4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Jagwa Music
Results: 1 to 1 of 1
 • Jagwa Music

  Country  Tanzania
  Genres coastal roots urban
  Website www.jahazi-media.com
  FestivalSauti za Busara 2005, 2006, 2009, 2011, 2012, 2017
  Recordings

  Bongo Hotheads, 2013

  Jagwa Music - "Mpango Mzima" (live at Roskilde)

  Jagwa Music
  Jagwa Music

  Kikundi cha Jagwa kinakusanya wasanii tisa ambao ndio viranja wa muziki wa mchiriku.  Muziki huu ulianza miaka ishirini iliyopita mitaani Dar es Salaam.  Walianza muziki kwa kutumia kinanda cha Casio na ghafla kuwa na washabiki wengi wa aina ya muziki wao.  Tangu miaka hiyo mchiriku umekuwa ukikuwa na kupendwa zaidi Tanzania na kupendwa hata nchi nyenginezo ambapo Jagwa huwa wanatembelea. Vyombo vya habari vya hapa nchini vimekuwa vinaudharau na kutoupa sifa inayostahili kwa sanaa hii, wanaona kama ni uhuni na sio sanaa.

  Karibia watu wote wanaoishi Dar es Salaam wanazipenda nyimbo zinazoimbwa na Jagwa, na utakuta mashairi ya nyimbo zao yameandikwa kwenye madaladala.  Mashairi haya yanagusia maisha ya jijini unapokabiliwa na taabu na ukosefu wa kazi, yanagusia uonevu kwenye familia, pia kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi na maisha ya ukapera.

  Jagwa wameshiriki kwenye matamasha maarufu ya muziki duniani kama vile, tamasha la WOMEX, tamasha la WOMAD nchini Uingereza, tamasha la Roskilde la nchini Denmak na pia wameshiriki huko Marekani kwenye tamasha lijulikanalo kama Centre Stage.