanii wa kurekodi, akizagaa katika muziki wa bossa jazz, marrabenta-bossa, upbeat reggaeton na Afro soul; Isabel ameunda aina ya muziki kwa ajili yake - ‘pop-world soul’.

     

    Ufunuo wa Isabel Novella kama msanii wa kimataifa anayetumbuiza na kuonekana katika rekodi zake, ukimualika kurekodi hutokea kama vile anatumbuiza kwenye hadhira. Sauti za weusi na milio mizuri ambayo inafanya muziki wakiafrika kama uliovunwa kutoka makanisani, harusini na au sherehe mbalimbali za kimila ambazo zinapenya katika muziki wake wote wakati anafanya majaribio na vifijo, mfano wa melodi za muziki wa trance unaoamsha ngoma za kale.

     

    Tangu akiwa na umri mdogo, Isabel Novella alijenga mapenzi katika sanaa na akiwa na miaka mitano tu tayari alikua ameshashiriki katika TV, vipindi vya redio na matamasha. Alitunga nyimbo ya kwanza akiwa na miaka kumi. Wakati alipofikisha miaka 14, Isabel alianza kuimba kama kazi kwa kuwa muimbaji msaidizi katika makundi tofauti nchini Msumbiji, Afrika kusini na Uholanzi. Tangu mwaka 2005 Isabel Novella ameshashiriki kwenye Neco Novellas (bendi yake ya familia) katika zaidi ya matamasha ya jazz zaidi ya 50 duniani huko Uholanzi, Ufaransa, Ujerumani, Bulgaria, Belgium, Luxembourg, Cape Verde na Afrika Kusini.

     

    Kuhusu muziki wake, Isabel Novella anasema: ‘Awali ya yote nataka kufika na kugusa watu wengi kadri ninavyoweza kwa muziki na ujumbe wangu. Lugha kwa urahisi katika uandishi wangu kwa vile ninapenda kuchanganya kireno, kiingereza na lahaja kutoka nyumbani. Ninaamini sio lazima kila mara uelewe mashairi katika nyimbo ili upende nyimbo, na ninataka watu pia wahisi ninachofanya. Nimekua nikisikiliza na kupata hamasa za aina tofauti za muziki, kuanzia muziki wa roots kama vile wenye mahadhi yaki tamaduni za kiafrika na ule wa magharibi (soul, jazz, funk, classic, world….) Ninapotengeneza muziki wangu, akili yangu huruka katika aina zote hizi na ninajikuta nikizichanganya. Unaweza kucheza/kuimba/kulia/kufikiri/kuhisi au ukasikiliza tu na kuburudika!’

    LOGO-FUNDAC
    with support from FUNDAC