4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Joe Driscoll and Sekou Kouyate
Results: 1 to 1 of 1
  • Joe Driscoll and Sekou Kouyate

    Country  USA Guinea
    Genres roots reggae fusion
    Website joeandsekou.com
    FestivalSauti za Busara 2014
    Recordings📼

    Faya, 2012

    Joe Driscoll & Sekou Kouyate 'Wonamati'

    Joe Driscoll and Sekou Kouyate
    Joe Driscoll and Sekou Kouyate

    Katika Mji wa Marseilles, mji ambao wenye vipaji vingi vilivyohamia kutoka sehemu mbalimbali duniani na ambapo Joe Driscoll na Sekou Kouyate walikutana kwa mara ya kwanza. Wawili hao walikutana kwenye tamasha la "Nuit Metis" kulikuwa na kikwazo cha lugha lakini waliweza kufanya kitu ambacho kiliweza kurahisisha mawasiliano kupitia muziki. Baada ya kipindi kifupi waliweza kutambuana kwamba wanaweza kubuni muziki kutokana na tamaduni zao Sekou ana asili ya Guinea, ambako alikulia kwenye familia ya muziki wa asili. Nchini Ufaransa anajulikana kwa jina la utani kama "Jimi Hendrix wa Kora" kutokana na aina yake ya kipekee ya upigaji na uwezo wake wa ubunifu. Amezunguka sehemu nyingi za dunia akiwa katika bendi ya Ba Cissoko iliyojumuisha ndugu zake wengi. Joe Driscoll, naye amefanya ziara nyingi za kimuziki akitambulisha muziki wake wa fusion na hip hop. Kutokana na mapinduzi ya sasa ya kiutaalam, yalipelekea kufanya maonyesho akiwa peke yake jukwaani. Alishafanya maonyesho kwenye matamasha mbalimbali kama Electric Picnic nchini Ireland na Lake of Stars nchini Malawi. Baada ya kuwa pamoja kwa muda wa wiki waliweza kutoka na kitu cha pamoja kilichowaunganisha kama ndugu. Hatimaye kutoka na albamu yenye mchanganyiko wa afrobeat, hip hop, folk na Rege. Kouyate and Driscoll wameunganisha mipaka yao, na kunukuu maneno ya mwanafalsafa Louis Armstrong "Kuna aina mbili ya muziki: Mzuri na mbaya."

    From-the-American-People
    With thanks to the US Embassy