4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Jembe Culture Group
Results: 1 to 1 of 1
 • Jembe Culture Group

  CountryTanzania
  Genrestraditional
  FestivalSauti za Busara 2012
  Jembe Culture Group
  Jembe Culture Group

  Kundi lilianzishwa rasmi mwaka 2006 na vijana watatu kutoka katika mkoa wa Dodoma wanaume wawili na mwanamke mmoja katika jiji la Dar es Salaam.

  Mwaka 2009 waliongezeka watu watatu zaidi na kufikia watu sita ndani ya mwaka mmoja baadae ikafikia idadai ya watu 13 ambao ndio wapo na kikundi mpaka sasa . kikundi makazi yake makuu ni Dar es salaam katika kitongoji cha Mbezi na hufanya maonyesho yao katika kijiji cha makumbusho mara mbili kwa wiki.

  Kundi limefanikiwa kurekodi albamu yake mnamo mwaka 2010 na bado wapo katika harakati za kurekodi video.

  Kundi linatumia vifaa tofauti vinavyotumiwa kabila la wagogo kutoka Dodoma kama malimba, zeze, manyanga, njuga na aina tofauti ya ngoma.